Hongera Kinana kwa kumjibu Tundu Lissu ila kazi bado ipo

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,247
26,149
Katika CCM ya sasa watu pekee ambao naweza kusema wana maarifa na uwezo wa kuweza kujibu hoja nzito za wapinzani na Watanzania ni Makamu Mwenyekiti wa chama Ndug. Abdulrahman Kinana na Katibu Mkuu Ndug. Emmanuel Nchimbi.

Kitendo cha Kinana leo kutoka na kumjibu Lissu kimeonesha kuwa japo huyu mtu sasa anazeeka ila bado ana uwezo mkubwa sana wa kujibu hoja za Wapinzania na angalau akaeleweka kwa Jamii ya watu wasomi wanaofikiri vizuri.

Pamoja na kuweza kuzijibu hoja za Tundu Lissu japo si kwa kiwango ambacho wengi walitegemea hasa kwenye maswali magumu ya Katiba yetu na masuala ya Muungano naweza kusema huko mbeleni suala la Katiba na Muungano zinaweza kuwa hoja ngumu sana kwa CCM

Maswali ya Lissu kuhusu wazanzibari kushika nafasi Tanzania Bara ambazo hazihusiani na masuala ya Muungano, pamoja na Katiba yetu kuwapa nguvu wanasiasa zaidi ya wataalam na kutoweka mazingira ya kuwawajibisha wanasiasa ni hoja nzito sana ambazo nina uhakika kwa kadri siku zinavyokwenda zitawapa wana CCM wakati mgumu sana katika kuzijibu.

Mimi ni CCM ila napenda kukiri kati ya Mambo ambayo ni lazima yafanyiwe kazi sasa ni:

1. Kukubaliana na Mawazo ya Marehemu Rais Karume kwa kuufanya Muungano wetu kuwa wa Nchi Moja na Serikali Moja

2. Kurekebisha Katiba iliyopo au kuja na Katiba mpya ambayo itaweka iwajibikaji wa Wanasiasa na Viongozi kwa Wananchi kiasi ambacho itamlazimu Kiongozi kuiheshimu na kuilinda katiba ambayo itambana kutofanya jambo lolote kinyume na Katiba.
 
05 May 2024

Abdulrahman Kinana Amvaa Tundu Lissu Suala la Rais Mzanzibari, "Nani Amekataa?
".

View: https://m.youtube.com/watch?v=zFJ1jRSRBXs
Leo Mei 5,2024, Makamu Mwenyekiti wa CCM anazungumza na waandishi wa habari na wanaCCM katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma. Anategemewa kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo kujibu shutuma mbalimbali zilizoibuliwa na upinzani ambazo CCM wameziita ni za kibaguzi dhidi ya Muungano.
 
😂😂😂

Unadhani kwanini Nyerere na Karume walikuja na Muungano wa Serikali mbili na siyo moja?

Ukinijibu kwa mfumo wa Hesabu za Seti Darasa la Pili nitakuelewa Vizuri
Mfumo huu wa Muungano ni wazo la Nyerere na wala halikuwa pendekezo la Karume.

Kwa hali ilivyo na tunavyoelekea huko mbele itakuwa shida sana kuutetea huu muungano hasa watanganyika wakiona kuna watu wananufaika zaidi na what is called Muungano kuliko wao.

Hata zinazosemwa kero za Muungano ukiangalia kwa undani suluhisho lake sio Serikali 2 au 3 bali ni Serikali 1

Kuna mambo kama tunaipenda lweli nchi yetu ni lazima tuyafanyie maamuzi sasa.
 
Sera ya muungano ilikuwa hoja ya act wazakendo, sera ya muungano ilikuwa sera ya DP sasa hawa washenzi washaacha sera zao za kupambana na ufisadi na kupigania utalawala wa majimbo sasa wamerukia sera zingine kabisa yaani wanayumba ka ngama ya wakara
 
Katika CCM ya sasa watu pekee ambao naweza kusema wana maarifa na uwezo wa kuweza kujibu hoja nzito za wapinzani na Watanzania ni Makamu Mwenyekiti wa chama Ndug. Abdulrahman Kinana na Katibu Mkuu Ndug. Emmanuel Nchimbi.

Kitendo cha Kinana leo kutoka na kumjibu Lissu kimeonesha kuwa japo huyu mtu sasa anazeeka ila bado ana uwezo mkubwa sana wa kujibu hoja za Wapinzania na angalau akaeleweka kwa Jamii ya watu wasomi wanaofikiri vizuri.

Pamoja na kuweza kuzijibu hoja za Tundu Lissu japo si kwa kiwango ambacho wengi walitegemea hasa kwenye maswali magumu ya Katiba yetu na masuala ya Muungano naweza kusema huko mbeleni suala la Katiba na Muungano zinaweza kuwa hoja ngumu sana kwa CCM

Maswali ya Lissu kuhusu wazanzibari kushika nafasi Tanzania Bara ambazo hazihusiani na masuala ya Muungano, pamoja na Katiba yetu kuwapa nguvu wanasiasa zaidi ya wataalam na kutoweka mazingira ya kuwawajibisha wanasiasa ni hoja nzito sana ambazo nina uhakika kwa kadri siku zinavyokwenda zitawapa wana CCM wakati mgumu sana katika kuzijibu.

Mimi ni CCM ila napenda kukiri kati ya Mambo ambayo ni lazima yafanyiwe kazi sasa ni:

1. Kukubaliana na Mawazo ya Marehemu Rais Karume kwa kuufanya Muungano wetu kuwa wa Nchi Moja na Serikali Moja

2. Kurekebisha Katiba iliyopo au kuja na Katiba mpya ambayo itaweka iwajibikaji wa Wanasiasa na Viongozi kwa Wananchi kiasi ambacho itamlazimu Kiongozi kuiheshimu na kuilinda katiba ambayo itambana kutofanya jambo lolote kinyume na Katiba.
Kinana hajajibu chochote ni brainwasher, alichokisema hakina mashiko ni kama ametupa wanachama lambalamba siku ipite, personally sijaona hoja
 
Kinana ni hazina ya taifa
Ni Mwanasiasa mahiri zaidi kuwahi kutokea katika karne hii kwa Chama cha Mapinduzi. Ndo mana aliaminiwa kuwa campaing manager na Mkapa then Kikwete na akaongoza Jahazi kuongoza kampeni za Magufuli 2015.

Hofu yangu ni kama akiondoka CCM watapata wapi mtu wa haiba na uwezo wake? Maana hawa waliopo sasa na tunaowaona wote ni weupe kupindukia, wanaweza siasa za kiki tu na sio hoja!
 
Kinana hajajibu chochote ni brainwasher, alichokisema hakina mashiko ni kama ametupa wanachama lambalamba siku ipite, personally sijaona hoja
Kuna hoja kaweza kuzipangua kwa mifano. Hasa issue ya wingi wa watu na uwakilishi. Tena katoa mifano hai kabisa kutoka nchi mbalimbali.

Ila kwenye Katiba na Muungano hapo tutamuonea. Pale hata Malaika hawezi toa majibu yatakayoeleweka.

Hivi unamshawishi vipi mtu kuwa Mzanzibar anaweza kuteuliwa DC Tanganyika na Mtanganyika hawezi kuteuliwa DC Zanzibar? Hapo kwenye Muungano na Katiba kusema kweli tupaweke sawa tu. Hakuna anayeweza kupajibia
 
Back
Top Bottom