Mdomo wa Lissu haujawahi kuwa na adabu wala hekima

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,994
10,481
Ndugu zangu Watanzania,

Huwa nashangaa sana ni vipi Lissu ni kiongozi ndani ya CHADEMA, ni vipi watu wenye akili timamu na wanaojitambua wanaweza kumpatia Lissu uongozi wa juu wa chama, nafasi inayohitaji mtu mwenye hekima, busara, staha na nidhamu ya kiuongozi?

Ni vipi chama kikuu cha upinzani kinaweza kumpa uongozi mtu mropokaji na asiye juwa aongee nini awapo jukwaani? Ni vipi Lissu aliyekosa adabu, mbaguzi, mropokaji na mwenye mihemuko anaweza kuwa kiongozi wa juu ndani ya chama katika nafasi anayokuwa kama mlezi wa chama hasa vijana na viongozi wengine wanaochipukia?

Kipi unachoweza kujifunza kutoka kwa Lissu kiuongozi? Ni mtu ambaye mdomo wake haujawahi kuwa na adabu wala staha wala hekima wala busara za aina yoyote ile ya kiuongozi. Ni aibu na fedheha kubwa sana kuona mtu mzima kama Lissu akitoa maneno ya kibaguzi na chuki pasipo hoja za msingi.

Ni kukosa kwa adabu na hekima kwa Lissu na malezi mabaya aliyokulia na kukuzwa nayo ,amewahi kumtukana Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ndani ya Bunge la katiba. Jambo ambalo liliishitua nchi na Taifa zima kwa ujumla wake. Kumtukana mtu na kiongozi anayeheshimika na kuheshimiwa na Dunia nzima. Lakini kwa kukosa kwake adabu alimtukana mtu ambaye alikuwa amelala ardhini na hana uwezo wa kufumbua mdomo kujitetea.

Kwa hakika hii ilikuwa ni laana kubwa sana inayoendelea na itakayoendelea kumuandama mtu huyu aliyekosa adabu na mwenye kuonekana kama ana matatizo fulani kichwani mwake. Sasa baada ya kulewa na uhuru uliotolewa na kuruhusiwa na serikali ya Rais Samia ,ameanza kutoa lugha za kibaguzi, kuchochea machafuko na kuhamasisha kuvunjwa kwa muungano wetu adhimu. Lakini hajaishia hapo bali amekwenda mbali zaidi kwa kuanza kumshambulia Rais wetu mpendwa pamoja na Familia yake.

Hii yote ni kutafuta chokochoko na kutaka ajibiwe ili aendelee kubwatuka zaidi.jambo naloamini kuwa Rais wetu hatamjibu chochote na badala yake atampuuza na kuendelea na kazi yake ya kuwatumikia watanzania na kuwainua kiuchumi.

Kizuri zaidi ni kuwa watanzania wamekataa kabisa kumsikiliza na kumuunga mkono ujinga wake wa kutaka kutugawa kama Taifa pamoja na kutaka kupandikiza mbegu ya chuki na uhasama sisi kwa sisi. Watanzania wamegoma kubeba mawazo hayo ya kijinga vichwani na akilini mwao na badala yake wanaendelea kulaani kauli hizo chafu na zisizokubalika kabisa hapa Nchini. Na wameahidi kuwaadhibu kisawasawa katika sanduku la kura ikiwa watashiriki uchaguzi wowote ule.

Rais wetu namuomba aendelee na kazi za kugusa maisha ya watanzania na wala asimjibu chochote kile huyu mtu anayeonekana kukosa adabu na malezi mazuri. Maana lengo lake anataka ajibiwe .chapa kazi Rais wetu na songa mbele kwa kishindo kwa kuwa mamilioni ya watanzania wapo upande wako.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Ccm bwana! Mtu akiwa msema kweli anasakamwa kweli kweli!.

Kuna chochote alichosema Lisu ambacho siyo cha kweli ama chenye ukakasi??
Ni vipi mtu mwenye akili Timamu unaweza kuunga mkono kauli za kibaguzi na ubaguzi za Lissu? Ni vipi unaweza unga mkono kauli zake za kichochezi na kutaka kupandikiza mbegu za chuki kwa wananchi? Lissu anapaswa kupingwa na kukemewa na kila mtanzania mwenye akili Timamu na mwenye mapenzi mema na Taifa letu.
 
