Nawasalimu wana jamii, pia nawapa pole na mihangaiko ya hapa na pale
Pamoja na salaam pia naombeni ushauri. Naomba kwa yeyote aliyetayali kunishauri anishauri kwa dhati ya moyo wake, si kukejiei wala nini sababu hii siyo hadithi bali ni kitu cha ukweli na ndo maana nimeamua kuleta hapa mbele yenu muweze kunishauri kwani niko njia panda.
Niko katika mahusiano ambayo kwa kweli yananiacha njia panda, nina jamaa yangu wa muda mrefu tu, binafsi yangu nampenda sana huyu bwana, japo na yeye anaonyesha kunipenda lakini simuelewi sana. Mimi nina mtoto ambaye sikuzaa nae, huwa anaonyesha mapenzi makubwa sana kwa mtoto wangu ikiwa ni pamoja na kunisaidia kumlipia ada, kuongea nae kwenye cm kama vile baba afanyavyo kwa mtoto wake, akiwa nae anamtambulisha kwa marafiki zake kwamba ni mtoto wake wa kumzaa mimi pia ananiita mkewe, tunaishi mbali mbali (yaani mikoa tofauti) yeye yuko Dar mimi niko Mwanza. Tatizo liko kwenye kufunga ndoa, nimekuwa nikiwambia mara kwa mara kufunga ndoa lakini amekuwa akinipa moyo kila kukicha kwamba usiwe na haraka tutafunga tu ndoa, hili si jambo la kufanyia haraka na maneno mengine kibao, tumependana tangu mtoto wangu akiwa darasa la kwanza na hivi sasa mtoto yuko kidato cha tatu.
Nikiwa karibu nae kwa kweli namuonyesha mapenzi yangu ya dhati kwa kumpikia, kumfulia na kufanya vile ambavyo mke mwema anatakiwa kufanya. Ndugu zake kama dada, kaka na wadogo zake wananifahamu, wao pia wanipenda pamoja na mtoto wangu na wanasema sisi hatumtambui mtu mwingine zaidi yako.
Moyo wangu huko kwake, sijisikii kuwa na mtu mwingine kabisa ni kwamba nampenda sana, na yeye pia anaonyesha kunipenda, hila siwezi jua moyoni mwake. Sasa wapendwa wanajamii naombeni msaada wenu wa ushauri, kama wewe ni mwanamke nisaidie kama ingekuwa wewe ungefanyaje na kama ni mwanaume angalia hii hali na unishauri kwa kuwa wewe ni mwanamume na hii hali ya mwanaume mwenzio unaionaje? Naomba tusifanye kejeli wala utani.