Kwa wale Wapenzi wa Wenzangu wa Muziki wa Congo DR ( Bana Bandeko Nangai ) hivi Bendi ya Wenge Musica BCBG isingevunjika leo tungekuwa na huu Ubunifu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,784
109,452
Kwa Maoni yangu GENTAMYCINE ( Rais wa Wapenzi wote wa Bendi ya Wenge Musica BCBG JamiiForums nzima ) japo niliumia sana kwa Bendi hii Kuvunjika na kila Mtu Kuunda Wenge Musica yake yaani JB Mpiana akibakia na Wenge BCBG, Werrason akibakia na Wenge Musica Maison Mere, Adolphe Dominguez akibakia akibakia na Wenge Tonya Tonya na BlaIse Bula ( Injinia wa Ndege ) kubakia na Wenge Musica Ponderation ila kuna niliyoyagundua ambayo ningependa Kushea nanyi na pia nanyi mseme yenu ili mradi tu Mjadala unoge na Sisi Wadau wa Muziki wa Congo DR hasa kwa Wapenzi wa Wenge Musica BCBG tuweze Kuelimika zaidi.

Hivi Wadau wangu bila ya hii Bendi Kuvunjika kule leo hii tungeona Ubunifu mkubwa wa Wanamuziki wa Congo DR? Je, Vipaji vipya vingeonekana kama ambavyo vinaonekana sasa baada ya kila Mtu Kuunda Kundi lake? Kwa mfano mnadhani Mghani / Rapa ( Kifaransa wanaitwa Animateur na Kilingala wanaitwa Atalakus) Hodari na Mahiri GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE angejulikana kama Wenge Musica BCBG iliyokuwa na Marapa ( Animateurs ) Wawili tu Wakubwa kama Roberto Wunda Enkokota na Mwalimu wa Maapa wote wa sasa Congo DR nzima Tutu Calugi Yombo Lumbu?

Je, mnadhani bila ya Kuvunjika kwa Bendi ya Wenge Musica BCBG leo hii Vijana wengi Congo DR wangepata Ajira zao Kubwa katika Bendi Kubwa Nne zenye Uzao wa Wenge BCBG na hata Kuajiriwa katika Bendi zingine Kubwa kama za akina Koffi Olomide, Extra Musica, Felix Wazekwa na Zaiko Langa Langa?

Kwangu Mimi naona huku Kuvunjika kwa hii Bendi na hata kwa Wanamuziki wengine Maarufu wa Bendi Kubwa na Wasanii Wakubwa kuamua Kujitoa na Kuanzisha Bendi zao kumesaidia Kutatua tatizo la Ajira lakini pia limeweza Kukuza Mapato yao na hata Uchumi kwani 97% ya Wanamuziki wa Bendi za Congo DR wao muda mwingi wanakuwa Ulaya, Marekani na Kwingineko Barani Afrika na Duniani wakipiga Muziki ( kwa Ziara ) hivyo kuwasaidia kuwapatia Vipato Vikubwa mno.

Taarifa ikufikie kuwa hakuna Mwanamuziki anayeimba na Bendi zozote Kubwa Congo DR au zenye Wasanii wakubwa ambaye ni Masikini. Kwa mfano Mshahara wa chini kabisa kwa hawa Wadada Wanenguaji wa Bendi Kubwa za Congo DR ni Shilingi Milioni Nne za Kitanzania huku wale Waimbaji wa hizi Bendi wengi Wao Mishahaa yao inaanzia Shilingi Milioni 6 hadi Milioni 8 za Kitanzania na ndiyo maana Koffi Olomide alivyokuwa akifanyiwa Interview na Mwanahabari Mmoja Mzungu huko Canada aliyemuuliza kwanini Wanenguaji wake wanapenda Kucheza wakiwa karibia Nusu Uchi Koffi Olomide wala hakumchelewesha kama ambavyo hata Mimi GENTAMYCINE huwa siwacheleweshagi Wajinga Wajnga na Wapumbavu hapa JamiiForums wakiingia katika 18 zangu ambapo alimjibu kuwa hawa Wanenguaji unaowaona hapa Mishahara yao ya kila Mwezi inaweza kuwa ndiyo Mshahara wako wa mwaka mzima katika hii Media uliyopo na baada ya hapo Yule Mwandishi akawa Mpole na kuuliza Maswali yenye Tija zaidi huku akiwa ameshika pia Adabu zake.

Hivyo basi tusiogope kuwa na Chetu hata kama tulikuwa tunapata kutoka katika Chetu Kimoja ili Wengine wapate Okay?

ANGALIZO

Kama unajua HUMPENDI GENTAMYCINE na Mada ( Threads ) zake hapa JamiiForums HUZIPENDI tafadhali nakushauri KIUSTAARABU tu acha KUZIFUNGUA, KUZISOMA na hata KUZICHANGIA badala yake nenda Kawasome tu wale MEMBERS wako UNAOWAKUBALI zaidi hapa na Mimi niachie wale MEMBERS wangu WANAONIELEWA KUTWA na hawana USWAHILI, UPUUZI, USHAMBA na UPUMBAVU wa KUTUKUKA kama ulionao.

Ukikaidi hili ANGALIZO langu usije KUNILAUMU kwa MAJIBU YANGU UMIZA ambayo NITAKUPOROMOSHEA pale tu UTAKAPOSHOBOKA nami kwa KUWASHWAWASHWA Kwako nami kama MNYAMA JIKE anayetaka KUPANDWA ( KUINGILIWA ) na MNYAMA DUME a.k.a GENTAMYCINE.

Nimemaliza.
 
Nje ya maada kuna mwanadada anaimba Rhumba kanaitwa Cindy Le Couer kana sauti fulani tulivu balaa.

Napenda nyimbo zake mbili
Mon Bonheur na Je Te jure.
 
Nje ya maada kuna wadada kanaimba Rhumba kanaitwa Cindy Le Couer kana sauti fulani tulivu balaa.

Napenda nyimbo zake mbili
Mon Bonheur na Je Te jure.
Sijaelewa hata umeandika nini au unataka nini hebu irejee kuiangalia upya hii Post yako nadhani inahitaji Marekebisho.
 
mheshimiwa Blaise Bula yule ni mhandisi kabisa kwa utaaluma?
Ndiyo Mkuu Jamaa ni Msomi wa juu kabisa wa Uinjinia na hasa ule wa katika Ndege. Ni sawa na Mwanamuziki Mwingine wa Wenge BCBG yake JB Mpiana aitwae Jules Kibens Molongeshi huyu alikuwa ni Mwalimu wa Lugha Chuo Kikuu Congo DR ila kaacha hiyo Kazi kajikita katika Muziki.

Na hata Nyimbo nyingi za sasa za Wenge BCBG yake JB Mpiana kile Kifaransa kilichonyooka unachokisikia Kikitamkwa katika maneno ya Wimbo mara nyingi huyu Mtaalam wa Lugha Mwalimu Jules Kibens Molongeshi ndiyo huwa anaandika na hata Kuhariri.

Na sasa pia ndiyo Kiongozi wa Waimbaji wa Bendi huku Mpiga Drums maaruu wa hiyo Bendi atwae Seguen Mignon Bongongo akiwa ndiyo Mkurugenzi wa Bendi na JB Mpiana Mwenyewe ndiyo akiwa Rais na Mmiliki wa Bendi ya Wenge BCBG ( Mashine ya Muziki Congo DR ) kama wanavyojiita na hawa ni Mashine ya Muziki kweli kweli kwani ukiona hadi GENTAMYCINE nawakubali jua wako vizuri 100%.
 
Bro genta
Nisaidie majina ya rappers waliokiwasha kwenye ngoma ya force de frappe
Mimi ni mwana Wenge BCBG hivyo niulize mambo ya Wenge tu kwani hawa ulioniulizia hapa Kinafiki ( kama Kunipima ) wakati unajua hata tu ukienda Google ukiwaulizia unawapata ni wa kutoka Bendi ya Koffi Olomide ya Quarter Latin. Marapa pekee wa Koffi Olomide niliokuwa nawajua na niliwakubali ni akina Mboshi Bola, Parabolique, Kerozene ambaye Kaka yake nae ni yule aliyekuwa Rapa wa Koffi Olomide zamani na akaenda kwa Werasson anaitwa Bill Clinton na hawa wa sasa ( hivi karibuni ) akina Aristotle na huyu Kirikuu.
 
