Tundu Lissu aendelea kushambuliwa mitaani kwa kauli zake za kibaguzi na chuki

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
16,784
11,085
Ndugu zangu Watanzania,

Kauli za kibaguzi ambazo zimetolewa na zimekuwa zikitolewa kupitia mdomo wa Lissu zimeendelea kulaaniwa na kukemewa sana na watanzania maeneo mbalimbali nchini. Ambapo watanzania wengi wameonyesha kuchukizwa na kauli za Lissu ambazo zinatokana na uchu na uroho wake wa madaraka.

Watanzania wanapinga na kukemea sana ubaguzi na chuki inayopandikizwa na Lissu ,ambapo hata hivyo watanzania wamekataa na kugoma kabisa kuingia katika mtego huo wa kutaka kuwagawa. ikumbukwe ya kuwa Lissu hana uchungu wa aina yoyote ile na Taifa letu pale litakapogawanyika na kupasuka vipande vipande au kutokea machafuko hapa nchini.

Hii ni kwa kuwa watoto wa Lissu wana Uraia wa Marekani ,kauli ambayo amewahi kuitoa na kukili kwa mdomo wake mwenyewe lissu .kwa mantiki hiyo mnaweza kutambua kwa nini Lissu hana habari wala uoga wala hofu wala aibu ya kupandikiza chuki na ubaguzi hapa nchini. Yeye hata yakitokea machafuko leo ,basi yeye kesho yake anapanda zake ndege na kwenda ulaya au Marekani kutulia na familia yake akiwa ameshika kinywaji mkononi mwake kupeleka mdomoni mwake, huku akiangalia kupitia Tvs namna watanzania wanavyohangaika na kuteseka,huku akina mama wakiwa na watoto migongoni na wengine wajawazito wakilia kwa uchungu pasipo msaada.

Mtakumbuka hata 2020 alipotaka watanzania waandamane halafu yeye akaenda kujificha ubalozini huku akiwa na tiketi ya ndege mkononi mwake kwa ajili ya kwenda ulaya kula upepo. Sasa hamjiulizi kwanini alikwenda kujificha ubalozini? Kama alikuwa anakiogopa kifo ,je alitaka mtoto wa nani ndio afe kwa ajili ya maslahi yake binafsi? Kwanini asingetoka hadharani aongoze maandamano kama walivyokuwa wakifanya akina Dkt Martin Luther King junior kule Marekani?

Kwanini alitaka awarubuni watanzania wakati yeye tayari anayo tiketi ya ndege mfukoni na mipango ya kusindikizwa hadi uwanja wa ndege kupanda ndege kwenda ulaya? Uzalendo wake ulikuwa wapi? Alitaka nani aongoze hayo maandamano ikiwa muanzisha maandamano alikuwa msitari wa mbele kutimua mbio? Je siyo kwamba alikuwa anataka awalaghai watanzania na kusababisha machafuko hapa nchini kwa maslahi yake binafsi?

Sasa Lissu baada ya kuona watanzania wamekuwa wakimgomea kuandamana,ameamua kuanza kutumia njia nyingine ya kutaka kupandikiza mbegu ya ubaguzi,chuki,uhasama pamoja na kuleta nyufa na mpasuko kwa Taifa letu. Hii ni baada ya kuishiwa hoja ,sera na ajenda zenye kugusa maisha ya watu na kupata uungwaji mkono. lakini bado watanzania wamesimama kidete kupinga kauli zake za kibaguzi na zenye lengo la kujenga chuki na uhasama miongoni mwa watanzania.

Hayati Baba wa Taifa amewahi kutuasa na kutumbia kuwa kuna watu wakikosa hoja na sera za kuwashawishi watanzania kuwapigia kura ,huanza kutumia hoja za ubaguzi kwa misingi ya Udini au ukabila. Sasa ndio haya tunayo yaona kwa Lissu leo hii akitumia katika kutaka kupata uungwaji mkono kwa njia ya kuwagawa watu na kulisambaratisha Taifa letu ,baada ya kuwa amefirisika kisera.

