Tetesi: Salim Abdallah ‘Try Again’ katika jaribio la kumng’oa Mo Dewj Simba!

Nifah

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
31,579
65,463
IMG_5241.jpeg


Moto unawaka SSC! Ni vita kubwa!
Klabu ya Simba ipo katika kipindi kigumu cha vita inayozidi kukomaa kila uchwao baina ya Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Simba Salim Abdallah Muhene Try Again dhidi ya Rais wa heshima wa Simba Mohamed Mo Dewj.

Wawili hao walianza kukosa maelewano baada ya Mo Dewj kuhamisha makazi yake nchini ambapo taarifa za uhakika ni kwamba anaishi Dubai hadi hivi sasa.

Baada ya Mo Dewj kuhamisha makazi uwekezaji wake Simba ulisuasua, ikitaarifiwa kumuachia mzigo mkubwa wa uendeshaji timu Try Again ambao ulimuelemea!

Try Again alijitahidi kadiri ya uwezo wake baada ya tajiri kujitenga kiaiana, akihaha huku na huko kutafuta namna ya kuinusuru Klabu ya Simba ambayo kwa msimu wa tatu sasa mfululizo imekuwa na matokeo ya kusuasua. Jitihada zake hizo zikionekana kuzaa matunda kwa kiasi kisichoendana na kipindi ambacho muwekezaji alikuwa ameshikilia usukani.

Try Again adhamiria mapinduzi, amlenga Said Salim Bakhressa!
Baada ya Try again kususiwa timu na muwekezaji Mo Dewj, Try Again aliona uwezekano wa kupindua meza, na kama ilivyo ada ya wafanyabiashara wakubwa kuwa na jicho angavu la udhia, S.S Bakhressa hakusita kupenyeza rupia!

Vita kubwa iliyopo hivi sasa ni Try Again aliyeko kwenye mikakati thabiti ya kumpindua Mo Dewj kama muwekezaji kisha nafasi hiyo apewe muwekezaji asiye na mbambamba S.S. Bakhressa, huku Mo Dewj nae akiwa katika mipango ya kujidhatiti kushikilia nafasi yake hiyo adhimu ambayo huitumia mara nyingi kama kielelezo cha mali zake (SSC)

Serikali yakoleza vita!
Hivi karibuni, Serikali imetoa agizo la kuanzishwa upya kwa mchakato wa undeshwaji wa kisasa kwa klabu ya Simba. Kama mtakumbuka vyema mchakato huo ulioanza miaka kadhaa nyuma, haukuwahi kukamilika.

Serikali imetoa agizo hilo baada ya kujidhihirisha kuwa mchakato wa awali ulikuwa na makosa mengi, hivyo ulikuwa batili ukikosa uhalali.

Agizo hilo limekuwa chachu kwa Try Again na timu yake, kwani endapo ukifanikiwa kuanza kuna uwezekano mkubwa wa S.S. Bakhressa na wawekezaji wengine kujitokeza na kushika hatamu katika mgawanyo wa hisa, huku ikielezwa kwamba Mo Dewj atarudishiwa fedha zake alizolipia katika mchakato wa awali uliohuishwa ambako alijitwalia hisa 49% za umiliki wa klabu ya Simba.

Mo Dewj atupa shilingi mechi ya Yanga!
Hii ni tahadhari kwa Klabu ya Yanga, Hersi na wenzio kama hamjaipata nawapa hii…

Mo Dewj amejipanga kuitumia mechi ya tarehe 20/04/2024 dhidi ya Yanga kama turufu yake ndani ya Simba.

Mo Dewj ambaye inaarifiwa ametenga fungu nono kuhakikisha Simba inashinda mechi hiyo, amejipanga sawia na mkakati wake huo ambao tayari ameshaanza utekelezaji.

Mkakati huu wa Mo ni kwamba endapo Simba ikishinda mechi hiyo, atafanikiwa kurudisha imani na mapenzi kwa mashabiki, hivyo kutumia hilo kama zengwe la kuwang’oa Try Again na Mangungu pale Simba.

Kila mmoja ana mpango kazi!
Try Again ambaye hapo awali alitumia janja janja kuwang’oa aliyekuwa CEO wa Klabu bibie Barbara na Rweyemamu ambaye alikuwa meneja wa timu kwa kuwachonganisha na muwekezaji Mo Dewj, anahaha kulinda maslahi yake kwani endapo Mo Dewj akishinda vita hii (Kwa Simba kushinda dhidi ya Yanga) amepanga kuwarejesha Barbara, Rweyemamu ambaye hivi sasa yupo Kikosi B na aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ambaye alijiengua Mkwabi.

Try Again ambaye wameungana na Mangungu kumuhujumu Mo Dewj, nao hawako nyuma. Wanatumia turufu yao ya ujanja wa mjini kuhakikisha Mo Dewj anang’oka Simba kwa namna yoyote!

Inaarifiwa hata agizo la kuanza upya kwa mchakato wa uendeshaji wa kisasa wa timu umechagizwa na connection za Try Again pamoja na S.S.B na mpaka hivi sasa mpango wao umetiki.

Je, nani ataibuka mshindi katika vita hii? Ni watoto wa mjini Salim Abdallah, Try again au tajiri Mo Dewj?

Ni mimi na chanzo changu nyeti,

Nifah.

Pia soma
- Tetesi: - Simba imepasuka. Kuna Simba ya Try Again na Simba ya Mo, Kila upande unauroga upande mwingine
 
View attachment 2966280

Moto unawaka SSC! Ni vita kubwa!
Klabu ya Simba ipo katika kipindi kigumu cha vita inayozidi kukomaa kila uchwao baina ya Mkurugenzi wa bodi ya Wakurugenzi ya Simba Salim Abdallah Mhene ‘Try Again’ dhidi ya ‘Rais wa heshima’ wa Simba Mohamed ‘Mo’ Dewj.

Wawili hao walianza kukosa maelewano baada ya Mo Dewj kuhamisha makazi yake nchini ambapo taarifa za uhakika ni kwamba anaishi Dubai hadi hivi sasa.

Baada ya Mo Dewj kuhamisha makazi uwekezaji wake Simba ulisuasua, ikitaarifiwa kumuachia mzigo mkubwa wa uendeahaji timu Try Again ambao ulimuelemea!

Try Again alijitahidi kadiri ya uwezo wake baada ya ‘tajiri’ kujitenga ‘kiaiana’, akihaha huku na huko kutafuta namna ya kuinusuru Klabu ya Simba ambayo kwa msimu wa tatu mfululizo imekuwa na matokeo ya kusuasua. Jitihada zake hizo zikizaa matunda kwa kiasi kisichoendana na kipindi ambacho muwekezaji alikuwa ameshikilia usukani.

Try Again adhamiria mapinduzi, amlenga Said Salim Bakhressa!
Baada ya Try again ‘kususiwa’ timu na muwekezaji Mo Dewj, Try Again aliona uwezekano wa kupindua meza, na kama ilivyo ada ya wafanyabiashara wakubwa kuwa na jicho angavu la udhia, S.S Bakhressa hakusita kupenyeza rupia!

Vita kubwa iliyopo hivi sasa ni Try Again aliyeko kwenye mikakati thabiti ya kumpindua Mo Dewj kama muwekezaji kisha nafasi hiyo apewe muwekezaji asiye na ‘mbambamba’ S.S. Bakhressa, huku Mo Dewj nae akiwa katika mipango ya kujidhatiti kushikilia nafasi yake hiyo adhimu ambayo huitumia mara nyingi kama kielelezo cha mali zake (SSC)

Serikali yakoleza vita!
Hivi karibuni, Serikali imetoa agizo la kuanzishwa upya kwa mchakato wa undeshwaji wa kisasa kwa klabu ya Simba. Kama mtakumbuka vyema mchakato huo ulioanza miaka kadhaa nyuma, haukuwahi kukamilika.

Serikali imetoa agizo hilo baada ya kujidhihirisha kuwa mchakato wa awali ulikuwa na makosa mengi, hivyo ulikuwa batili ukikosa uhalali.

Agizo hilo limekuwa chachu kwa Try Again na timu yake, kwani endapo ukifanikiwa kuanza kuna uwezekano mkubwa wa S.S. Bakhressa na wawekezaji wengine kujitokeza na kushika hatamu katika hisa, huku ikielezwa kwamba Mo Dewj atarudishiwa fedha zake alizolipia katika mchakato huo uliohuishwa ambako alijitwalia hisa 49% za umiliki wa klabu ya Simba.

Mo Dewj atupa shilingi mechi ya Yanga!
Hii ni tahadhari kwa Klabu ya Yanga, Hersi na wenzio kama hamjaipata nawapa hii…

Mo Dewj amejipanga kuitumia mechi ya tarehe 20/04/2024 dhidi ya Yanga kama turufu yake ndani ya Simba.

Mo Dewj ambaye inaarifiwa ametenga fungu ‘nono’ kuhakikisha Simba inashinda mechi hiyo, amejipanga sawia na mkakati wake huo ambao tayari ameshaanza utekelezaji.

Mkakati huu wa Mo ni kwamba endapo Simba ikishinda mechi hiyo, atafanikiwa kurudisha imani na mapenzi kwa mashabiki, hivyo kutumia hilo kama zengwe la kuwang’oa Try Again na Mangungu pale Simba.

Kila mmoja ana mpango kazi!
Try Again ambaye hapo awali alitumia ‘janja janja’ kuwang’oa aliyekuwa CEO wa Klabu bibie Barbara na Rweyemamu ambaye alikuwa meneja wa timu kwa ‘kuwachonganisha’ na muewekezaji Mo Dewj, anahaha kulinda maslahi yake kwani endapo Mo Dewj akishinda vita hii (Kwa Simba kushinda dhidi ya Yanga) amepanga kuwarejesha Barbara, Rweyemamu ambaye hivi sasa yupo Kikosi B na aliyekuwa Mkurugenzi wa bodi ya wawekezaji ambaye alijiengua Nkwabi.

Try Again ambaye wameungana na Mangungu kumuhujumu Mo Dewj, nao hawako nyuma. Wanatumia turufu yao ya ‘ujanja wa mjini’ kuhakikisha Mo Dewj anang’oka Simba kwa namna yoyote!

Inaarifiwa hata agizo la kuanza upya kwa mchakato wa uendeshaji wa kisasa wa timu umechagizwa na ‘connection’ za Try Again pamoja na S.S.B na mpaka hivi sasa mpango wao ‘umetiki’.

Je, nani ataibuka mshindi katika vita hii? Ni ‘watoto wa mjini’ Salim Abdallah, Try again au tajiri Mo Dewj?

Ni mimi na chanzo changu nyeti,

Nifah.
Vita vya Panzi
 
Mwenye kisu kikali anakuwa wa kwanza kutafuna nyama.

Hao wawili wote watang'oka Simba wao wenyewe kwa hiyari yao aidha kwa pamoja au kwa nyakati tofautitofauti isipokuwa timu ipate matokeo mazuri.
Lisingekuwa agizo la kuanza upya mchakato Try again asingepata nguvu ya kuthubutu kumpindua Mo, hii ngoma ni ngumu kwa maana kila mmoja ana nafasi.
 
Nifah naona umeiva kitengo cha propaganda.
Unajibu mapigo kwa propaganda za Simba kuhusu mishahara ya wabongo pale Yanga.

Soka letu Kivyetu : Mzinze vs Guede-Season 1 episode 1.
Soka letu Kivyetu: Mo vs TryAgain-Season 1 episode 2.
Hapana Mkuu, hii sio propaganda ni habari ya ukweli kabisa.

Na huyo mtu ambaye ni chanzo changu ni mwanachama hai wa Simba mwenye access na taarifa za ‘ndani’ huko kwenye klabu yao.
 
Mo alikuwa hatoi pesa huku akiubana uongozi kwa mikataba yake ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa inamnufaisha yeye. Baada ya kuona hiyo changamoto Mangungu na Try again walikutana na Bakhresa Zanzibar ili wafanye taratibu za kumwondoa mo Kama mwekezaji mpya. Bahati mbaya kwao na nzuri kwa mo alipata habari hivyo mo akaanza kulipa watu waanzishe kuendesha kampeni ya kumwondoa Mangungu na Try again.
Ni muda utaongea.
 
Back
Top Bottom