- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
- Tunachokijua
- Zaidi ya watu bilioni 2 kutoka nchi zaidi ya 180 hutumia WhatsApp kufanya mawasiliano na marafiki au familia, wakati wowote na mahali popote.
Programu hii maarufu ya ujumbe wa papo hapo inayomilikiwa na kampuni ya Meta, ilianzishwa na Jan Koum na Brian Acton mnamo mwaka 2009, lakini baadaye ilinunuliwa na Facebook (ambayo sasa inaitwa Meta) mwaka 2014 kwa thamani kubwa ya dola bilioni 19.
Kwa sasa makao yake makuu yapo Meta Way, Menlo Park, California 94025, Marekani.
Kuzuka kwa Madai ya kubadilika kwa Sera za Matumizi ya WhatsApp
Kumekuwepo na ujumbe unaosambaa kwenye Makundi sogozi ukibainisha kuwa kampuni ya Meta imebadili Sera za Matumizi ya Mtandao wa WhatsApp.
Madai haya yameonekana pia kwenye Mtandao wa X Machi 21, 2024 ambapo taarifa zake zimehifadhiwa hapa na hapa.
Baadhi ya madai hayo ni kuanzishwa kwa utaratibu mpya wa kurekodi simu zote pamoja na nakala za rekodi za mawasiliano zitahifadhiwa. Aidha, WhatsApp, Facebook, Twitter, Instagram na mitandao mingine ya kijamii itafuatiliwa.
Ujumbe huo unaenda mbali zaidi kwa kubainisha kwa Polisi wataanza kufuatilia mawasiliano ya watu kupitia Mtandao huo kisha watatoa taarifa pamoja na kufungua kesi za uhalifu wa mtandaoni kwa kila mtu atakayechapisha ujumbe wenye utata.
Kwa upande wa makundi Sogozi, Sheria hii mpya inaonesha kuwa iwapo ujumbe utakuwa na alama moja ya tick itakuwa na maana Ujumbe husika umepelekwa.
- Alama mbili za bluu kumaanisha Ujumbe umesomwa.
- Alama tatu za bluu kumaanisha Serikali imechukua note ya ujumbe.
- Alama mbili za bluu na moja nyekundu kumaanisha Serikali inaweza kuchukua hatua dhidi yako.
- Moja ya bluu na mbili nyekundu kumaanisha Serikali inachunguza taarifa yako.
- Alama tatu za nyekundu kumaanisha Serikali imeanza kuchukua hatua dhidi yako na utapata wito wa mahakama hivi karibuni.
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia vyanzo vyake vya kuaminika umebaini kuwa suala hili halina ukweli.
Aidha, JamiiCheck imefahamishwa pia na Kampuni ya Meta kuwa taarifa hii ni Uzushi hivyo watu wanapaswa kuipuuza.