Wee luca hebu jibu hoja za TL acha kutoa maneno ya kutisha na kukemea, km huna hoja si ukae kimya? Kwan CCM mwanachama wee pekee ako?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Huwa nashangaa sana ni vipi Lissu ni kiongozi ndani ya CHADEMA, ni vipi watu wenye akili timamu na wanaojitambua wanaweza kumpatia Lissu uongozi wa juu wa chama, nafasi inayohitaji mtu mwenye hekima, busara, staha na nidhamu ya kiuongozi?

Ni vipi chama kikuu cha upinzani kinaweza kumpa uongozi mtu mropokaji na asiye juwa aongee nini awapo jukwaani? Ni vipi Lissu aliyekosa adabu, mbaguzi, mropokaji na mwenye mihemuko anaweza kuwa kiongozi wa juu ndani ya chama katika nafasi anayokuwa kama mlezi wa chama hasa vijana na viongozi wengine wanaochipukia?

Kipi unachoweza kujifunza kutoka kwa Lissu kiuongozi? Ni mtu ambaye mdomo wake haujawahi kuwa na adabu wala staha wala hekima wala busara za aina yoyote ile ya kiuongozi. Ni aibu na fedheha kubwa sana kuona mtu mzima kama Lissu akitoa maneno ya kibaguzi na chuki pasipo hoja za msingi.

Ni kukosa kwa adabu na hekima kwa Lissu na malezi mabaya aliyokulia na kukuzwa nayo ,amewahi kumtukana Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ndani ya Bunge la katiba. Jambo ambalo liliishitua nchi na Taifa zima kwa ujumla wake. Kumtukana mtu na kiongozi anayeheshimika na kuheshimiwa na Dunia nzima. Lakini kwa kukosa kwake adabu alimtukana mtu ambaye alikuwa amelala ardhini na hana uwezo wa kufumbua mdomo kujitetea.

Kwa hakika hii ilikuwa ni laana kubwa sana inayoendelea na itakayoendelea kumuandama mtu huyu aliyekosa adabu na mwenye kuonekana kama ana matatizo fulani kichwani mwake. Sasa baada ya kulewa na uhuru uliotolewa na kuruhusiwa na serikali ya Rais Samia ,ameanza kutoa lugha za kibaguzi, kuchochea machafuko na kuhamasisha kuvunjwa kwa muungano wetu adhimu. Lakini hajaishia hapo bali amekwenda mbali zaidi kwa kuanza kumshambulia Rais wetu mpendwa pamoja na Familia yake.

Hii yote ni kutafuta chokochoko na kutaka ajibiwe ili aendelee kubwatuka zaidi.jambo naloamini kuwa Rais wetu hatamjibu chochote na badala yake atampuuza na kuendelea na kazi yake ya kuwatumikia watanzania na kuwainua kiuchumi.

Kizuri zaidi ni kuwa watanzania wamekataa kabisa kumsikiliza na kumuunga mkono ujinga wake wa kutaka kutugawa kama Taifa pamoja na kutaka kupandikiza mbegu ya chuki na uhasama sisi kwa sisi. Watanzania wamegoma kubeba mawazo hayo ya kijinga vichwani na akilini mwao na badala yake wanaendelea kulaani kauli hizo chafu na zisizokubalika kabisa hapa Nchini. Na wameahidi kuwaadhibu kisawasawa katika sanduku la kura ikiwa watashiriki uchaguzi wowote ule.

Rais wetu namuomba aendelee na kazi za kugusa maisha ya watanzania na wala asimjibu chochote kile huyu mtu anayeonekana kukosa adabu na malezi mazuri. Maana lengo lake anataka ajibiwe .chapa kazi Rais wetu na songa mbele kwa kishindo kwa kuwa mamilioni ya watanzania wapo upande wako.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Mdomo wake uwe na adabu kwa majizi?
 
Back
Top Bottom