Nifanyeje ili kutuliza akili na roho kumuacha huyu dada isiwepo?

holy spirit

JF-Expert Member
Nov 30, 2020
700
1,040
Heshima kama zote kwenu wana JF.

Umri wangu sio mkubwa sana ila ngazi ya tatu naanza kuipanda soon.

Kwenye miaka yangu ya 20s nimekuwa mtu wa kubadilisha wadada sijawahi kuwa na mahusiano yaliyokaa zaidi ya miezi miwili maana nilikuwa mzinguaji sana hasa nikishapewa tunda akili inanituma nihamie kwa mdada mwingine.

Kwa sasa nimejitafakari mwenyewe nikaona ni vyema nianzishe mahusiano ya kueleweka na mtu mmoja ikiwezekana yapelekee ndoa.

Mdada nilienzisha nae mahusiano kiukweli anaonyesha kunipenda sana, tunaelewana na mimi pia nampenda.

Tatizo ana mtoto mmoja, baba mtoto alimkana mtoto akamwambia mdada na familia yake wafate mambo yao waache kumfatilia ye hamtambui huyo mtoto.

Pia ni wa kabila fulani la kaskazini huwa wanasemwa eti wagawaji sana.

Mimi sio mtu wa kusikiliza maneno ya watu sana ila haya ninayoambiwa na watu wa karibu kisa kuwa na mahusiano na huyu dada yananipa hofu na wasiwasi, yani akili na roho havijatulia kabisa kwasababu mdada sitaki kumuacha wala nini mwamba nimefall in love.

Mfano wa maneno ninayoambiwa
"Hapo baba mtoto atakuja kuomba tu msamaha atasamehewa ataendelea kupewa mzigo kama kawaida"

"Huyo hakupendi anatafuta sehemu ya kujishikiza na wewe ndo umedakwa kirahisi" ( huyu tena ni mwanamke na hapa ndo niliogopa zaidi).

"Hilo kabila la huko mhhh.. haya ni wewe lakini na maamuzi yako"

" Ila huwezi kujua wapo waliooa wenye watoto na wengine hilo hilo kabila ila wapo kwenye ndoa zao na mambo yanaenda" (bro mmoja alinitia moyo kidogo).

Wakuu niko kwenye dilemma sio siri anxiety inaniingia. Nifanyeje ili kutuliza akili an roho kumuacha huyu dada isiwe option kwanza tafadhali.
 
Mwanamke huwa anamzalia Mwanaume anaempenda tu especially kabla ya ndoa.

MTOTO NI KIUNGANISHI KATI YAO.

Kwanini ujibebeshe mizigo isiyokuwa na ulazima? Halafu tambua kuwa kulea mtoto ambae sio wako kuna changamoto sana.

PambanaZaidi/CottonandMore
Nimekuelewa mkuu. Lakini hakuna uwezekano kwamba ilikuwa bahati mbaya tu hakutegemea mimba
 
Tatizo ana mtoto mmoja, baba mtoto alimkana mtoto akamwambia mdada na familia yake wafate mambo yao waache kumfatilia ye hamtambui huyo mtoto.
Mkuu,

YOU ARE NOT SPECIAL. narudia tena YOU ARE NOT SPECIAL (Hauna Upekee huo ambao unahisi unao). Kilichomshinda Mwanaume mwenzako, hata wewe kitakushinda vilevile. Ni swala la Muda tu utajifunza hili. Wanawake huwa hawasemi Ubaya wao hata siku moja.

MZIGO unaoenda kuubeba, ni wewe pekee ndio utaweza kujitua. sisi kukupa tahadhari ni wajibu wetu.

Be a Man, tafuta Binti safi mwenye utii, umri mdogo ambaye hana Mtoto, tulia naye mjenge Familia na akupe amani ya nafsi.
 
Asante kwa wazo lako mkuu
 
Heshima kama zote kwenu wana JF.

Umri wangu sio mkubwa sana ila ngazi ya tatu naanza kuipanda soon.

Kwenye miaka yangu ya 20s nimekuwa mtu wa kubadilisha wadada sijawahi kuwa na mahusiano yaliyokaa zaidi ya miezi miwili maana nilikuwa mzinguaji sana hasa nikishapewa tunda akili inanituma nihamie kwa mdada mwingine.

Kwa sasa nimejitafakari mwenyewe nikaona ni vyema nianzishe mahusiano ya kueleweka na mtu mmoja ikiwezekana yapelekee ndoa.

Mdada nilienzisha nae mahusiano kiukweli anaonyesha kunipenda sana, tunaelewana na mimi pia nampenda.

Tatizo ana mtoto mmoja, baba mtoto alimkana mtoto akamwambia mdada na familia yake wafate mambo yao waache kumfatilia ye hamtambui huyo mtoto.

Pia ni wa kabila fulani la kaskazini huwa wanasemwa eti wagawaji sana.

Mimi sio mtu wa kusikiliza maneno ya watu sana ila haya ninayoambiwa na watu wa karibu kisa kuwa na mahusiano na huyu dada yananipa hofu na wasiwasi, yani akili na roho havijatulia kabisa kwasababu mdada sitaki kumuacha wala nini mwamba nimefall in love.

Mfano wa maneno ninayoambiwa
"Hapo baba mtoto atakuja kuomba tu msamaha atasamehewa ataendelea kupewa mzigo kama kawaida"

"Huyo hakupendi anatafuta sehemu ya kujishikiza na wewe ndo umedakwa kirahisi" ( huyu tena ni mwanamke na hapa ndo niliogopa zaidi).

"Hilo kabila la huko mhhh.. haya ni wewe lakini na maamuzi yako"

" Ila huwezi kujua wapo waliooa wenye watoto na wengine hilo hilo kabila ila wapo kwenye ndoa zao na mambo yanaenda" (bro mmoja alinitia moyo kidogo).

Wakuu niko kwenye dilemma sio siri anxiety inaniingia. Nifanyeje ili kutuliza akili an roho kumuacha huyu dada isiwe option kwanza tafadhali.
Wewe una watoto wangapi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom