Uhusiano na mahusiano

Nov 6, 2016
62
163
TOFAUTI KATI YA UHUSIANO NA MAHUSIANO

Na Comrade Ally Maftah
JITU LA MIRABA
CHALINENEE

Kuna changamoto kubwa binadamu anaipata nanapojikuta katika uhusiano badala kuwa na mahusiano, kwa tafsiri isiyo rasmi, natumia lugha ya picha kuelezea mazingira ambayo unajikuta unampenda mtu kuliko anavyokupenda wewe, au unamuhitaji kuliko anavyo kuhitaji wewe, ukijikuta katika mazingira ya hivi jua kwamba tayari unaelekea kujisononesha nafsi yako.

Kuna wakati unalazimika kuwa katika mahusiano ya hivyo ukiwa unasubiri kukubalika, fanya hivyo kwa kipindi unachokuwa umejiwekea ambacho unaweza kuwa katika hali ya uvumilivu, kila mwanadamu ana kiwango chake cha muda wa kuvumilia ( torerance period ) ikipita kipindi hicho bado mtu hajakupokea moyoni ebu tafuta mbadala.

Nilidhamilia kuzungumzia topic hii katika mahusiano ya kimapenzi na ndio msingi wa fikra zangu lakini wakati naandika nimegundua kwamba hili lipo hata katika mahusiano ya kirafiki, kikazi na kibiashara.

Nilitathmini sana, kuna wakati unatafuta kuwa karibu na mtu fulani kwa malengo mazuri ya kisiasa, kibiashara, kikazi au kimapenzi lakini kila ukifanya jitihada unajikuta wewe ndio unalazimika kuyapalilia na kuyalinda mahusiano, yeye hana habari kabisa na wewe, utagundua kwa kutazama dalili za yeye kukuhitaji, utaona,

USHAURI WANGU-: DUNIA BADO INA FURSA NYINGI, USITUMIE MUDA WA KUPITILIZA KUMFANYA MTU AKUPENDE/ AKUKUBALI/AKUSIKILIZE, BADO KUNA WATU WANAWEZA KUKUPENDA ILA HUJAJIPA MUDA KUWAPA NAFASI

Ndimi Comrade Ally Maftah
JITU LA MIRABA
CHALINENEE

CHAMA CHA MAPINDUZI
JUMUIYA YA WAZAZI
BASATA
MAKTABA YA TAIFA
 

Attachments

  • 1714024089136.jpg
    1714024089136.jpg
    344.8 KB · Views: 3
Huyu jamaa ni mkabila sana hlf mahasira mengiiiii

Pita hivi na mada zako za ajabu ajabu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom