LIVE Updates za Beijing Auto Show 2024 (25 April - 4 May)

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
19,548
51,570
Nipo Dar es Salaam, na kuna mvua + Mafuriko ila nafuatilia yanayoendelea uko China kwenye Beijing Auto Show ya mwaka 2024, ilioanza tar 25 April hadi 4 May.

Hii Beijing Auto Show kwa jina jingine inaitwa China Auto Show ndio show kubwa kulizo zote Duniani ya magari ambapo makampuni mbalimbali yanazindua nyuma vyao vya mwaka unaofuatia (au inayofuatia).

Maonesho aya yanafanyika kila baada ya miaka miwili. Kwahiyo, yaliopita yalikua 2022 na sasa tupo ya 2024.

Makampuni mbalimbali ya magari Duniani yanazindua magari na technology zao officially.

Toyota
Giant kutoka Japan kazindua gari mbili za umeme. Toyota bZ3X na bZ3C. Utatusamehe kwa majina ndio kaamua kuyaita ivo.

arenaev_002.jpg
arenaev_003.jpg

bZ3C ni crossover iliyotengenezwa kwa ushirikiano wa Toyota na Kampuni la Kichina linalofanya vizuri kwenye sekta ya magari ya umeme BYD.

Na huku gari la bZ3X lenyewe ni compact SUV ambalo Toyota wanasema "limetengenezwa kwaajili ya kulenga vijana wa generation Z kutoka China".
arenaev_004.jpg
arenaev_006.jpg

Magari yote mawili Toyota amesema yatakuja na Smart Drive Assistant System na yatakua na cockpit ya kisasa zaidi, sokoni yataingia mwaka huu 2024.
 
Mazda
Mkali wa hizi mambo Mazda nae kazindua chuma yake Mazda ZE6 ambayo ni gari ya umeme jamii ya Mazda 6 (Atenza). Hii itakuja na version mbili, pure umeme na hybrid.
240425b.jpg
mazda-ez-6.jpeg

Taarifa nyingi bado hazijawa official, ila juu juu wamesema EV itakua na range ya Kilometa 600.

Edit:
Mazda Arata
Mazda kazindua tena chuma nyingine (concept) ambayo ni small SUV itakua apo sokoni kuanzia 2025.
images (6).jpeg
 
Ji Yue 07 (kutoka kwa Jidu Auto)
Hii kampuni Jidu Auto unaweza ukawa hauijui, ila ipo uko China. Ikiundwa 2021 ikiwa ni muungano wa kibiashara wa makampuni mawili Geely (hii kampuni ya magari) na Baidu (hii kampuninya technology wana search engine kubwa kama Google uko China na wana online market kubwa kama Alibaba).

Sorry nawachosha. Ila hizi joint venture mnagawana majukumu. Mfano, kwenye hizi gari Geely yeye anatengeneza gari (sijui tuseme hardware) hafu Baidu anatengeneza software (ADAS (Advanced Driving Assistant System) na Connectivity kama Bluetooth na WiFi etc)

Jidu Auto wana magari mawili hadi sasa. La kwanza mwaka jana Ji Yue 01 ambayo ni full EV SUV ila mwaka huu wametuletea Ji Yue 07 ambayo ni Premium Sedan.

1-76.jpg

Kwa nje chuma ni ya moto. Ina muonekano mzuri, na ina cameras, radars na sensors za kutosha.

image-128.png

Kwa ndani kuna screen ya inch 35 yenye 6K resolution na ina chip (SoC) ya Qualcomm Snapdragon 8295 na steering ya kishua ya Yoke aka Halfmoon.

Jiyue kwenye presentation yao pia wamesema wameanza kushirikiana na NVIDIA kutengeneza smartcars zenye FSD (Full Self Driving) capabilities.

Hii gari imepata tuzo mbili, IF Design Award na Red Dot Design Award.
 
BYD
Wakali wa EV China kwa sasa BYD (Build Your Dreams), nao wamezindua vyuma viwili leo kwenye maonesho.

Ocean M ambayo ni Hatchback. Itauzwa around $27,000 kuanzia mwaka huu.
BYD-new-EVs.jpeg

BYD-new-EVs-3.jpeg

Denza Z9 GT ni sedan ambayo itacompete kwenye soko na Porsche Panamera. Hii gari ni powerful ina 1000hp.
BYD-new-EVs-5.jpeg

BYD ni watabe wa kutengeneza gari kwa bei rafiki, mfano wametoa mwaka huu Seagull kwa $10,000/= tu.

Hii haina maana kwamba Ocean M na Denza watauzaa cheap, kwasababu pia wana magari ya bei kubwa sana kuzidi $150,000 mfano super cars U8 na U9.
 
Ila madza kwenye design ni balaa Sana nimeona hiyo Toyota nao ni bonge moja chuma yamaana Sana.
BMW safari hii kachemka kinoma na hiyo gari yake ya i4 min cooper.

