Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa

Kuna mstari mwembaba Sana Kati ya kujishusha na kujidhalilisha

Isome kwa sauti
Kuna mstari mwembamba sana kati ya kuwaonesha watu mstari mwembamba ulio kati ya kujishusha na kujidhalilisha, na kuwapangia watu maisha huku uki wa judge bila hata kuwajua.

Shaggy katika "It Bun Me" alisema "You can't judge a man before you walk in his shoes".

Have some more understanding /mercy and less judgement please.
 
Kuna mstari mwembamba sana kati ya kuwaonesha watu mstari mwembamba ulio kati ya kujishusha na kujidhalilisha, na kuwapangia watu maisha huku uki wa judge bila hata kuwajua.

Shaggy katika "It Bun Me" alisema "You can't judge a man before you walk in his shoes".

Have some more understanding /mercy and less judgement please.
Huo mstari mwembamba kautengeneza yeye.

Mimi nikiongea kwa unyeyekevu kwa bosi wangu kuna mtu atasema najidhalilisha.
 
Kama lipi?

Ujue hayo mambo mawili ni mtambuka, wewe utasema hili mwingine akaona hivi na mwingine akaona vile.
Kwanza watu hatufanani.

Kwa mwanamfalme aliyezaliwa katika kasri la kifalme, inawezekana kumfuata mtu kumsalimia tu ni kujishusha, inatakiwa yeye ndiye afuatwe kusalimiwa, tena kwa kupigiwa magoti.

Wakati kwa mwenzangunamie pangu pakavu tia mchuzi hata nikifuta viatu vya watu kwa mahesabu yangu, naweza kujiona sijajishusha, naishi kwa mkakati wangu tu.

Sasa, inakuwaje mtoto wa mfalme anipangie mimi maisha yangu na kuniambia hapo mbona umejishisha sana unapangusa viatu vya watu vumbi, kwa kuangalia standards zake, wakati mimi maisha yangu si ya mtoto wa mfalme?
 
UTANGULIZI
Wakuu habari.

Naandika hii story yangu ikiwa ni mwaka sasa nipo mtaani nikiendelea na harakati za kusaka ajira mpya toka mkataba wangu wa ajira ulipoisha mnamo Desemba 2022. Nimeamua kushea uzoefu wangu kwa mtindo wa Masimulizi (katika episodes) kwa kuamini pengine inaweza kuwa na mafunzo kwa waajiri, waajiriwa au wanaotegemewa kuajiriwa. Naomba moderatoes wa JF wauache huu uzi wangu hapa hapa kwenye Jukwa la Ajira kwani muktadha wa simulizi hii maswala ya kubadilishana uzoefu katika swala la ajira na sio mambo ya entertainment. Twende kazi.

Episode 1: Sikuogopa kujidhalilisha ili kupata reliable connection

Mwaka 2011 nilipomaliza my 1st degree kama ilivo kwa wanachuo wengine, nilikuwa na expectation kubwa sana ya kupata ajira nzuri ndani ya muda mfupi. Hii ilijengwa na kiburi kwamba mwaka mmoja before sijamaliza niliwaaproach ndugu na wadau kwenye network yangu kwamba mwakani namaliza. Kila mmoja alinipromise kunisaidia kupata job au kuniconnect na waajiri mbali mbali. Swala likawa ni kwamba wewe maliza tu chuo then utuambie ili tukafanyie mipango.

Kimbebe kilikuja baada ya kumaliza. Nilitulia kwanza mwezi mmoja then nikaanza kucheki walionipromise job kwamba I am available. Asee nilipigwa dana dana za kutisha na mwishowe wengine wakawa hata hawapokei simu zangu. Nikiwaibukia nyumbani au maeneo yao ya kazi wanaishia kunipa nauli ya kurudia na kuniambia ajira ngumu cha muhimu wewe endelea kumuomba Mungu. It was very disappointing situation at that time na nikafikia hatua ya kuanza kuwachukia bila sababu as if wao ndio wanaonisababishia ugumu wa kuajiriwa, hahahaaa.

Basi nikaanza kuumiza kichwa how to go about finding the job. Nikaaply sana kazi kupitia job adverts za mtandaoni lkn mimi mwenyewe nikaona as a fresh graduate I didn’t have the skills and required experiences. Nikaanza kuona hata elimu yenyewe may be course niliyosoma haina maana bora lile boom ningelitumia kwa kuanzisha hata kimradi cha kuchoma popcorn mtaani.

Hali ilikuwa mbaya to most of the graduates mana kila nikiwacheki wana nao wanalalamika kama mm tuu isipokuwa wachache sana wenye connection tena za familia zao za kuzaliwa. Hapo nikakumbuka wakati naenda kuanza form 5 way back bro wangu aliwahi kuniambia “dogo huko shule nenda kawe na marafiki wa aina mbili, either wenye akili sana darasani au wale wanaotoka kwenye familia bora”. Nilikuja kumwelewa kipindi hiki ni nini bro alichomaanisha. Kwamba wale wenye akili sana darasani watakuinfluence kufauru na wale wanaotoka maisha bora ni future asset katika connection za ajira. Sasa mimi kutoka na usela wangu mavi wa teenager sikuwa na hata mmoja kati ya hao. Roho ilikuja kuniuma zaidi nilipogundua nilipokuwa advance niligombana na jamaa mmoja ambaye kwao walikuwa wapo poa sana wa kutokea mkoa wa Iringa, nilipooulizia habari zake nikasikia kwa kipindi kile natafuta ajira alikuwa ni msimamizi wa kampuni ya usafirishaji mizogo(malori) na walikuwa na ofidi zao bandarini (clearing and forwarding). Laiti yule jamaa ningemfanya best friend ukute ingekuwa rahisi kwa yeye kunipa mchongo. Anyway, les forget about him.

