Ukweli ni lazima usemwe, natafuta mrembo wa kuzeeka naye. Mapungufu yangu haya Hapa

Heci

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
3,485
5,821
Umri wangu ni miaka 45, Hali yangu ya kindoa ni mtalaka, watoto wanne, Kila mmoja na mama yake, na watoto wote wako kwa mama zao.

Kazi nafanya, Hela napata, pombe nakunywa. Mambo ya mabebzi labda itokee tu, wana gharama sana na Mimi ni bahili sana.

Mwanamke ninayemtaka awe na sifa zifuatazo, anivumilie Mimi na mapungufu yangu.

Nitaweka Kila kitu ndani, kifurushi kikubwa cha DSTV, umeme wa kutosha, vyakula na Kila kitu.

Mke atapewa pocket money ya sh. 250,000/ kwa mwezi. Gari sina, ukiniona naendesha ujue ni la ofisi. Usiahoboke nalo.

Wadada karibuni sana, single mothers watapewa kipaumbele.
Elimu Yako kaa nayo hukohuko, hata ukiwa na PhD Yako, kwangu wewe ni mke tu sawa na wa darasa la saba. Zingatia sana hili kabla hujaja PM.
Namba ya simu itapatikana PM.
 
Watoto wanne kila mmoja na mama yake.
Ina maana umeachana na wanawake wanne Ila wa tano mtawezana.
Bro. Jipime Tena.
Halafu Tsh 250,000 huyo mwanamke atakwenda saluni gani ili umpende zaidi?
Ubahili na wanawake wanaojielewa havikai nyumba moja.
 
Umri huo stick kwa single mom hutajuta, tena awe 32+, wote mnaingia dimbani na GG, mtaendana.

Msaidie jambo moja hapo kwa singo maza nae hajaliweka wazi....

Singo maza atakuja kuishi kwake na watoto wake ilhali watoto wa jamaa wanaishi na.mama zao na anawahudumia huko waliko.

Je watoto wa singo maza watahudumiwa na singo maza mwenyewe kwa posho ya laki 2.5 au singo maza apambane na watoto wake mwenyewe...?

Aje nao mjengoni au awaache kwa bibi yao?

Ila watoto wanaathirika sana na ngono zinazoishia kutunga mimba halafu baba na mama wa mtoto wanashindwana kuishi na kulea mtoto/watoto pamoja....

Basi tuu ila, nafsi nyingi sana za watoto zinauchungungu wa maisha tangu wadogo.
 
Ni bora kubaki single kuliko kulea bao la mwanaume/wanaume wenzako

Siku ukiwa unaoa nenda kamwambie mama au dada zako unaoa single maza watasikitika na kukushangaa sana

Hata kama mama yako alikulea akiwa single maza hakuna siku atakuuunga mkono uoe single maza mwenzake anaweza akalia sana

Ndio ujue wanawake wanajuana

Mungu naye akiwa mbinguni anakushangaa amemuagiza mwanaume aanzishe familia yake wewe unaenda kujiunga kwenye familia ya mwanaume mwenzako!

Imagine siku umemuoa single maza halafu unawatembelea wazazi wako ukiwa na watoto wa mwanaume mwenzako. Then unawaambia watoto wa mwanaume mwenzako msalimie bibi na babu yenu. Lazima baba yako na mama yako wakuone mpumbavu na mjinga, a useless son.

Learn or perish
 
Umri wangu ni miaka 45, Hali yangu ya kindoa ni mtalaka, watoto wanne, Kila mmoja na mama yake, na watoto wote wako kwa mama zao.

Kazi nafanya, Hela napata, pombe nakunywa. Mambo ya mabebzi labda itokee tu, wana gharama sana na Mimi ni bahili sana.

Mwanamke ninayemtaka awe na sifa zifuatazo, anivumilie Mimi na mapungufu yangu.

Nitaweka Kila kitu ndani, kifurushi kikubwa cha DSTV, umeme wa kutosha, vyakula na Kila kitu.

Mke atapewa pocket money ya sh. 250,000/ kwa mwezi. Gari sina, ukiniona naendesha ujue ni la ofisi. Usiahoboke nalo.

Wadada karibuni sana, single mothers watapewa kipaumbele.
Elimu Yako kaa nayo hukohuko, hata ukiwa na PhD Yako, kwangu wewe ni mke tu sawa na wa darasa la saba. Zingatia sana hili kabla hujaja PM.
Namba ya simu itapatikana PM.
Kabisa.......
Kama kuna mwanamke wa hivyo aje pm
Inshallah
 
Wanaume sometimes tunazingua sana.

Kwahy jamaa umeacha wanawake wako wanne wenye watoto na bado unatafuta wa tano umzalishe ili nae umuache utafute wa sita.?

Naomba niishie hapa mana ntazidi kukuona ww ni mpumbavu tangu siku ya kwanza kuzaliwa.

Mpaka hapo naomba nikuambie tuu ww mtoa mada ni mpumbavu kama wapumbavu wengine.
 
Aiseee! Umeamka na matusi leo
Unaweza kutoa maoni bila kumfanya mtu ajisikie vibaya,..Inawezekana
 
Watoto wanne kila mmoja na mama yake.
Ina maana umeachana na wanawake wanne Ila wa tano mtawezana.
Bro. Jipime Tena.
Halafu Tsh 250,000 huyo mwanamke atakwenda saluni gani ili umpende zaidi?
Ubahili na wanawake wanaojielewa havikai nyumba moja.
Yaani kwako wewe laki 2.5 za kupewa na mwanaume hauwezi kwenda salon ukapendeza?

Basi jigharamie kwa kipato chako cha mshahara kisha uje na ushahidi wa receipt halali za huduma ili tuutathimini ukweli wako.

Humu Jf watu tunajikweza sana lakini kiuhalisia wengi wanaishi maisha hohehahe.
 
Back
Top Bottom