'Mama Anatosha' Hii ndiyo kauli mbiu ninayotamba nayo mitaani kwangu na kuungwa mkono kwa wingi

Ndugu zangu Watanzania,

Katika kuendelea kumuunga mkono ,kumsemea na kumtetea Rais Samia kwa kazi nzuri alizofanya ,anazofanya na anazoendelea kuzifanya katika Taifa letu nimekuja na kauli mbiu mpya kabisa ambayo natamba nayo mitaani na kuungwa mkono na watu wengi sana,ambao wameonyesha hisia kali sana za upendo mkubwa sana na kumuunga mkono Rais Samia.

Kauli mbiu hiyo inaitwa MAMA ANATOSHA .hii ni kauli mbiu niliyokaa chini nakuamua kuja nayo na kuona imekubalika kwa kiasi kikubwa sana na kupokelewa kwa mikono miwili. Nimeamua kuja na kauli mbiu hii baada ya kuona kuwa Rais Samia amefanya kazi kubwa sana za kuliinua Taifa letu kiuchumi na kuwakwamua kiuchumi watanzania. Ambapo ukienda katika kila Secta unakuta mikono yake na hatua kubwa za kimaendeleo zimepigwa.

Mfano katika kilimo ambapo ameongeza bajeti ya kilimo kutoka Billion mia mbili na point kufikia Billion 970. Rais samia na serikali yake amekuwa akitoa pia mabilioni ya Ruzuku katika pembejeo hususani mbolea na hivyo kuchochea uzalishaji ,na hivyo kuinua kipato cha kaya moja moja na mtu mmoja mmoja hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa letu. Kwa sasa kilimo ni kimbilio siyo tu la vijana bali na wasomi mbalimbali wamejiingiza katika kilimo.kwasasa kilimo ni Biashara na shughuli inayoheshika sana.

Katika Secta ya Afya nako ni mapinduzi matupu ambapo vituo mbalimbali vya afya vimejengwa maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwepo 234 ambavyo vilitokana na tozo kupitia miamala ya simu.Rais Samia pia ametiririsha zaidi ya Trilioni sita katika Secta ya Afya hali iliyochochea upatikanaji wa vifaa tiba ,dawa pamoja na wataalamu bingwa na bobezi katika magonjwa mbalimbali.ndio maana hata wagongwa wanaotoka nje ya nchi kuja kutibiwa hapa nchini imeongezeka sana kipindi hiki cha Urais wa Rais Samia. Na wakati huo huo wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kutoka hapa nchini wamepungua sana kutokana na kupatikana kwa huduma zote za kibingwa hapa hapa nchini kunakotokana na uwekezaji mkubwa wa mabilioni ya pesa uliofanywa na Mama mwenyewe na serikali yake.

Ukija katika suala la ajira unakuta maelfu ya ajira yametolewa kwa vijana na hivi karibuni serikali inakwenda kutoa ajira elfu 46 baada ya kupata kibali kutoka kwa Mh Rais. watumishi wa umma kwa sasa wanafanya kazi kwa amani baada ya kuwa wamepandishwa madaraja mserereko pamoja na kulipwa stahiki zao huku serikali ikiwa katika mchakato wa kuangalia upya suala la kikokotoo ambacho kimeonekana kupigiwa kelele na watu wengi na kuwakatisha tamaa wastaafu na wanaolekea kustaafu.

Rais Samia amepandisha mapato kufikia Trilioni 2.2 kwa njia ya amani kabisa kwa wafanya biashara kulipa wenyewe kwa hiyari yao wenyewe na kujiona fahari kulipa kodi kwa Taifa lao.ukienda katika masuala ya nishati,maji, miundombinu uwekezaji unakuta ni mafanikio matupu.

Ndio maana nikaja na kauli mbiu hii kuwa MAMA ANATOSHA ,kwa maana kuwa anatosha kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili kama Rais wetu na Amiri Jeshi mkuu wetu.. Nimeona tusiseme au kuishia kusema tu NASIMAMA na Rais Samia au MAMA, Bali tuende mbele zaidi na kusema kuwa Rais Samia ANATOSHA.