Nakumbuka siku moja nikiendelea kusaga visigino katika harakati zangu za kutembeza bahasha, kwenye foleni mikamwona lecturer wangu mmoja hivi, tumuite Dr KJ (PhD ya kihaya hiyo) kwenye shangingi lake akiendeshwa na dereva wake kama kawaida. Huyu lecturer nilimkumbuka kwa sababu alikuwa na sifa sana kwenye vipindi vyake na alikuwa anafundisha somo la project Management.

Yaani huyu Muhaya alikuwa anatumia nusu ya muda wake kwenye lecture kujisifia. Ataanza kuwananga maprof kwamba japo yeye ana PhD ila hakuna prof anaemzidi akili na pesa chuo kizima, kwanza yeye anaendeshwa na mshahara anaimlipa dereva wake ni sawa na wa tutorial assistant wa pale chuo. Alikuwa mdhalilishaji sana kwa wanafunzi hususani watoto wa kike au wanaofeli somo lake. Ila watu walichompendea jamaa alikuwa sometimes anagawa sana maokoto akiwakuta wanafunzi njiani ila ndio mjue mtadhalilishwa. Jamaa alikuwa anatembea na dola au Euro akidai pesa za madafu ni nzito, hatukujua anapata wapi zile dola dola. Nakumbuka kuna semester alimlipia ada jamaa mmoja alikuwa anasoma kwa shida sana alikuwa hana boom. Alimlipia ada ya semester ya mwisho ila yule jamaa cha moto alikiona maana Dr KJ kwenye kila kipindi alichofundisha kwenye madarasa yake lazima amtolee mfano yule jamaa mpaka mlipiwa ada akawa famous chuo hahahaaa.

Basi bhana nilipomwona kwenye foleni Dr KJ vitu vingi vingi vikapita kama mshale kwenye mawazo yangu. Kwamba huyu jamaa anaweza akawa asset lkn anaweza akanidhalilisha vibaya sana na nitamuanzanje yupo kwenye gari. Je atanikumbuka maana wanafunzi tulikuwa wengi sana. Lkn nikifikiria pale geto nadaiwa kodi mwenye nyumba keshanivumilia kama two months (nilamua kukomaa mjini sikutaka kwenda mkoani). Wakati naendelea kuwaza foleni ikaanza kutembea, asee sijui ni nini kilinikuta nikajikuta naikimbilia ile gari na kwenda kuisimamia kwa mbele nikiizuia isiende huku nikimwonyeshea ishara dereva apaki pembeni. Dereva alipoona anaweka foleni akamuuliza bosi wake wafanyeje hahaaa maana nacheka kama ni mazuri. Basi Dr KJ kwa wasiwasi akamwambia aweke pembeni.

Basi nikasogea upande wa Dr KJ akawa hataki kushusha kioo, akanielekeza niende upande upande wa dereva. Nikajua tuu boss anaogopa labda nitamdhuru so he decided to sacrifice his driver- hahahaa. Basi nikaenda upande wa dereva aliposhusha kioo nikamsalimia.

Mimi: shikamoo Dr KJ

Yeye: Unanifaham?

Mimi: Ndio wewe ni mwalimu wangu wa somo flani nimemaliza mwaka jana.

Yeye: (Bado akiwa na wasiwasi) Nitaamini vipi na kwanini unanisimamisha kama jambazi?

Mimi: (Bila kujiuma uma) Naomba unisamehe sana Dr, ni kuvurugwa na hapa nimeopna kama bahati
kukuona. Dr mimi nipo katika harakati za kutafuta kazi, nimekusimamisha ili nikuacjie CV yangu maana naamini wewe network yako ni kubwa pengine unaweza ukaniconnect na wadau wako.
Yeye: (Akacheka sana huku akiniita niende upande wake). Kwa hiyo unatafuta kazi gani?

Mimi: Kwa sasa nahitaji sehemu yoyote ya kujishikiza ili nipate uzoefu, lakini uzuri wewe ni mwalimu wangu wa PM so unaweza ukaona ni wapi zile theory wapi naweza kuziapply.

Akaniangalia sana kisha akaniuliza unajua nini kuhusu project management na principles for effective project management? Nikamshushia madude kwa style ambayo nadhani ilimkamata kisawa sawa. nIkamsisitizia kwamba mimi sijawahi kushikwa kwenye somo lake. Baada ya kumjibu pale akaniambia. Mbona unaonekana una njaa sana? Shika hii nenda kale mimi nina mambo mengi sana na hapa unanichelewesha tuu. Sikupokea kwanza ile pesa ila nikamwambia Sir please just take my CV may you can see how you can help. Akaniuliza, sasa CV yako umeandika nini wakati hujawahi kufanya kazi popote? Halafu sina mda wa kutembea na makaratazi kwa gari yangu. Akawa anafunga kioo, asee nikaking’anga’ania. Akaniambia unataka nini sasa pesa nimekupa umekataa. Nikamwambia, kama huwezi kutembea na makaratasi basi naomba email address yako ili nikutumie. Akaniangaliaa, kisha akatoa business card akanipa. Mimi nikaicheki nikaona ile biz card sio yake ni ya mdada. Nikamwambia mbona sio yako. Akaniambia “vizuri sana upo makini, mpigie huyo dada simu kesho muda kama huu”. Hiyo ilikuwa ni kama saa tisa hivi. Kisha akanipa ile pesa, akasepa zake.

Mwendelezo #15
Hii inanikumbusha 2010 pale Exem Tower na Holiday Inn posta nilipoenda kuomba kazi.

Lete muendelezo mkuuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom