Nimechanganyikiwa msaada wa haraka

Acha upopoma wanaume hatuendeshwi kwa hisia mzee.
Kwa akili tu inabidi uoe huyo kakuzalia mtoto, sasa kama hana baya kwanini usimuoe, umemzalisha unaenda kuoa kwingine kisha keshokutwa mnakuja kuwananga haoa SINGLE MAZAs
 
Poleni na majukumu ya Kila siku, nimekuja kuomba ushauri hapa Jamii Forums sababu naamini humu kuna watu wenye uzoefu au washawahi kutokewa na scenario kama hii.

Nisiwachoshe, mimi ni kijana wa miaka 34, baada ya kuona umri unasogea halafu sipati mtu ambae ninampenda, nilizoeana na binti ambae tulianzisha mahusiano ila lengo langu ilikua ni kupata mtoto, basi yule binti akaja nyumbani, tukaendelea kuishi huku tukilea mtoto, mtoto Ana umri wa mwaka mmoja Sasa.

Tatizo ni kwamba huyu binti ni wife material Lakini Sasa kwa upande wangu sina hisia nae hata kidogo, cha Kushangaza nimempenda binti mwingine ambae pia anamtoto ambae sio wangu.

Na huyu binti ambae nnaishi nae mwenye mtoto wangu karudi kwao anasema mpaka niende kumtolea posa ndo atarudi, la sivyo atabadilisha Namba za simu, na sitampata tena, na mtoto akikua atamwonesha kaburi na kumwambia baba ake alikufa.

Kinachofanya nichanganyikiwe ni kwamba, nikimuoa huyu mwenye mtoto wangu ndio sina hisia nae ila hana tatizo, nikimuoa huyu single mother ambae nnampenda, siwezi kua na Amani sababu mtoto angu ataenda kuishi na baba wa kambo huku mimi nnalea mtoto wa mwingine

N.B Mimi ni mwanaume nnaependa sana watoto, ninampenda sana mtoto wangu, mbaya zaidi ni wa kike. Naamini Kuna watu humu wanajua kudadavua haya mambo ya mahusiano na pia wanaupeo mkubwa kuliko mimi.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kabisa.
Mkuu una tatizo la kisaikolojia....ambalo husababisha uwenda wazimu.asante na karibu
 
Back
Top Bottom