Watanzania tumuogope na kuwaogopa kama ukoma watu aina ya Lissu wanaotaka kutugawa na kulisambaratisha na kulipasua Taifa letu kwa kauli za kibaguzi. Tumkemee na tuungane kumkataa Lissu na CHADEMA yake dhidi ya kauli zao chafu za kibaguzi. Tuwakatae kuanzia mitaani hadi katika sanduku la kura lolote lile watakaloweka wagombea wao.

Tuwaambie kuwa tunahitaji siasa safi,siasa za hoja,ajenda,sera na ushindani wa mbinu bora za kutatua kero zilizopo pamoja na kulipeleka mbele Taifa letu likiwa moja,lenye amani,upendo, utulivu na mshikamano. Kama siyo amani na utulivu huu uliotamalaki hapa Nchini, hao akina Lissu wasingepata nafasi ya kutoa maneno yao hayo machafu ya kibaguzi.tuulinde Muungano wetu na Taifa letu na umoja wake. Lissu kama amechoka kuishi hapa nchini basi ni bora aondoke haraka sana Nchini na siyo kupandikiza chuki ambazo haziwezi kamwe mpatia hata kura moja tu kwenye sanduku la kura.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Bandiko lako ndefu mno alafu hakuna point yeyote ya maana na hata huo ubaguzi unaosema umeshindwa kuonesha, badala ya kutuonesha ubaguzi wa LISSU umeishia kuongelea familia yake Tu.

Uzuri Kwa LISSU mkianza kuandika namna hii kesho atakuja na ujio wa makombora mengine mpaka mkimbie
 
Hata akizungumza vipi bado hatapata uungwaji mkono kutoka kwa watanzania,maana hakuna mtanzania mzalendo aliyetayari kuona Taifa letu likipandikizwa chuki na ubaguzi kwa maslahi ya mtu mmoja na chama chake kwa uchu na uroho wao wa madaraka.ambayo wameshindwa kuyapata kwa njia za kushawishi watu kuwaunga mkono.
 
Hamna mahali lissu kapindikiza chuki, ila ame state obvious facts, Muungano una shida, and it seems upande mmoja una faidishwa ,unasikilizwa kuliko mwingine why?
 
Sijui mitaa gani iyo? Mm nilipo wanampongeza na wanataka agombee ubunge kabisa mwakani.

KAZI ni kipimo cha UTU
Naona mmeanza kusema agombee ubunge baada ya kuona kwenye Urais Kila mwenye akili Timamu anamkataa na kumpinga vikali,kuwa hawezi na hafai kuongoza hata ubalozi tu wa nyumba kumi.
 
Hamna mahali lissu kapindikiza chuki, ila ame state obvious facts, Muungano una shida, and it seems upande mmoja una faidishwa ,unasikilizwa kuliko mwingine why?
Basi itakuwa una matatizo ikiwa umeshindwa kuona ubaguzi katika kauli zinazotolewa kwenye mdomo wa Lissu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kauli za kibaguzi ambazo zimetolewa na zimekuwa zikitolewa kupitia mdomo wa Lissu zimeendelea kulaaniwa na kukemewa sana na watanzania maeneo mbalimbali nchini. Ambapo watanzania wengi wameonyesha kuchukizwa na kauli za Lissu ambazo zinatokana na uchu na uroho wake wa madaraka.

Watanzania wanapinga na kukemea sana ubaguzi na chuki inayopandikizwa na Lissu ,ambapo hata hivyo watanzania wamekataa na kugoma kabisa kuingia katika mtego huo wa kutaka kuwagawa. ikumbukwe ya kuwa Lissu hana uchungu wa aina yoyote ile na Taifa letu pale litakapogawanyika na kupasuka vipande vipande au kutokea machafuko hapa nchini.

Hii ni kwa kuwa watoto wa Lissu wana Uraia wa Marekani ,kauli ambayo amewahi kuitoa na kukili kwa mdomo wake mwenyewe lissu .kwa mantiki hiyo mnaweza kutambua kwa nini Lissu hana habari wala uoga wala hofu wala aibu ya kupandikiza chuki na ubaguzi hapa nchini. Yeye hata yakitokea machafuko leo ,basi yeye kesho yake anapanda zake ndege na kwenda ulaya au Marekani kutulia na familia yake akiwa ameshika kinywaji mkononi mwake kupeleka mdomoni mwake, huku akiangalia kupitia Tvs namna watanzania wanavyohangaika na kuteseka,huku akina mama wakiwa na watoto migongoni na wengine wajawazito wakilia kwa uchungu pasipo msaada.

Mtakumbuka hata 2020 alipotaka watanzania waandamane halafu yeye akaenda kujificha ubalozini huku akiwa na tiketi ya ndege mkononi mwake kwa ajili ya kwenda ulaya kula upepo. Sasa hamjiulizi kwanini alikwenda kujificha ubalozini? Kama alikuwa anakiogopa kifo ,je alitaka mtoto wa nani ndio afe kwa ajili ya maslahi yake binafsi? Kwanini asingetoka hadharani aongoze maandamano kama walivyokuwa wakifanya akina Dkt Martin Luther King junior kule Marekani?

Kwanini alitaka awarubini watanzania wakati yeye tayari anayo tiketi ya ndege mfukoni na mipango ya kusindikizwa hadi uwanja wa ndege kupanda ndege kwenda ulaya? Uzalendo wake ulikuwa wapi? Alitaka nani aongoze hayo maandamano ikiwa muanzisha maandamano alikuwa msitari wa mbele kutimua mbio? Je siyo kwamba alikuwa anataka awalaghai watanzania na kusababisha machafuko hapa nchini kwa maslahi yake binafsi?

Sasa Lissu baada ya kuona watanzania wamekuwa wakimgomea kuandamana,ameamua kuanza kutumia njia nyingine ya kutaka kupandikiza mbegu ya ubaguzi,chuki,uhasama pamoja na kuleta nyufa na mpasuko kwa Taifa letu. Hii ni baada ya kuishiwa hoja ,sera na ajenda zenye kugusa maisha ya watu na kupata uungwaji mkono. lakini bado watanzania wamesimama kidete kupinga kauli zake za kibaguzi na zenye lengo la kujenga chuki na uhasama miongoni mwa watanzania.

Hayati Baba wa Taifa amewahi kutuasa na kutumbia kuwa kuna watu wakikosa hoja na sera za kuwashawishi watanzania kuwapigia kura ,huanza kutumia hoja za ubaguzi kwa misingi ya Udini au ukabila. Sasa ndio haya tunayo yaona kwa Lissu leo hii akitumia katika kutaka kupata uungwaji mkono kwa njia ya kuwagawa na kulisambaratisha Taifa letu ,baada ya kuwa amefirisika kisera.

Watanzania tumuogope na kuwaogopa kama ukoma watu aina ya Lissu wanaotaka kutugawa watanzania na kulisambaratisha na kulipasua Taifa letu kwa kauli za kibaguzi. Tumkemee na tuungane kumkataa Lissu na CHADEMA yake dhidi ya kauli zao chafu za kibaguzi. Tuwakatae kuanzia mitaani hadi katika sanduku la kura lolote lile watakaloweka wagombea wao.

Tuwaambie kuwa tunahitaji siasa safi,siasa za hoja,ajenda,sera na ushindani wa mbinu bora za kutatua kero zilizopo pamoja na kulipeleka mbele Taifa letu likiwa moja,lenye amani,upendo, utulivu na mshikamano. Kama siyo amani na utulivu huu uliotamalika hapa Nchini, hao akina Lissu wasingepata nafasi ya kutoa maneno yao hayo machafu ya kibaguzi.tuulinde Muungano wetu na Taifa letu na umoja wake. Lissu kama amechoka kuishi hapa nchini basi ni bora aondoke haraka sana Nchini na siyo kupandikiza chuki ambazo haziwezi kamwe mpatia hata kura moja tu kwenye sanduku la kura.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Punguani, ulichobakiza ni kuokota makopo na kutembea na suruali begani. Hayo yanakuja kwa upande wako, kwa sababu hatua zote za awali za uwendawazimu na unafiki umekwishazipita.
 
Utaungana na punguani wenzako. Wenye akili wote wakiwemo baadhi ya viongozi wa CCM wanamshukuru sana Lisu, japo siyo kwa kutangaza hadharani.
Ungesubiri mada na hoja zenye kulingana na akili yako. Nikiweka nitakwambia maana hii ipo juu ya uwezo wako.
 
Back
Top Bottom