Nimechanganyikiwa msaada wa haraka

Mwanaume unaendeshwaje na hisia? Eti hauna hisia? Like seriously😂😂😂.

Bwana mdogo, kwenye haya maisha mwanaume unapaswa uombe kupata mke mwema, haijalishi mambo ya hisia wala kupenda, wanaume tunatumia ubongo kufanya maamuzi na siyo mioyo, mambo ya hisia waachie wanawake.

Huyo unayesema una hisia naye, anaweza kuja kukuchemsha ubongo mpaka hisia zikate mara 100 zaidi ya huyu wa sasa.

Chukua bapa narusha muamala. Ila iwe bapa kubwa.
 
Wewe muoe tu huyo single maza, ukishapigwa tukio ndo utajua kumbe ulimpenda sana baby mama wako ila ukatanguliza tamaa mbele.
Hawajui watoto hawa,huyo usiyekuwa na hisia nae unasema hana tatizo lolote.
Sasa unaenda wapi?
Huyo ndo mwenzio huyo mzoee tu,
Bibi na babu zetu walivumiliana wakaishi vizuri tu.
Unakaa nae huyohuyo badae mnazoeana life linakua mchekea tu.
Huyo singo maza ni anatafuta hifadhi tu.
Atadunguliwa tena ukiwae humohumo nani uanza kutafuta mkaa.
Shauri yako.
Hakuna ushauri hapa.
 
Hadithi ya kusadikika

Yaani habari nzima ni 👇




2B9X.gif
 
Pole sana, vijana wengi wa siku hizi wana hali kama hiyo unayoisema. Binafsi nawaona kama vile hawajitambui. Wanajiingiza kwenye changamoto nzito ambazo zinapelekea wawe na msongo wa mawazo hata kuwa na magojwa ya kudumu. Wewe asikudanganye mtu. Oa mwanamke anayejitambua. Huyo unayesema unampenda, humpendi bali unamtamani tu. Na mara nyingi wanakuwa na vimbwanga usipime. Atakuoneshea siku moja mpaka utasema poo. Usiwachulie poa wanawake. Wanaweza wakakufanya mpaka ukaogopa kurudi kwenye nyumba uliyojenga mwenyewe.
Wewe unamtweza mwanamke ambaye wee mwenyewe umekiri hana shida yoyote. Halafu wewe unaanza kufunga safari kwenye kuyatimba.
Sina mengi, ni hayo tu.
Asipochuku huu ushauri basi tena
 
Mimi kama daktari mwenye uzoefu na experience ya kutosha kuhusu matatizo ya afya ya akili. Nadiriki kusema una tatizo kitalaamu linaitwa SMOD au kwa kirefu Single Mother Obsession Disorder.

Acha upuuzi mkuu.
 
M
Poleni na majukumu ya Kila siku, nimekuja kuomba ushauri hapa Jamii Forums sababu naamini humu kuna watu wenye uzoefu au washawahi kutokewa na scenario kama hii.

Nisiwachoshe, mimi ni kijana wa miaka 34, baada ya kuona umri unasogea halafu sipati mtu ambae ninampenda, nilizoeana na binti ambae tulianzisha mahusiano ila lengo langu ilikua ni kupata mtoto, basi yule binti akaja nyumbani, tukaendelea kuishi huku tukilea mtoto, mtoto Ana umri wa mwaka mmoja Sasa.

Tatizo ni kwamba huyu binti ni wife material Lakini Sasa kwa upande wangu sina hisia nae hata kidogo, cha Kushangaza nimempenda binti mwingine ambae pia anamtoto ambae sio wangu.

Na huyu binti ambae nnaishi nae mwenye mtoto wangu karudi kwao anasema mpaka niende kumtolea posa ndo atarudi, la sivyo atabadilisha Namba za simu, na sitampata tena, na mtoto akikua atamwonesha kaburi na kumwambia baba ake alikufa.

Kinachofanya nichanganyikiwe ni kwamba, nikimuoa huyu mwenye mtoto wangu ndio sina hisia nae ila hana tatizo, nikimuoa huyu single mother ambae nnampenda, siwezi kua na Amani sababu mtoto angu ataenda kuishi na baba wa kambo huku mimi nnalea mtoto wa mwingine

N.B Mimi ni mwanaume nnaependa sana watoto, ninampenda sana mtoto wangu, mbaya zaidi ni wa kike. Naamini Kuna watu humu wanajua kudadavua haya mambo ya mahusiano na pia wanaupeo mkubwa kuliko mimi.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kabisa.
Mimi ni mwanamke,ila nakupa ushauri wa Bure!

Ukitaka kuishi Kwa amani achana na huyo unaesema una hisia nae!
Utakuja kutulilia hapa!
Kwa Dunia ilivyo ss,acha kabisa,Baki na uliyezaa nae utakuja kutushukuru!
 
Unachanganyikiwa kisa wanawake ati umuoe yupi are you serious??
NDOA NI UTAPELI
NDOA NI ULAGHAI
subiri huyo single mama akunyooshe ulee mtoto wa mwenzio na mke wa mwenzio.
KATAA NDOA TUNZA FURAHA YAKO.
 
Usipende sana kufatisha moyo Mkuu moyo hua unadanganya sana tumia Zaid akili na sio moyo....kingine Muombe Mungu akusaidie ufanye maamuz sahihi...thamini cha kwako kwanza
 
Back
Top Bottom