Sisi tumewekeza sana kwenye siasa za maji takaAmazing..hawa jamaa wametuacha mbali sana sijui nchi zetu zitawezaje kufika kwenye tech kama hizi au hata kama upo mpango kwenda kwenye robotic manufacturing
Maeda?Huyu hapa Ikuo Maeda ndio General Manager wa Mazda Design team.
View attachment 2974773
Apewe maua yake kwa kuleta Kodo design (Soul of Motion).
Huenda watengenezaji wa Chinese trucks & buses wakatangulia kufikiria kuwekeza Afrika Mashariki na kati maana kwa sasa wameliteka sokoBYD, XIAOMI au kampuni yoyote ya magari ije pia iwekeze Tanzania aisee. Dah Xiaomi mbaya sana kwenye EV yaani najua kabisa Elon Musk kila akilala lazima aote gari za Xiaomi zikiwa zina mkimbiza 😂
Hatari sanaXpeng AeroHT wazindua Flying Car
It's officially. Wamesema litagharimu atleast $140,000 na utahitaji vibali special.
View attachment 2975213View attachment 2975214
Haya sio mapigo yetu ila wakina Bakherssa na Mo wanaweza daka vyuma ivo.
Kiwanda cha mabasi ya Mwendokasi kije huku TanzaniaHuenda watengenezaji wa Chinese trucks & buses wakatangulia kufikiria kuwekeza Afrika Mashariki na kati maana kwa sasa wameliteka soko
Ndiyo maana Marekani ana mpiga vita sana mchina. Yaani amesha shindwa kwa kila kitu mbele ya mchinaYaani hao BYD wanamtesa Tesla.
View attachment 2975196
Au ata East Africa aisee. Wakiuza kwa bei rafiki kitu gani kujaribu.
Sipati picha hili gari likitumika huku bongo na hawa bodaboda itakuaje!!!Volkswagen tena.
Wapenzi wa Volkswagen wametuletea Volkswagen ID.Concept ambayo ni Smart Car.
View attachment 2975180
Hii ni SUV flani, ambayo Volkswagen wamesema ina latest and most advanced Level 4 Automated driving.
PS: Automated Driving zina level kadhaa kuanzia level 1 hadi level 5. Hii Level 1 ni simple and lighter driving assistance mfano Cruise Control, Lane Keeping Assistant etc wakati Level 4 ni FSD (Full Self Driving) kwamba gari itafanya kila kitu kuanzia acceleration, braking, cornering, kusimama kwenye traffic lights, kupark, kusimama zebra, etc as long umeshaweka destination kwamb naenda Mbagala Rangi Tatu. Tuendelee na gari letu..
Hapa dereva ukiacha gari ijiendeshe, wewe na abiria wako wa mbele mnaweza geuka kabisa 180 degrees kupiga story na abiria wa nyuma. Sio kigeuza shingo, kugeuza seat kabisa.
View attachment 2975191
Ukiwa unaendesha hii chuma afu uka engage "Center Pilot" hapa AI inatake over inaanza kuendesha yenyewe chuma. Kwanza mkwara unaanza steering wheel ambayo inashape yetu pendwa ila mbaya Yoke style inazama na kubakisha dashboard plain, kama kwenye Sci-fi movies.
View attachment 2975183
Pia vioo vyote, cha mbele na vya pembeni, vina display information mbalimbali ambazo utaamua watu wa nje wazione au muzione nyie wa ndani tu.
Mfano, unaweza ukawa uko ndani unaendesha chuma afu unapita sehemu kuna mazingira mabaya, ukaamua kuweka display vioo vya pembeni vikawa vinaonesha wallpaper beach au kitu garden, ili passengers wafurahi.
Kioo cha mbele kina HUD augmented reality down to earth projection, nadhani hii tumeona kwenye Mercedes Benz EQS yaan HUD hii unakua unaona kabisa as if vitu vimewekwa kwa chini. Nashindwa kuelezea ila ngoja angalia hii picha kama itakusaidia.
View attachment 2975186
Na mwisho kuna hygiene mode, ambayo uta engage mfano umetoka safari afu ulikua na familia. Gari chafu kwa ndani. Basi mkishuka, uka enable gari itahakikisha ndani hakuna mtu afu itatoa UV light na antibacteria filters zitasafisha hewa ya ndani na kuna vacuum cleaner anaitwa Lupo ataanza kusafisha ndani kuondoa takataka ndogo ndogo.
View attachment 2975189
Ilikua moja ya presentation nzuri tungeweka link hapa ya video ila haina maana vitajaa vilink sana.
Hao ni Golden DragonKiwanda cha mabasi ya Mwendokasi kije huku Tanzania