Maana kuna mtu anaweza kusema NASIMAMA na Rais Samia au MAMA halafu ukigeuka nyuma unakuta hayupo au yupo Bize na mambo yake au amesimama na wewe lakini ana imani na mtu mwingine na hapo yupo tu kama picha .au mtu anaweza kusema NASIMAMA na mama halafu kumbe yeye amesimama hapo tu kuangalia kinachoendelea lakini hayupo mahali hapo kifikira na kimawazo na kiimani.lakinii mtu akisema Mama ANATOSHA, maana yake anatosha kweli kweli na haijalishi mtu yupo mahali hapo au yupo vijijini lakini imani yake inabaki kuwa Mama ANATOSHA na hakuna cha kumzuia wala wa kumzuia kuendelea na muhula wa pili kuwatumikia watanzania.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.View attachment 2972006View attachment 2972007View attachment 2972008View attachment 2972010View attachment 2972011
Wanao Tamba naye ni:
1. Wajinga wa kutupwa.
2.punguani kama wewe
3.wamerogwa na muumba wa mbingu na nchi kama wewe
4. Matapeli
5. Misukule kama wewe
Mwenye akili na mpenda nchi kamwe hawezi chagua jitu dhaifu na la hovyo.
Wewe ni shetani na jinga. Mungu chukua hili lishetani haraka Sana lichome moto
 
Wanao Tamba naye ni:
1. Wajinga wa kutupwa.
2.punguani kama wewe
3.wamerogwa na muumba wa mbingu na nchi kama wewe
4. Matapeli
5. Misukule kama wewe
Mwenye akili na mpenda nchi kamwe hawezi chagua jitu dhaifu na la hovyo.
Wewe ni shetani na jinga. Mungu chukua hili lishetani haraka Sana lichome moto
Wewe hunaga akili kabisa. Ni kichaa usiyejitambua.
 
Huku mvua ikinyesha mimi nakimbilia kitanda kulala, ila sipendi mvua sababu inaleta uvivu
Poleeee Sanaaaa maana mvua za huko naona kwa sasa ni muda wote utafikiri mmepasua bomba la maji. Mnaweza jikuta mnalala muda wote utafikiri wagonjwa waliopooza mwili. Mungu awasaidie tu zisiwe na madhara makubwa.

Ila kama kawaida mimi naendelea kukuombea tu Mungu aendelee kukulinda na kuwa karibu yako ,huku moyo wangu nao ukiwa karibu yako utafikiri kope za macho.
 
Poleeee Sanaaaa maana mvua za huko naona kwa sasa ni muda wote utafikiri mmepasua bomba la maji. Mnaweza jikuta mnalala muda wote utafikiri wagonjwa waliopooza mwili. Mungu awasaidie tu zisiwe na madhara makubwa.

Ila kama kawaida mimi naendelea kukuombea tu Mungu aendelee kukulinda na kuwa karibu yako ,huku moyo wangu nao ukiwa karibu yako utafikiri kope za macho.
😂😂Utanivunja mbavu zangu
Leo usiku nitakuombea
 
Serikali ilitoleaga ufafanuzi kuwa viti na meza zao zilikuwa zinatengeneza na walipelekewa siku hiyo hiyo
Kabisa mama anatosha!

Mitano tena kwa mama.

#Nasimamanamama
IMG_20231105_173110.jpg
 
Usiku nitakuombea uje kua Rais ili nile mema ya nchi, kwanza nataka nione ikulu kule ndani kupoje nawaonea wivu wasanii wanavyoalikwa wanaenda kula misosi
Wala usijali ephen ,Muda wote utakuwa unashinda ikulu utafikiri wale ndege Tausi wa ikulu. Hata ukitaka jua la asubuhi uwe unaotea na kupiga mswaki ukiwa mbuga ya Serengeti itawezekana tu ephen.
 
Sisi ndio wananchi na ndio tunaona makubwa yaliyofanywa na Rais wetu mpendwa na ndio maana tunaendelea kuyatangaza kwa nguvu zote bila kuchoka. Wenye chuki binafsi mnaumia sana mnapoona kazi za Rais wetu mpendwa zikitangazwa na wananchi kwa hiyari yao kutokana na upendo mkubwa walio nao kwa Rais wao.
sijakataa kua wewe ni mwananchi na una haki ya kutoa maoni yako lakini usitumie wingi wakati uko peke yako! mimi naangalia vitu vichache sana kupima utendaji wa mtu si kufuata maneno ya kusombwa kwa wingi! sasa mtu anaupiga mwingi kwa kuruhusu bei ya sukari kua tsh 5000 kutoka 2500?bei ya petrol ambayo ndiyo huathiri kila kitu kufika 3500 na unasema ameupiga mwingi tuache unafiki kiasi tuanze kuongea kwa takwimu halisi za ulinganifu wa awali na sasa kwa kila kinachogusa maisha moja kwa moja tuuone huo mwingi
 
Back
Top Bottom