A
Anonymous
Guest
Kuna kero kubwa tunaipata Wazazi dhidi ya Shule ya Msingi Nyabulugoya iliyopo Nyegezi Jijini Mwanza, tunaomba tupazie sauti ili wenye nafasi zao wapate ujumbe huu.
Kila Jumamosi Wanafunzi wanaenda kufanyishwa mitihani kwa hela, imekuwa ni kitega uchumi cha Walimu.
Sasa hivi likizo ya wiki moja Watoto pia wanaambiwa waende tuition ya Shilingi 500 na ni lazima, tunakubali kuwa elimu ni ghali lakini Watoto pia wanahitaji kupumzika, sasa likizo ya one week tuition ya nini? Hii ni kero kwa kweli.
Itafika hatua akili za Watoto zitachoka kwa kuwa wanakosa muda wa kupumzika, muda wote ni kusoma na mitihai tu, hii sio sawa, Wizara ya Elimu ingalie hiki kinachoendelea, inawezekana sio hapa pekee.