Juzi nilikuwa nasoma mtandao wa Quora digest watumiaji wa Tesla wanalalamika Sana magari Yana shida nyingi hii inapelekea china kuteka soko la Ev's duniani maana jamaa Wanatengeneza vyuma vya maana na bei zao ni kitonga

angalia SUVs za kampuni ya kichina ya HAVAL haya magari yanagombewa Huko Australia kama pipi , nahisi ndani ya miaka hii miwili yataingia bongo nahisi hapa itakuwa mwisho wa magari ya kijapan kama ilivyo mabus ya Scania dhidi ya YUTONG
 
Volkswagen Tayron
Volkswagen wametuletea SUV yenye 2.0L Turbo engine kwenye menu. Ila kuna uwezekano baadhi ya nchi wakapata 1.5L plug-in hybrid na 2.0L diesel engine.
1-42.jpg

Kwa ndani ina share muonekano na Volkswagen Tiguan mpya.
4-29.jpg
3-37.jpg

Chuma ni kali, kwenye presentation yao wamejisifia sana 360 degrees camera, wireless phone charging, Heads up Display, Dual zone climate na ADAS (ambavyo ni vitu vya kawaida kwa magari ya sasa).
 
Hivyo ndivyo inavyotakiwa ushindani muhimu sana unachangamsha industry sasa BMW lazima ajifunze kuwa watu wapo serious na kazi japo kwa performance anaweza kuwa kawapiga gap ila muonekano akajipange tena
 
Ila madza kwenye design ni balaa Sana nimeona hiyo Toyota nao ni bonge moja chuma yamaana Sana.
BMW safari hii kachemka kinoma na hiyo gari yake ya i4 min cooper.

Juzi nilikuwa nasoma mtandao wa Quora digest watumiaji wa Tesla wanalalamika Sana magari Yana shida nyingi hii inapelekea china kuteka soko la Ev's duniani maana jamaa Wanatengeneza vyuma vya maana na bei zao ni kitonga

angalia SUVs za kampuni ya kichina ya HAVAL haya magari yanagombewa Huko Australia kama pipi , nahisi ndani ya miaka hii miwili yataingia bongo nahisi hapa itakuwa mwisho wa magari ya kijapan kama ilivyo mabus ya Scania dhidi ya YUTONG
Huyu hapa Ikuo Maeda ndio General Manager wa Mazda Design team.
Ikuo-Maeda-2-lg.jpg

Apewe maua yake kwa kuleta Kodo design (Soul of Motion).
 
Ila madza kwenye design ni balaa Sana nimeona hiyo Toyota nao ni bonge moja chuma yamaana Sana.
BMW safari hii kachemka kinoma na hiyo gari yake ya i4 min cooper.

Juzi nilikuwa nasoma mtandao wa Quora digest watumiaji wa Tesla wanalalamika Sana magari Yana shida nyingi hii inapelekea china kuteka soko la Ev's duniani maana jamaa Wanatengeneza vyuma vya maana na bei zao ni kitonga

angalia SUVs za kampuni ya kichina ya HAVAL haya magari yanagombewa Huko Australia kama pipi , nahisi ndani ya miaka hii miwili yataingia bongo nahisi hapa itakuwa mwisho wa magari ya kijapan kama ilivyo mabus ya Scania dhidi ya YUTONG
Yeah kwa Toyota umenena, kaingia vizuri sana.

Tesla anakumbwa na matatizo mengi sana kwa sasa. Especially build quality.

Hii issue ya Monopoly inamtesa sana, yaani imefika kipindi serikali ya US inataka izuie EV za China zisiende kwenye soko lao.
 
Ni nzuri sana. Mapinduzi yanaendelea katika utengenezaji wa magari serikali ya ccm ione aibu itutengenezee Barabara nzuri za kupitisha hizo ndinga maana bandarini wapo more active kuchukua kodi.

Naumia sana gari ikiwa chini kwa Barabara za bongo ni full stress..
Acha, unakutana na matuta ova shamba la viazi. Bado barabara mbovu kuna sehemu haupeleki.

Pia, wangetekeleza ile kauli ya magari ya umeme yaje na free kodi.

Hii iendane na sera ya bwawa la Nyerere.
 
Volkswagen Tayron
Volkswagen wametuletea SUV yenye 2.0L Turbo engine kwenye menu. Ila kuna uwezekano baadhi ya nchi wakapata 1.5L plug-in hybrid na 2.0L diesel engine.
View attachment 2974767
Kwa ndani ina share muonekano na Volkswagen Tiguan mpya.
View attachment 2974768View attachment 2974769
Chuma ni kali, kwenye presentation yao wamejisifia sana 360 degrees camera, wireless phone charging, Heads up Display, Dual zone climate na ADAS (ambavyo ni vitu vya kawaida kwa magari ya sasa).
Chuma hichi hapa.

Bei inalala ngapi Mkuu?
 
Yeah kwa Toyota umenena, kaingia vizuri sana.

Tesla anakumbwa na matatizo mengi sana kwa sasa. Especially build quality.

Hii issue ya Monopoly inamtesa sana, yaani imefika kipindi serikali ya US inataka izuie EV za China zisiende kwenye soko lao.
Marekani ni mafala Sana yaani hawa wajinga wanataka kilakitu wanachofanya dunia ipokee kama kilivyo bila challenge angalia mfano wa simu zao za Apple hazina lolote la maana Ila wanataka dunia tununue huku wakiuza bei ya juu .
Angalia mfano wa App ya tik tok inavyowatesa wamarekani wanajua baada ya simu kadhaa mitandao Yao ya Facebook na Instagram hawatakuwa na soko .

Huawei ndiyo simu yenye camera Kali Ila Leo hii imepigwa marufuku USA
 
Back
Top Bottom