Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 16,171
- 10,655
- Thread starter
- #21
Asante kwa marekebishoKajifunze kwanza kuandika kiswahili. Siyo "anakubarika" bali "anakubalika".
Asante kwa marekebishoKajifunze kwanza kuandika kiswahili. Siyo "anakubarika" bali "anakubalika".
MAMA ANATOSHA kuendelea na muhula wa pili wa kuliongoza Taifa letu.Nitafsiri kitu kisichoandikwa??
Mnaposema anatosha muwe mnafafanua anatosha kwenye nini.
HATOSHI kuendelea kuwa kiongozi wetu.
Tanzania ni moja na watanzania ni wamoja .ndio maana Tunaendelea kujivunia muungano wetu huu adhimu kabisa.Kwenda kwao Kizimkazi wanataka uende Kwa Passport.
Hakuna "maulanzi" Kuna "ulanzi".Acha ujuha Allen ndugu yangu.maana majibu ya swali lako yanapatikana katika andiko langu.au tayari umeshajipakia maulanzi yako ya iringa😃😃😃
Anatosha nyumbani kwakoNdugu zangu Watanzania,
Katika kuendelea kumuunga mkono ,kumsemea na kumtetea Rais Samia kwa kazi nzuri alizofanya ,anazofanya na anazoendelea kuzifanya katika Taifa letu nimekuja na kauli mbiu mpya kabisa ambayo natamba nayo mitaani na kuungwa mkono na watu wengi sana,ambao wameonyesha hisia kali sana za upendo mkubwa sana na kumuunga mkono Rais Samia.
Kauli mbiu hiyo inaitwa MAMA ANATOSHA .hii ni kauli mbiu niliyokaa chini nakuamua kuja nayo na kuona imekubalika kwa kiasi kikubwa sana na kupokelewa kwa mikono miwili. Nimeamua kuja na kauli mbiu hii baada ya kuona kuwa Rais Samia amefanya kazi kubwa sana za kuliinua Taifa letu kiuchumi na kuwakwamua kiuchumi watanzania. Ambapo ukienda katika kila Secta unakuta mikono yake na hatua kubwa za kimaendeleo zimepigwa.
Mfano katika kilimo ambapo ameongeza bajeti ya kilimo kutoka Billion mia mbili na point kufikia Billion 970. Rais samia na serikali yake amekuwa akitoa pia mabilioni ya Ruzuku katika pembejeo hususani mbolea na hivyo kuchochea uzalishaji ,na hivyo kuinua kipato cha kaya moja moja na mtu mmoja mmoja hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa letu. Kwa sasa kilimo ni kimbilio siyo tu la vijana bali na wasomi mbalimbali wamejiingiza katika kilimo.kwasasa kilimo ni Biashara na shughuli inayoheshika sana.
Katika Secta ya Afya nako ni mapinduzi matupu ambapo vituo mbalimbali vya afya vimejengwa maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwepo 234 ambavyo vilitokana na tozo kupitia miamala ya simu.Rais Samia pia ametiririsha zaidi ya Trilioni sita katika Secta ya Afya hali iliyochochea upatikanaji wa vifaa tiba ,dawa pamoja na wataalamu bingwa na bobezi katika magonjwa mbalimbali.ndio maana hata wagongwa wanaotoka nje ya nchi kuja kutibiwa hapa nchini imeongezeka sana kipindi hiki cha Urais wa Rais Samia. Na wakati huo huo wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kutoka hapa nchini wamepungua sana kutokana na kupatikana kwa huduma zote za kibingwa hapa hapa nchini kunakotokana na uwekezaji mkubwa wa mabilioni ya pesa uliofanywa na Mama mwenyewe na serikali yake.
Ukija katika suala la ajira unakuta maelfu ya ajira yametolewa kwa vijana na hivi karibuni serikali inakwenda kutoa ajira elfu 46 baada ya kupata kibali kutoka kwa Mh Rais. watumishi wa umma kwa sasa wanafanya kazi kwa amani baada ya kuwa wamepandishwa madaraja mserereko pamoja na kulipwa stahiki zao huku serikali ikiwa katika mchakato wa kuangalia upya suala la kikokotoo ambacho kimeonekana kupigiwa kelele na watu wengi na kuwakatisha tamaa wastaafu na wanaolekea kustaafu.
Rais Samia amepandisha mapato kufikia Trilioni 2.2 kwa njia ya amani kabisa kwa wafanya biashara kulipa wenyewe kwa hiyari yao wenyewe na kujiona fahari kulipa kodi kwa Taifa lao.ukienda katika masuala ya nishati,maji, miundombinu uwekezaji unakuta ni mafanikio matupu.
