Rafiki wa kuchat anatafutwa

Habari zenu,naitwa epi Niko dar umri miaka 30 natafuta marafiki wa kuchat nao na kurelax akili yangu.angalizo naitaji marafiki tafadhali na cyo wapenzii ......Asante
Hahahahaaa.... Eti unahitaji Marafiki na sio Wapenzi...!
Wanawake bhana....!!

Hayaaa Vijana wenzio watakuja....!
 
Inashangaza sana Watanganyika, mtu yupo kwenye mtandao wa kijamii tena kwenye Jukwaa la Mahausiano na zaidi kwenye sub-forum inayoitwa ''Love Connect''; lakini kuna watu wanashangaa kuwa mtu anatafuta marafiki wa kuchat nao.

Kipi kinashangaza hapa na kuja na maswali kama ''kwani mtaani kwenu hakuna watu''? Kama wewe unajua mtaani kuna watu kwanini upo Jamii Forums? Kaa na watu wa mtaani kwenu mjadili na kuzungumza huko.

Tuache akili za kufungwa; mtu anahoji eti miaka 30 unatafuta marafiki? Ni wapi wameandika kuwa mtu wa miaka 30 hatakiwi kuwa na marafiki?

Tuache kujifanya kuwa tuna ''standards'' fulani hivi kiasi cha kushangaa namna wengine wanavyoishi. Wewe na standards zako baki nazo mtaani kwako.

Tukubali kuishi maisha tukiwa na utofauti, kama unaona hili analofanya huyu dada sio ''standards'' zako kaa kimya na acha aishi maisha yake.

Tukianza kuwekeana mipaka kwenye maisha, tutapoteza radha ya maisha.

Wapo watu hawaijui kabisa Jamiiforums na wanaishi vizuri kabisa, huna haja ya kumshangaa.

Wapo wanaokwenda Dubai kwa mapumziko mwisho wa mwaka na yupo ambaye hana uwezo hata wa kwenda msitu wa Pugu lakini hawashangaani; kila mtu kwa maisha yake.

Wapo wanasomesha watoto shule IST na hawashangai wakiona mtoto anasoma pale Uhuru Mchanganyiko au Ubungo Kibangu; kila mtu aishi maisha yake.

Kama wewe una marafiki ukiwa na miaka 20 acha anayetafuta marafiki akiwa na miaka 30 aishi maisha yake.

Kuishi ni rahisi iwapo kila mmoja atatambua mipaka na uhuru wa mwingine.

Wewe umepanga nyumba unalipa laki 3 kwa mwezi na mwingine anaishi kwa elfu 30 kwa mwezi na yupo mwingine analipa Milioni 2 kwa mwezi na hakuna haja ya kushangaana.

Kuna mtu kilipo kitanda, ndipo ilipo friji, Tv, kabati na jiko la gesi; na analala na kupata usingizi, ni maisha yake.

Tambua maisha ni yako, usijipe umuhimu kwenye maisha ya mwingine, ishi kwa standards zako lakini usilazimishe watu waishi kama wewe kwa sababu wewe sio ''standard unit'' ya watu.

Siku njema.
 
Habari zenu,naitwa epi Niko dar umri miaka 30 natafuta marafiki wa kuchat nao na kurelax akili yangu.angalizo naitaji marafiki tafadhali na cyo wapenzii ......Asante
Ndo huyu wewe sasa
Screenshot_20231208-175437.png
 
Habari zenu,naitwa epi Niko dar umri miaka 30 natafuta marafiki wa kuchat nao na kurelax akili yangu.angalizo naitaji marafiki tafadhali na cyo wapenzii ......Asante
Nipo rafiki, mimi ndio mchatishaji bora wa mwaka 2022-2023
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom