'Mama Anatosha' Hii ndiyo kauli mbiu ninayotamba nayo mitaani kwangu na kuungwa mkono kwa wingi

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,605
10,000
Ndugu zangu Watanzania,

Katika kuendelea kumuunga mkono ,kumsemea na kumtetea Rais Samia kwa kazi nzuri alizofanya ,anazofanya na anazoendelea kuzifanya katika Taifa letu nimekuja na kauli mbiu mpya kabisa ambayo natamba nayo mitaani na kuungwa mkono na watu wengi sana,ambao wameonyesha hisia kali sana za upendo mkubwa sana na kumuunga mkono Rais Samia.

Kauli mbiu hiyo inaitwa MAMA ANATOSHA .hii ni kauli mbiu niliyokaa chini nakuamua kuja nayo na kuona imekubalika kwa kiasi kikubwa sana na kupokelewa kwa mikono miwili. Nimeamua kuja na kauli mbiu hii baada ya kuona kuwa Rais Samia amefanya kazi kubwa sana za kuliinua Taifa letu kiuchumi na kuwakwamua kiuchumi watanzania. Ambapo ukienda katika kila Secta unakuta mikono yake na hatua kubwa za kimaendeleo zimepigwa.

Mfano katika kilimo ambapo ameongeza bajeti ya kilimo kutoka Billion mia mbili na point kufikia Billion 970. Rais samia na serikali yake amekuwa akitoa pia mabilioni ya Ruzuku katika pembejeo hususani mbolea na hivyo kuchochea uzalishaji ,na hivyo kuinua kipato cha kaya moja moja na mtu mmoja mmoja hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa letu. Kwa sasa kilimo ni kimbilio siyo tu la vijana bali na wasomi mbalimbali wamejiingiza katika kilimo.kwasasa kilimo ni Biashara na shughuli inayoheshika sana.

Katika Secta ya Afya nako ni mapinduzi matupu ambapo vituo mbalimbali vya afya vimejengwa maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwepo 234 ambavyo vilitokana na tozo kupitia miamala ya simu.Rais Samia pia ametiririsha zaidi ya Trilioni sita katika Secta ya Afya hali iliyochochea upatikanaji wa vifaa tiba ,dawa pamoja na wataalamu bingwa na bobezi katika magonjwa mbalimbali.ndio maana hata wagongwa wanaotoka nje ya nchi kuja kutibiwa hapa nchini imeongezeka sana kipindi hiki cha Urais wa Rais Samia. Na wakati huo huo wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kutoka hapa nchini wamepungua sana kutokana na kupatikana kwa huduma zote za kibingwa hapa hapa nchini kunakotokana na uwekezaji mkubwa wa mabilioni ya pesa uliofanywa na Mama mwenyewe na serikali yake.

Ukija katika suala la ajira unakuta maelfu ya ajira yametolewa kwa vijana na hivi karibuni serikali inakwenda kutoa ajira elfu 46 baada ya kupata kibali kutoka kwa Mh Rais. watumishi wa umma kwa sasa wanafanya kazi kwa amani baada ya kuwa wamepandishwa madaraja mserereko pamoja na kulipwa stahiki zao huku serikali ikiwa katika mchakato wa kuangalia upya suala la kikokotoo ambacho kimeonekana kupigiwa kelele na watu wengi na kuwakatisha tamaa wastaafu na wanaolekea kustaafu.

Rais Samia amepandisha mapato kufikia Trilioni 2.2 kwa njia ya amani kabisa kwa wafanya biashara kulipa wenyewe kwa hiyari yao wenyewe na kujiona fahari kulipa kodi kwa Taifa lao.ukienda katika masuala ya nishati,maji, miundombinu uwekezaji unakuta ni mafanikio matupu.

Ndio maana nikaja na kauli mbiu hii kuwa MAMA ANATOSHA ,kwa maana kuwa anatosha kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili kama Rais wetu na Amiri Jeshi mkuu wetu.. Nimeona tusiseme au kuishia kusema tu NASIMAMA na Rais Samia au MAMA, Bali tuende mbele zaidi na kusema kuwa Rais Samia ANATOSHA.

Maana kuna mtu anaweza kusema NASIMAMA na Rais Samia au MAMA halafu ukigeuka nyuma unakuta hayupo au yupo Bize na mambo yake au amesimama na wewe lakini ana imani na mtu mwingine na hapo yupo tu kama picha .au mtu anaweza kusema NASIMAMA na mama halafu kumbe yeye amesimama hapo tu kuangalia kinachoendelea lakini hayupo mahali hapo kifikira na kimawazo na kiimani.lakinii mtu akisema Mama ANATOSHA, maana yake anatosha kweli kweli na haijalishi mtu yupo mahali hapo au yupo vijijini lakini imani yake inabaki kuwa Mama ANATOSHA na hakuna cha kumzuia wala wa kumzuia kuendelea na muhula wa pili kuwatumikia watanzania.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
IMG-20240315-WA0027.jpg
IMG-20240206-WA0025.jpg
IMG-20240116-WA0009.jpg
IMG-20240202-WA0010.jpg
IMG-20240309-WA0024.jpg
 
Urais ni taasis kubwa mno na nzito yenye kuogofya too sad mabarakala( chawa ) wanaidhalilisha sana kwa kumfanya rais kuonekana ni kama mtu anayependa sifa za kijinga na kutukuzwa ili atoe mkate kwa mabarakala ( chawa)
 
Fore sure,

:KasugaYeah: :KasugaYeah: mama ndio habari ya mjini, vijijini na vitongijini,

iwe ni shambani anazungumzwa Dr.samia, sokoni ni Dr.Samia, harusini ni Dr.Samia, vijiweni ni Dr.Samia, michezoni, Dr. Samia, kwenye maamdamano ni Dr. Samia, kwemye mikutano mathaalani ya BAWACHA anazungumzwa Dr. Samia ...

for sure every where ni Dr.Samia tu, kiongozi na kipenzi cha waTanzania :KasugaYeah: :KasugaYeah:
 
Kupe wa mama kwenye 1 na 2,,,mtaani hawamuelewi msilazimishe mambo
Rais Samia anakubarika Sana na Watanzania huku mitaani. Watu wanampenda mama mpaka wanatamani uchaguzi uwe kesho tu ili wampigie kura za ndio kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima.
 
Back
Top Bottom