Ndio maana nikaja na kauli mbiu hii kuwa MAMA ANATOSHA ,kwa maana kuwa anatosha kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili kama Rais wetu na Amiri Jeshi mkuu wetu.. Nimeona tusiseme au kuishia kusema tu NASIMAMA na Rais Samia au MAMA, Bali tuende mbele zaidi na kusema kuwa Rais Samia ANATOSHA.
Maana kuna mtu anaweza kusema NASIMAMA na Rais Samia au MAMA halafu ukigeuka nyuma unakuta hayupo au yupo Bize na mambo yake au amesimama na wewe lakini ana imani na mtu mwingine na hapo yupo tu kama picha .au mtu anaweza kusema NASIMAMA na mama halafu kumbe yeye amesimama hapo tu kuangalia kinachoendelea lakini hayupo mahali hapo kifikira na kimawazo na kiimani.lakinii mtu akisema Mama ANATOSHA, maana yake anatosha kweli kweli na haijalishi mtu yupo mahali hapo au yupo vijijini lakini imani yake inabaki kuwa Mama ANATOSHA na hakuna cha kumzuia wala wa kumzuia kuendelea na muhula wa pili kuwatumikia watanzania.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.View attachment 2972006View attachment 2972007View attachment 2972008View attachment 2972010View attachment 2972011
Utatakiwa uwe na Passport kwenda Kizimkazi.Tanzania ni moja na watanzania ni wamoja .ndio maana Tunaendelea kujivunia muungano wetu huu adhimu kabisa.
Anatosha kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.No kweli anatosha kupika ugali na kulea wajukuu kabisa au we unaonaje Mwaisa!!?
Hata Afrika ingekuwa ni nchi basi Rais Samia ndiye angetosha kuliongoza bara hilo la Afrika na kulipaisha kimaendeleoAnatosha nyumbani kwako
Hivi Alleni wewe ndiye ulikuwa unakuwa kwenye kipindi fulani hivi cha Ibon Fm pamoja na mwalimu fulani hivi wa pale MUCE mkifanya uchambuzi wa masuala mbalimbali siku ya jumamosi?Hakuna "maulanzi" Kuna "ulanzi".
Unapenda sana kuandika bandiko reefu wakati ulichoandika kingetosha kuandikwa kwa sentensi moja tu.
Siku hizi unakera sana, Kwa Nini umeacha kuweka namba yako ya simu.Hata Afrika ingekuwa ni nchi basi Rais Samia ndiye angetosha kuliongoza bara hilo la Afrika na kulipaisha kimaendeleo
Sijui...🤣🤣🤣😜Hivi Alleni wewe ndiye ulikuwa unakuwa kwenye kipindi fulani hivi cha Ibon Fm pamoja na mwalimu fulani hivi wa pale MUCE mkifanya uchambuzi wa masuala mbalimbali siku ya jumamosi?
Jibu swali acha ujinga hapa kama Ba vichaa 😃😃😃Sijui...🤣🤣🤣😜
Sijui siyo jibu!??Jibu swali acha ujinga hapa kama Ba vichaa 😃😃😃
Nijibu swali langu maana nilikuwa napenda sana kufuatilia kipindi hicho ambacho uchambuzi ulikuwa unakuwa mzuri kiukweli. nakumbuka ni kama kilikuwa kinaongozwa na dada mmoja anaitwa Neema Msafiri alikuwa anajiita Mama John kama sijakosea. Kipindi hicho nilikuwa naishi Iringa kwa miaka mitatu mpaka nilipoondoka 2016.
Sijui...😜😅😅🤣Nijibu swali langu maana nilikuwa napenda sana kufuatilia kipindi hicho ambacho uchambuzi ulikuwa unakuwa mzuri kiukweli. nakumbuka ni kama kilikuwa kinaongozwa na dada mmoja anaitwa Neema Msafiri alikuwa anajiita Mama John kama sijakosea. Kipindi hicho nilikuwa naishi Iringa kwa miaka mitatu mpaka nilipoondoka 2016.
Nashangaa sana Lucas Mwashambwa kaacha kuweka namba zake.Mkuu mm kazi yangu ni kukumbusha kuweka no za sim basi
Nimeacha ili nawe uweke namba yakoMkuu mm kazi yangu ni kukumbusha kuweka no za sim basi
Wahuni walimuita kwamba akachukue cheo, kufika huko wakampa onyoNashangaa sana @Lucas Mwashambwa kaacha kuweka namba zake.