UZUSHI Unywaji wa pombe Kali kama konyagi na K Vant huongeza nguvu za kiume

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Habari Jamiichek

Kwa muda sasa katika Jamii yetu ya Kiswahili kumekuwa na hii nadharia kwamba mwanaume akitumia pombe Kali Aina ya konyagi au k vant halafu akaenda kufanya mapenzi, hutumia muda mrefu Sana kufika mshindo kitu ambacho inasemekana kinaridhisha wanawake kiurahisi.

Huku mitaani, nimeshuhudia vijana wengi wakiingia katika mkumbo huu wa matumizi ya pombe Kali kwa lengo wakashiriki mapenzi na wanawake zao na kuthibitisha uanaume wao, tena kulingana na wimbi kubwa la tatzo la upungufu wa nguvu za kiume imefanya pombe hizi kupendwa na vijana wengi zaidi

Sasa ni vema Jamiichek na madaktari wa mambo ya uzazi hasa kwa wanaume mjitokeze mtoe ufafanuzi zaidi.
---
1713826611277.png

Chanzo cha picha: Getty Images
 
Tunachokijua
Pombe ni aina ya kinywaji kinachotengenezwa kwa mchanganyiko wa vitu mbalimbali ukiambatana na kilevi Cha kiwango tofauti tofauti. Pombe zipo za aina nyingi na zinatofautiana kiwango cha vilevi huku pombe aina ya wiski ambazo ndizo zinazosifika kwa kuwa na kiwango kikubwa cha vilevi. Watu wamekuwa wakinywa kwa kiwango tofauti tofauti na kwa malengo tofauti.

Kumekuwa na hoja kutoka kwa baadhi ya wanajamii wakiamini kwamba unywaji wa pombe unasaidia kuongeza nguvu za kiume kwa wanaume.

Baadhi ya Wamaume wamekuwa wakinywa pombe kabla ya tendo wakiamini inawaongezea Uwezo na ufanisi wa kushiriki mapenzi na wenza wao.

Je, kuna ukweli wowote kuhusu hoja hii?
Katika kutafuta ukweli wa hoja hii JamiiCheck imepitia vyanzo mbalimbali pamoja na kuzungumza na Wataalamu wa Afya.

Mathalani JamiiCheck imepitia ukurasa wa Dimedic EU (Watoa huduma za Kliniki za mtandaoni ndani ya Umoja wa mataifa ya Ulaya) wanakanusha pombe kuongeza nguvu za kiume kwa kueleza namna inavyoweza kuleta athari hasi kwa mwanaume katika kushiriki kufanya mapenzi.

Wakifafanua hoja hii Dimedic wanaeleza:

Matumizi ya pombe kupita kiasi yanaweza kusababisha madhara hasi kwenye uwezo wa kushiriki mapenzi kwa mwanaume. Inaweza kusababisha kuchelewa au kuzuia kabisa uume kusimama. Pia pombe inaathiri vibaya hamu ya ngono na hali ya akili ya mwanaume. Pombe nyingi huleta msongo wa mawazo, hofu, na hali za unyonge wa akili, ambazo huathiri ufanisi wa ngono kwa Mwanaume.

Nao ukurasa unaochambua na kufanya masuala ya Afya wa Healthline unatoa ufafanuzi unaendana na Dimedic, ambapo pia wanaeleza kuwa matumizi ya pombe yaliyopitiliza yanaweza kusababisha athari ya nguvu za kiume kwa mwanaume (kushindwa kusimamisha).

Wakieleza hoja yao Healthline wanasema:

Pombe huweza kuathiri uwezo wa Mwanaume kusimamisha uume wakati wa tendo. Pombe huathiri kiwango cha homoni, mfumo wako wa neva, na mzunguko wa damu.
Kunywa pombe kwa muda mrefu pia kunaweza kusababisha matatizo ya nguvu za kiume ya muda mrefu pia.

Zaidi ya hayo JamiiCheck imezungumza na Dkt. Godfrey Chale (Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake) aliyefafanua kuwa Unywaji wa Pombe Kali kama K Vant hauongezi nguvu za Kiume bali unatanua mishipa ya damu, hivyo mzunguko wa damu unakuwa mkubwa zaidi na kufanya uume kusimama.

"Kutokana na athari ya pombe kali kuongeza joto la mwili na kuongeza mzunguko wa damu, hivyo kusaidia kusimamisha uume. Unapotumia pombe kali unatanua mishipa ya damu nakufanya mzunguko wake unakuwa una nguvu zaidi.

