Ni nani wa kujibu hoja za Tundu Lissu?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,819
23,699
Salaam, Shalom.

Ni wiki sasa, Mwanasheria msomi Tundu Lissu ametoa HOJA nzito kuhusiana na Muungano wetu, bandari, na anatoa HOJA Kwa kutumia Katiba ya nchi iliyopo.

Cha kushangaza wanaibuka viongozi tena wenye hadhi ya juu kabisa kimamlaka na kumjibu TUNDU Lissu kiujumla jumla tu. Anauliza swali Kwa kunukuu Katiba ya nchi, lakini anajibiwa Kwa kauli nyepesi za kisiasa bila ushahidi wowote au nukuu yoyote kisheria, imekaaje hii?

Jamani, HOJA hujibiwa Kwa HOJA,

Angalau Serikali chini ya AG ingeitisha mdahalo wa wazi, Lissu akaalikwa na HOJA muhimu zikajadiliwa Kwa maslah ya Taifa Kwa uelewa wa umma wa wananchi.

Swali linabaki kuwa, huko serikalini hawapo watu wenye capacity ya kumjibu TUNDU Lissu Kwa HOJA?

Karibuni🙏
 
Salaam, Shalom.

Ni wiki sasa, Mwanasheria msomi Tundu Lissu ametoa HOJA nzito kuhusiana na Muungano wetu, na anatoa HOJA Kwa kutumia Katiba ya nchi iliyopo...
Kumpuuza nalo ni jibu tosha, kwani hayo kaanza kuyaongea leo?
 
Nchi hii Pana wasomi wengi,

Ungeitishwa mdahalo, waitwe viongozi wenye weledi kuhusiana na masuala hayo ya kisheria na kikatiba, Lissu aalikwe zijadiliwe HOJA hizo muhimu,

Uchaguzi umekaribia, wananchi wangependa kuwajua viongozi wanaoijua Katiba na Sheria za Nchi yetu Ili wapewe kuongoza.
 
Ametoa HOJA kuwa bandari zetu zote za bara wamepewa waarabu,

Lakini Bandari za Zanzibar hazijaguswa,

HOJA kama hiyo Badala ya kulijibu unaamua kuipuuza kweli?
ni ya kupuuza kabisa, kwasababu tayari mambo hayo yaliisha kwa mujibu wa sheria :whatBlink:
 
🇹🇿 Huyo Hana hoja yoyote na ni mazuzu tuu wanamwona anaongea point kumbe kupayuka kote ni vapor tuu

🔹 Kwa makusudi anajua accord ya muungano wetu kuwa unique dunia nzima ei Neither federal nor unitary

🔹 Inajulikana kabisa na sababu zilitolewa kuwa hakuna kitu kinachoitwa Tanganyika kwa Sasa kwa sababu ili surrender all it's power kwenye muungano na ila dissolve lakini Zanzibar ili surrender some na ku retain some.
🔹 Ndio maana Zanzibar Wana sub katiba Yao, ndio maana Zanzibar Wana sub citizenship Yao. Lengo ilikuwa ni kutokana na udogo wake is dissolve Moja kwa Moja kwenye muungano

🔹 Hivyo vi hoja kuwa Kwa nini Wana vitbulisho vya ukaazi ni hoja dhaifu Sana kwani ni sawa sawa na ninyi mlivyo kwenye daftari la ukoo

🔹 Kitendo Cha baadhi ya mazuzu kuulazimisha au kuleta hoja kana kwamba hii ni purely unitary ni utaahira.

🔵 Haya ma federation na ma unitary mnayoyadoma duniani yalianzishwa na watu. Kwa nini msiwapongeze wazee wetu Nyerere na karume kwa kutunga muungano ambao ni unique na unauoumiza vichwa vya wasomali.duniani kote kuufanyia utafiti ? Kwa nini tusiwape u proffesa waasisi Hawa na kuwapa credit zao?

🔹 Wazazabari na wazanzibari na wazanzibari ni Watanzania. Watanzania bara ni Watanzania . Utake ni hivyo hivyo usitake ni hivyo hivyo
 
Back
Top Bottom