Case Study: Kaka Yangu hana marafiki hata wa kumtembelea, ni super introvertm Baba alimlea kwa namna aliyodhani itamlinda kumbe ni kumletea matatizo

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,407
19,047
Na mimi nililelewa kwa staili hii lakini nilipokuja kuona tunaishi tofauti na jamii nilimkaidi mzee na ndio ponea yangu, (nilishaweka uzi huu).

Ipo hivi yani, Mzee ni mtu ambae alikuwa anatulea katika mtindo ambao ulitufanya tuwaone watu nje ya familia kama vile hawahitajiki.
  • Kufungiwa ndani, yani geti kali hakuna kutoka.
  • Hakuna kucheza na watoto wengine hata uwanja wa karibu ama nje ya geti
  • Hakuna kuingiza marafiki ndani,
  • Kila mara kutuasa kwamba watu ni wabaya hawaaminiki bila kutuelimisha ni vipi tunakabiliana na huo ubaya zaidi ya kufungiwa ndani tu.
Kaka alikuwa anatii sana hizi, binafsi sikuona faida nilianza kutoka sana nje mzee akaanza kupewa taarifa mtoto wako tulimuona anacheza mpira nje, tulimkuta anacheza na wenzake nyumba flani, n.k basi nilikuwa nachapwa sana, gari iliyokuwa inatufata niliigomea maana ni watu wanne tu tulikuwa tunafatwa na magari darasa zima lenye watu 40, niliona iko poa zaidi kuongozana na wenzangu wengine wakiwa majirani, n.k.

Basi kaka yangu alikolezwa sana na hayo malezi kiukweli kawa hawa mnaowaita ma introvert, ni mtu wa kupenda sana kukaa peke yake, Nyumbani kwake hakunaga wageni kabisa labda iwe ni wale wa upande wa mke wake tu.

Ugeni katika kuishi na watu kwa kukosa mwanya huo akiwa mtoto umemfanya apitie mengi mazito, katika kujaribu hivi ukichanganya na ugeni wa urafiki kajikuta mara kadhaa akigeuzwa kuwa ngazi bila kujua anatumika tu, mbaya zaidi alipopata hata rafiki alikuwa ni kunganganizi sana hata rafiki yake wakigombana yeye anatumia nguvu sana kumbembeleza na kuomba msamaha, hii ilifanya wahuni kumtumia kirahisi

vitu vinahitaji kiasi chake, ukizidisha unaharibu,

Maisha ni kama baiskeli, unapomfundisha mtoto kuiendesha kuna muda unamshika kuna muda unamwachia kidogo, akitaka kudondoka unamshika, ivo ivo mpaka huku ukubwani tayari anajua kuendesha baiskeli bila kushikiliwa,
 
Na mimi nililelewa kwa staili hii lakini nilipokuja kuona tunaishi tofauti na jamii nilimkaidi mzee na ndio ponea yangu.

Ipo hivi yani, Mzee ni mtu ambae alikuwa anatulea katika mtindo ambao ulitufanya tuwaone watu nje ya familia kama vile hawahitajiki...
Hongera kwako mkuu
 
Marafiki ama maisha smt Ni automatic yanatokea na sio kufosi. People everywhere since ancient time are always Trading for profit gain.

None trade something just for you take his value or money.if it happens you take his value , money,gain anything is because they calculated right numbers but probability wasn't in their favour even though the odds were high
 
Na mimi nililelewa kwa staili hii lakini nilipokuja kuona tunaishi tofauti na jamii nilimkaidi mzee na ndio ponea yangu, (nilishaweka uzi huu)...
Nadhani mzee alikuwa sahihi japo kama binadamu kuna makosa alifanya.. Hakuna kitu kibaya kama kuwekeza kwa watu wanaoitwa marafiki alisimia 90 ni wanafiki,watakuwa na misaada myepesi kwako tena kwa mara moja.

Kuwa na marafiki lakini jifunze kujisimamia kwenye shida.

Wafundishe wano kuwa na marafiki lakini usisite kuwaambia ukweli rafiki ni nani na kwa wakati gani

Thread 'Marafiki wa kweli ni wa utotoni' Marafiki wa kweli ni wa utotoni.

FB_IMG_1684407215812.jpg
 
Nadhani mzee alikuwa sahihi japo kama binadamu kuna makosa alifanya.. Hakuna kitu kibaya kama kuwekeza kwa watu wanaoitwa marafiki alisimia 90 ni wanafiki,watakuwa na misaada myepesi...
Alikuwa mgeni sana hata kwenye mambo ya urafiki, uwezo wake mdogo wa kujua kuishi na watu ushamfanya atumike kirahisi kwa kujaribu kuanzisha urafiki, kuna ile mtu anakuganda sana sasa kwa baadhi ya hao aliowahi kuwa nao marafiki wakaanza kum blackmail afanye mambo yao ili urafiki uendelee. kiufupi hata elimu ile ya kujua vya kukwepa kwa watu kaja kuijua ukubwani sana baada ya kutumika sana.
 
Alikuwa mgeni sana hata kwenye mambo ya urafiki, uwezo wake mdogo wa kujua kuishi na watu ushamfanya atumike kirahisi kwa kujaribu kuanzisha urafiki, kuna ile mtu anakuganda sana sasa kwa baadhi ya hao aliowahi kuwa nao marafiki wakaanza kum blackmail afanye mambo yao ili urafiki uendelee. kiufupi hata elimu ile ya kujua vya kukwepa kwa watu kaja kuijua ukubwani sana baada ya kutumika sana.
Learned a hard way.. Akili yake ilichelewa kupevuka
 
Sometimes geti kali Ni muhimu sana kwa watoto
Kitu kikizidishwa zaidi kina madhara, inabidi iwe kawaida tu, geti kali kiasi ila kucheza maeneo ya karibu unapoweza kumuona unaacha tu nae afurahi,
 
Na mimi nililelewa kwa staili hii lakini nilipokuja kuona tunaishi tofauti na jamii nilimkaidi mzee na ndio ponea yangu, (nilishaweka uzi huu)

Ipo hivi yani, Mzee ni mtu ambae alikuwa anatulea katika mtindo ambao ulitufanya tuwaone watu nje ya familia kama vile hawahitajiki,

-Kufungiwa ndani, yani geti kali hakuna kutoka.
-Hakuna kucheza na watoto wengine hata uwanja wa karibu ama nje ya geti
-Hakuna kuingiza marafiki ndani,
-Kila mara kutuasa kwamba watu ni wabaya hawaaminiki bila kutuelimisha ni vipi tunakabiliana na huo ubaya zaidi ya kufungiwa ndani tu,

Basi kaka yangu alikolezwa sana na hayo malezi kiukweli kawa hawa mnaowaita ma introvert, ni mtu wa kupenda sana kukaa peke yake, Nyumbani kwake hakunaga wageni kabisa labda iwe ni wale wa upande wa mke wake tu.

Ugeni katika kuishi na watu kwa kukosa mwanya huo akiwa mtoto umemfanya apitie mengi mazito, katika kujaribu hivi ukichanganya na ugeni wa urafiki kajikuta mara kadhaa akigeuzwa kuwa ngazi bila kujua anatumika tu, mbaya zaidi alipopata hata rafiki alikuwa ni kunganganizi sana hata rafiki yake wakigombana yeye anatumia nguvu sana kumbembeleza na kuomba msamaha, hii ilifanya wahuni kumtumia kirahisi

Sawa najua hata mimi marafiki ni moja ya watu wasaliti wanaoweza kukuharibia maisha yako lakini pia najua kwamba watu ndio wametuzunguka na kuna umuhimu wa kujua kuishi na watu, sio lazima mtu awe rafiki ila kujua tu namna ya kuishi nae kunaweza kuwa na msaada mkubwa kuliko kutojua kuishi nao na kuwazuia kwa kuwa introvert.

Mimi niseme tu kwamba malezi nayo yanachangia sana kumfanya mtu awe introvert, dunia hii iliyojaa watu ukimzuia mtoto kujifunza kuishi na watu ni hatari mno kwake kuzidi faida utayopata kwa kumuwekea vizuizi.
Dah na mimi ngoja niokoteze hapa coz sina rafiki na hata nnapokaa ni mwaka wa 5 huu hakuna hata mtu wa kazin kwang au jirani aliyewahi kuingia kwangu ni salaam bas.

Huenda nikawa naonekana mkimya sana au dharau kwa baadhi ya watu but mtu akiwa ananiongelesha sana huwa napenda kumsikiliza tu na akifos niwe naongea naanza kujiskia vibaya mno na kujihis hasira juu.

Nmejtahid sana kuchange ila nmeangukia kufeli
 
Kaka ako ana Hasara chache kuliko Faida,huwezi ziona kwa macho lakini kwa maisha ya kaka ako

Faida zake ni nyingi sana,introvert hufanya mambo yao wenyewe wakiamini hawana mahali wanaweza

pata msaada hii hupelekea akili yao kufanya mambo kwa usahihi kwa asilimia 70 kwani hawana muda wa kusahihisha

Unatakiwa usimuonee huruma kaka ako bali umpongeze kwani kuna siku 1 itafika utagundua alikua sahihi sana kuishi namna anavyoishi sasa.
 
Kitu kikizidishwa zaidi kina madhara, inabidi iwe kawaida tu, geti kali kiasi ila kucheza maeneo ya karibu unapoweza kumuona unaacha tu nae afurahi,
Tatizo hilo wala hajasababisha faza ako bali Ni jinsi alivyoumbwa kakako manake Mimi nilikuwa geti kali lakini shuleni nilikuwa na marafiki vivyo hivyo mpaka secondary na kuendelea yaani nikifika home mimi geti kali ila nikifika school na change...
 
Hii ni tabia tu hata mngeachiwa huenda asingekuwa anajichanganya.

Watoto wanafungiwa ndani na mbwa wakali na bado unaambiwa mwanao J2 kaonekana kibaha huko ni mcheza mpira, ukija kufuatilia ndiye kapten wa timu baba hujui hata kama ni mchezaji.
 
Unaweza kuishi maisha hayo ila katika mazingira ya shule na kazi ukawa mtu tofauti pia
 
Back
Top Bottom