Hili linatokea kwa muda mfupi kwa Mtu ambaye hana shida ya nguvu za kiume na sio kwamba ni mbadala wa kuongeza nguvu za kiume. Ndio maana Nchi kama Urusi na Italia kwenye baridi hutumia pombe kwa ajili ya kupata joto na sio mbadala wa kuongeza nguvu za kiume kwa sababu haileti athari hiyo.

Anayekunywa pombe kupita kiasi hawezi kusimamisha kwa muda mrefu, kwa sababu pombe huchosha mwili hivyo hataweza kufanya kitu chochote
' amesema Dkt. Chale

Hivyo, kutokana na ufafanuzi huo kutokea kurasa zinazofafanua masuala ya Afya pamoja na ufafanuzi wa Mtaalamu wa Afya JamiiCheck inaona kuwa hoja inayodai kuwa pombe inasaidia kuongeza nguvu za kiume haina ukweli.
Haziongezi nguvu za kiume, zinaua ganzi viungo vya mwili kwahiyo sense zinachelewa kupata moto, wazungu wanakua mbali sana, usipovuta hisia game inaweza kuisha kichupa bado kina Mls za kutosha! Next time kajaribu JackDaniels.. utakuja kunishkuru!
 
Haziongezi nguvu za kiume, zinaua ganzi viungo vya mwili kwahiyo sense zinachelewa kupata moto, wazungu wanakua mbali sana, usipovuta hisia game inaweza kuisha kichupa bado kina Mls za kutosha! Next time kajaribu JackDaniels.. utakuja kunishkuru!
Kisayansi hii ipo?
 
What happens scientifically is that alcohol is one of the inhibitors of nerve impulse transmission. When a man takes more alcohol, the more it accumulates in synaptic clefts.

And sex pleasure is largely relying on nerve impulses, if poorly transmitted it means low sense of pleasure is detected. Hence more time is needed for climax (orgasm) to be attained.
 
Na ndio uwe umepiga hayo mavyombo halafu ukatumia na yale maplastic utakesha ni balaa
 
Acha kuwatisha watu pombe ni zao la sayansi
Kunywa pombe ili uweze kufanya jambo fulani, kwa mfano kupoteza mawazo au kupata nguvu ni kujenga dependency ya pombe; hilo ni jambo baya. Kunywa glass moja mbili kupoteza muda wakati wa maongezi na wenzako ni jambo la kawaida lakini siyo kunywa ili ikusaidiea kukamilisha jambo ambalo huwezi kulikamilisha bila kunywa.
 
Hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha kwamba matumizi ya pombe kali kama Konyagi au K Vant huongeza uwezo au muda wa kufika mshindo wakati wa tendo la ngono. Kinyume chake, matumizi ya pombe kwa kiasi kikubwa mara nyingi yana madhara kwa afya ya ngono. Pombe inaweza kusababisha kupungua kwa uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na pia inaweza kuathiri utendaji kazi wa neva na misuli, ambayo inaweza kusababisha utendaji hafifu wakati wa tendo la ngono.

Madhara ya pombe kwa uwezo wa kijinsia yanategemea mambo kadhaa kama vile kiasi cha pombe kinachotumika, afya ya mtu, na mara ngapi mtu anatumia pombe. Matumizi ya mara kwa mara ya pombe kali yanaweza kuwa na matokeo hasi kama vile:

1. Upungufu wa Nguzu za Kiume: Pombe inaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume kwa muda mrefu, na kusababisha shida za kisaikolojia na kimwili.
2. Kuchelewa au Kushindwa Kufika Kileleni: Ingawa baadhi ya watu wanaweza kuhisi kwamba pombe inawasaidia kuchelewesha mshindo, kwa wengine, pombe inaweza kusababisha kushindwa kabisa kufika kileleni.
3. Madhara ya Afya ya Akili: Pombe pia inaweza kuathiri hali ya akili, kusababisha hisia za huzuni au wasiwasi, ambazo zinaweza kuathiri utendaji wa tendo la ngono.

Ni muhimu kuzingatia kwamba kuna tofauti kubwa kati ya matumizi ya pombe kwa ajili ya kujiburudisha na matumizi yake yasiyo salama au yenye madhara. Ni vyema kushauriana na wataalam wa afya au washauri iwapo mtu anahisi ana tatizo kwenye masuala ya nguvu za kiume kuliko kutumia pombe kama suluhisho la muda mfupi ambalo lina madhara makubwa baadae.
 
Pombe kali huwa zinakata mawasiliano au kupunguza.
Ndio maana ukizipiga sana unaweza kushindwa hata kusimamisha kwa wakati.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom