- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Habari Jamiichek
Kwa muda sasa katika Jamii yetu ya Kiswahili kumekuwa na hii nadharia kwamba mwanaume akitumia pombe Kali Aina ya konyagi au k vant halafu akaenda kufanya mapenzi, hutumia muda mrefu Sana kufika mshindo kitu ambacho inasemekana kinaridhisha wanawake kiurahisi.
Huku mitaani, nimeshuhudia vijana wengi wakiingia katika mkumbo huu wa matumizi ya pombe Kali kwa lengo wakashiriki mapenzi na wanawake zao na kuthibitisha uanaume wao, tena kulingana na wimbi kubwa la tatzo la upungufu wa nguvu za kiume imefanya pombe hizi kupendwa na vijana wengi zaidi
Sasa ni vema Jamiichek na madaktari wa mambo ya uzazi hasa kwa wanaume mjitokeze mtoe ufafanuzi zaidi.
---
Chanzo cha picha: Getty Images
Kwa muda sasa katika Jamii yetu ya Kiswahili kumekuwa na hii nadharia kwamba mwanaume akitumia pombe Kali Aina ya konyagi au k vant halafu akaenda kufanya mapenzi, hutumia muda mrefu Sana kufika mshindo kitu ambacho inasemekana kinaridhisha wanawake kiurahisi.
Huku mitaani, nimeshuhudia vijana wengi wakiingia katika mkumbo huu wa matumizi ya pombe Kali kwa lengo wakashiriki mapenzi na wanawake zao na kuthibitisha uanaume wao, tena kulingana na wimbi kubwa la tatzo la upungufu wa nguvu za kiume imefanya pombe hizi kupendwa na vijana wengi zaidi
Sasa ni vema Jamiichek na madaktari wa mambo ya uzazi hasa kwa wanaume mjitokeze mtoe ufafanuzi zaidi.
---
Chanzo cha picha: Getty Images
- Tunachokijua
- Pombe ni aina ya kinywaji kinachotengenezwa kwa mchanganyiko wa vitu mbalimbali ukiambatana na kilevi Cha kiwango tofauti tofauti. Pombe zipo za aina nyingi na zinatofautiana kiwango cha vilevi huku pombe aina ya wiski ambazo ndizo zinazosifika kwa kuwa na kiwango kikubwa cha vilevi. Watu wamekuwa wakinywa kwa kiwango tofauti tofauti na kwa malengo tofauti.
Kumekuwa na hoja kutoka kwa baadhi ya wanajamii wakiamini kwamba unywaji wa pombe unasaidia kuongeza nguvu za kiume kwa wanaume.
Baadhi ya Wamaume wamekuwa wakinywa pombe kabla ya tendo wakiamini inawaongezea Uwezo na ufanisi wa kushiriki mapenzi na wenza wao.
Je, kuna ukweli wowote kuhusu hoja hii?
Katika kutafuta ukweli wa hoja hii JamiiCheck imepitia vyanzo mbalimbali pamoja na kuzungumza na Wataalamu wa Afya.
Mathalani JamiiCheck imepitia ukurasa wa Dimedic EU (Watoa huduma za Kliniki za mtandaoni ndani ya Umoja wa mataifa ya Ulaya) wanakanusha pombe kuongeza nguvu za kiume kwa kueleza namna inavyoweza kuleta athari hasi kwa mwanaume katika kushiriki kufanya mapenzi.
Wakifafanua hoja hii Dimedic wanaeleza:
Matumizi ya pombe kupita kiasi yanaweza kusababisha madhara hasi kwenye uwezo wa kushiriki mapenzi kwa mwanaume. Inaweza kusababisha kuchelewa au kuzuia kabisa uume kusimama. Pia pombe inaathiri vibaya hamu ya ngono na hali ya akili ya mwanaume. Pombe nyingi huleta msongo wa mawazo, hofu, na hali za unyonge wa akili, ambazo huathiri ufanisi wa ngono kwa Mwanaume.
Nao ukurasa unaochambua na kufanya masuala ya Afya wa Healthline unatoa ufafanuzi unaendana na Dimedic, ambapo pia wanaeleza kuwa matumizi ya pombe yaliyopitiliza yanaweza kusababisha athari ya nguvu za kiume kwa mwanaume (kushindwa kusimamisha).
Wakieleza hoja yao Healthline wanasema:
Pombe huweza kuathiri uwezo wa Mwanaume kusimamisha uume wakati wa tendo. Pombe huathiri kiwango cha homoni, mfumo wako wa neva, na mzunguko wa damu.Kunywa pombe kwa muda mrefu pia kunaweza kusababisha matatizo ya nguvu za kiume ya muda mrefu pia.
Zaidi ya hayo JamiiCheck imezungumza na Dkt. Godfrey Chale (Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake) aliyefafanua kuwa Unywaji wa Pombe Kali kama K Vant hauongezi nguvu za Kiume bali unatanua mishipa ya damu, hivyo mzunguko wa damu unakuwa mkubwa zaidi na kufanya uume kusimama.
"Kutokana na athari ya pombe kali kuongeza joto la mwili na kuongeza mzunguko wa damu, hivyo kusaidia kusimamisha uume. Unapotumia pombe kali unatanua mishipa ya damu nakufanya mzunguko wake unakuwa una nguvu zaidi.
Hili linatokea kwa muda mfupi kwa Mtu ambaye hana shida ya nguvu za kiume na sio kwamba ni mbadala wa kuongeza nguvu za kiume. Ndio maana Nchi kama Urusi na Italia kwenye baridi hutumia pombe kwa ajili ya kupata joto na sio mbadala wa kuongeza nguvu za kiume kwa sababu haileti athari hiyo.
Anayekunywa pombe kupita kiasi hawezi kusimamisha kwa muda mrefu, kwa sababu pombe huchosha mwili hivyo hataweza kufanya kitu chochote' amesema Dkt. Chale
Hivyo, kutokana na ufafanuzi huo kutokea kurasa zinazofafanua masuala ya Afya pamoja na ufafanuzi wa Mtaalamu wa Afya JamiiCheck inaona kuwa hoja inayodai kuwa pombe inasaidia kuongeza nguvu za kiume haina ukweli.