Ndiyo Mkuu Jamaa ni Msomi wa juu kabisa wa Uinjinia na hasa ule wa katika Ndege. Ni sawa na Mwanamuziki Mwingine wa Wenge BCBG yake JB Mpiana aitwae Jules Kibens Molongeshi huyu alikuwa ni Mwalimu wa Lugha Chuo Kikuu Congo DR ila kaacha hiyo Kazi kajikita katika Muziki.

Na hata Nyimbo nyingi za sasa za Wenge BCBG yake JB Mpiana kile Kifaransa kilichonyooka unachokisikia Kikitamkwa katika maneno ya Wimbo mara nyingi huyu Mtaalam wa Lugha Mwalimu Jules Kibens Molongeshi ndiyo huwa anaandika na hata Kuhariri.

Na sasa pia ndiyo Kiongozi wa Waimbaji wa Bendi huku Mpiga Drums maaruu wa hiyo Bendi atwae Seguen Mignon Bongongo akiwa ndiyo Mkurugenzi wa Bendi na JB Mpiana Mwenyewe ndiyo akiwa Rais na Mmiliki wa Bendi ya Wenge BCBG ( Mashine ya Muziki Congo DR ) kama wanavyojiita na hawa ni Mashine ya Muziki kweli kweli kwani ukiona hadi GENTAMYCINE nawakubali jua wako vizuri 100%.
Nimeamini sasa ndio maana jamaa amekaa kisomisomi.
Kwa wakongo sio ajabu akaacha taaluma yake kwa ajili ya muziki kama ilivyo Kofi Olomide mwenye Masters ya Mathematics.
 
Nimeamini sasa ndio maana jamaa amekaa kisomisomi.
Kwa wakongo sio ajabu akaacha taaluma yake kwa ajili ya muziki kama ilivyo Kofi Olomide mwenye Masters ya Mathematics.
Wanamuziki wengi sana wa Congo DR wamesoma, ila Kwao Muziki ni sehemu inayolipa haraka na kwakuwa Kiasili Wakongo wanapenda sana Exposure ( hasa Kujichanganya nchi mbalimbali ) Kwao kwa Kupitia Muziki ni rahisi kwenda Ulaya ama kwa Kutembea au hata Kuzamia kabisa.
 
Demu wake na koffie of course kapo vizuri sauti yake kali
Katika Birthday yake ya miaka kama Mitatu Minne hivi Koffi Olomide ( Mumewe ) alimzawadia Baba Mkwe Gari New Model aina ya Range Rover lenye Thamani Kubwa sana. Koffi Olomide alishakuwa na Wanawake wengi na ni Mpenda chini kama GENTAMYCINE ila unaambiwa hakuna Mwanamke aliyempenda na anayempenda kama huyu wa sasa Cindy.

Hata hivyo moja ya sababu Kubwa ya kuwa na huyu Cindy na Kumpenda huku akimghaamia kila Kitu ni kutokana na Kuambiwa na Mganga wake Mkubwa wa Kienyeji ambaye pia anatumiwa na Fally Ipupa na ndiyo alikuwa pia akitumiwa na Papa Wemba, Madilu System na Zaiko Langa Langa pamoja na Viongozi ( Wakubwa ) wengi barani Afrika kuwa amuoe na ampende mno kwani Cindy ana Nyota nae Kali na atafika mbali nae Kimuziki na Kimaisha.

Siku nyingine Mizimu yangu ya Kizanaki na Kiyao ikitulia nitakuja hapa na Exclusive ya Ndumba za Wanamuziki wa huko.
 
Sio mchezo!

Halafu nimeambiwa wanawake wa kizanaki wazuri sana na watamu ila majeuri. Kuna ukweli?
 
Uzi wa popoma bila matusi haujakamilika sasa ndio umekamilika.
Post yako #8 kuwa Uzi wangu Umedoda umeitoa au unaiacha ili Uaibike sasa na uonekane Mpumbavu kama ulivyo?

Mimi ndiyo GENTAMYCINE The King na mtatumia Nguvu Kubwa ya Kunishusha Umaarufu hapa JF ila hamtoniweza kamwe. Mlichosahau ni kwamba GENTAMYCINE nimebarikiwa Nguvu Maalum ya Kimvuto na Mwenyezi Mungu na ndiyo maana hata nikisema tu nianzishe Uzi wa Kipuuzi bado utapata Wachangiaji.

Ulidhani Signature yangu isemayo..." Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer" imekosewa?
 
Back
Top Bottom