DOKEZO Sikonge: Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kiswahilini tunateseka kwa kukosa huduma muhimu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Nina kero kadhaa kuhusu Shule ya Msingi Kiswahilini inayopatikana Wilaya ya Sikonge, Kata Igigwa, Kijiji cha Tumbili, Kitongoji cha Kiswahilini yenye Wanafunzi 300 ina changamoto kadhaa

1. Mbali na kuwa na Wanafunzi 300, shule hiyo ya Mkoani Tabora ina matundu ya vyoo mawili tu tena yenye uchakavu, hata hivyo kuna matundu mengine 10 ambayo yamejengwa lakini hayajakamilika kwa muda wa miezi sita sasa.

Hivyo, Wanafunzi wote wanatumia matundu mawili jambo ambalo ni hatari kiafya.

2. Changamoto ya pili ni Walimu wa shule hiyo hawana vyoo vyao, hali mbayo inawafanya wawe wanaenda mtaani kupata huduma, wengine wanaenda vichakani, hiyo hali inaumiza sana.

3. Walimu wa hii Shule wanatembea umbali wa Kilometa 1.5 kwenda shule na wakati huohuo ikifika Saa Sita na Nusa Mchana wanarudi nyumbani kula na kurudi Saa Saba na Nusu ili kukamilisha muda uliobaki hadi saa kumi na nusu.

Tumeshafikisha malalamiko yetu kwa mamlaka husika lakini hakuna msaada wala majibu yoyote yanayotolewa ukizingatia shule ni mpya lakini bado imejengwa bila kuwepo kwa nyumba za Walimu na kuwafanya wawe wanaingia tu huku na huko.

Jambo lingine ni kuwa Shule hii yenye Darasa la Awali hadi la Tano ina jumla ya vyumba vya madarasa 3 tu, ambavyo vimejengwa kwa nguvu za Wananchi, kuna upungufu wa madarasa.
 
We mwalimu umelazimishwa?
Unakunya vichakani wanafunzi wako utawafundisha nini
 
Utamsikia makamba akasaini mktaba wa bilioni 75 za kukodi software kutokea India ya kufuatilia umeme kukatika. Mara atapiga tour na helicopter kucheki kina Cha maji.
Kuwa mwanasiasa na jambazi hawana tofauti kabisa. Wote wanaua watu ili wale ama waishi sema mwanasiasa anakuua taratibu mpaka kizazi Chako bila ya wewe kujua.
 
Back
Top Bottom