Nataka kumuacha lakini sina pa kuanzia

bagabe

JF-Expert Member
May 8, 2014
483
603
Wakuu kuna binti nimekua nae kwenye mahusiano almost miaka mitano. Tumepitia changamoto nyingi kwenye maisha lakini still tuko pamoja. Sababu kubwa iliyonileta hapa ni kuomba ushauri wenu ndugu zangu juu ya hili suala.

Huyu binti nimeshatoa barua kwao ilibaki mahali tu ili nifunge nae pingu za maisha. Aliamua kuhamia kwangu mazima tutafute maisha wote huku mambo mengine yakiendelea.

Lakini nilitoa barua kutokana na shinikizo la mtoto alijifingua bahati mbaya akafariki nikaona nitoe barua kwao kuonesha uungwana. Sasa kwa kipindi chote nimeishi nae nimegundua sina hisia nae kabisa yani akili yangu ipo kutoka nje ya huu mfumo nataka niwe huru.

Nadhani ujauzito ulikua shinikizo kubwa sana la mimi kua karibi nae. Tatizo linakuja tayari anajulikana na familia yangu yote na kila mtu wangu wa karibu anamjua na mimi kila mtu wao wa karibu ananijua.

Naombeni ushauri nataka nianze maisha yangu mapya bila uwepo wake ila sina pa kuanzia niafanyaje ndugu zangu wana JF?
 
Wakuu kuna binti nimekua nae kwenye mahusiano almost miaka mitano.Tumepitia changamoto nyingi kwenye maisha lakini still tuko pamoja.Sababu kubwa iliyonileta hapa ni kuomba ushauri wenu ndugu zangu juu ya hili suala.Huyu binti nimeshatoa barua kwao ilibaki mahali tu ili nifunge nae pingu za maisha.Aliamua kuhamia kwangu mazima tutafute maisha wote huku mambo mengine yakiendelea.

Lakini nilitoa barua kutokana na shinikizo la mtoto alijifingua bahati mbaya akafariki nikaona nitoe barua kwao kuonesha uungwana.Sasa kwa kipindi chote nimeishi nae nimegundua sina hisia nae kabisa yani akili yangu ipo kutoka nje ya huu mfumo nataka niwe huru.Nadhani ujauzito ulikua shinikizo kubwa sana la mimi kua karibi nae.Tatizo linakuja tayari anajulikana na familia yangu yote na kila mtu wangu wa karibu anamjua na mimi kila mtu wao wa karibu ananijua.Naombeni ushauri nataka nianze maisha yangu mapya bila uwepo wake ila sina pa kuanzia niafanyaje ndugu zangu wana jf?!.
Una umri gani?
 
Dah muonee huruma mzee ...
Siyo kumuonea huruma wala kumfanyia hisani.Anapaswa abebe jukumu la kuwa mwenza kwa akili nyingi.Kama wote tukiamua tu kusema hisia kwa wenza wetu zimeisha,kuna ndoa au mahusiano yatabaki salama?Mapenzi,ndoa au mahusiano ni hesabu,mipango,uchaguzi bora,uvumilivu,unyenyekevu,utu,dhamira njema,nia thabiti vinavyoongozwa na upendo maridhawa.Mapenzi siyo sukari tupu kwamba utailamba kwa furaha kila siku.Atulie na kutafakari.
 
Wakuu kuna binti nimekua nae kwenye mahusiano almost miaka mitano.Tumepitia changamoto nyingi kwenye maisha lakini still tuko pamoja.Sababu kubwa iliyonileta hapa ni kuomba ushauri wenu ndugu zangu juu ya hili suala.Huyu binti nimeshatoa barua kwao ilibaki mahali tu ili nifunge nae pingu za maisha.Aliamua kuhamia kwangu mazima tutafute maisha wote huku mambo mengine yakiendelea.

Lakini nilitoa barua kutokana na shinikizo la mtoto alijifingua bahati mbaya akafariki nikaona nitoe barua kwao kuonesha uungwana.Sasa kwa kipindi chote nimeishi nae nimegundua sina hisia nae kabisa yani akili yangu ipo kutoka nje ya huu mfumo nataka niwe huru.Nadhani ujauzito ulikua shinikizo kubwa sana la mimi kua karibi nae.Tatizo linakuja tayari anajulikana na familia yangu yote na kila mtu wangu wa karibu anamjua na mimi kila mtu wao wa karibu ananijua.Naombeni ushauri nataka nianze maisha yangu mapya bila uwepo wake ila sina pa kuanzia niafanyaje ndugu zangu wana jf?!.
Mungu anakupa unachostahili na siyo unachotaka
Huyo mwanamke unayemtaka kumuacha wapo wachache sana kwenye dunia ya sasa, wanatafutwa sana na kizazi chao kinakaribia kuisha kbsa.
Sasa hivi wapo unatongoza asubuhi, jioni gesi imeisha, simu mbovu, kodi imeisha na wadangaji wazoefu na utoaji hela kwake ndiyo upendo kwake.
Kila la kheri
 
hongera sana kwa hatua hii ya kuomba ushauri ni hatua nzuri. Mungu anataka kukuonesha makosa yako. Tafadhali naomba ujipe muda ujifunze
1. Nini maana ya mwanaume.
2. Kwanini umezaliwa mwanaume.
3. Ujifunze kufikiri na kuamua kama mwanaume.
 
Wakuu kuna binti nimekua nae kwenye mahusiano almost miaka mitano.Tumepitia changamoto nyingi kwenye maisha lakini still tuko pamoja.Sababu kubwa iliyonileta hapa ni kuomba ushauri wenu ndugu zangu juu ya hili suala.Huyu binti nimeshatoa barua kwao ilibaki mahali tu ili nifunge nae pingu za maisha.Aliamua kuhamia kwangu mazima tutafute maisha wote huku mambo mengine yakiendelea.

Lakini nilitoa barua kutokana na shinikizo la mtoto alijifingua bahati mbaya akafariki nikaona nitoe barua kwao kuonesha uungwana.Sasa kwa kipindi chote nimeishi nae nimegundua sina hisia nae kabisa yani akili yangu ipo kutoka nje ya huu mfumo nataka niwe huru.Nadhani ujauzito ulikua shinikizo kubwa sana la mimi kua karibi nae.Tatizo linakuja tayari anajulikana na familia yangu yote na kila mtu wangu wa karibu anamjua na mimi kila mtu wao wa karibu ananijua.Naombeni ushauri nataka nianze maisha yangu mapya bila uwepo wake ila sina pa kuanzia niafanyaje ndugu zangu wana jf?!.
Pumbavu huna akili kabisa, mama yako angefanyiwa hivi ungekuwepo wewe? Mabao mengine yanafaa chooni tu wazazi wanajua wamezaa mtoto wa kiume kumbe kichwani kuna akili za james delicious.
 
Kwa miaka mitano umekuwa naye halafu leo ndiyo hisia kwake zimekutoroka?Cheki vizuri.Yawezekana si hisia tu zilizojiweka kando nawe bali hata akili za kuchambua mambo hauna siku nyingi tu.Acha kuchezea maisha ya mwenzako kwa gharama nafuu ingawa upendo/mapenzi hayalazimishwi.Busara itawale.

Nifanyaje mkuu
 
Back
Top Bottom