Elimu ya bure kwa mnaojiuliza Bendi za Congo DR zinapata wapi pesa za kujiendesha pamoja na wamiliki wake kuwa matajiri

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,851
109,552
1. Hakuna Msaniii yoyote mkubwa wa Congo DR kuanzia kwa JB Mpiana, Koffi Olomide, Werrason, Felix Wazekwa, Roga Roga na Bendi yake ya Extra Musica, Fally Ipupa na Ferre Gola utamuita aje nchini Kwako kufanya Show bila ya Kwanza kumuingizia katika Akaunti yake kuanzia Shilingi Milioni 400 hadi 500 za Kitanzania.

2. Malipo yao pia hutegemea na nchi ambayo wanaenda Kufanya Shows zao. Kwa mfano wakiwa wanaenda nchi za Ulaya na hata Marekani huko ambako pia Waafrika wanaopenda Nyimbo zao/Miziki yao Gharama zao ambazo huwa wanataka wapewe Kwanza ndiyo waelekee huko huanzia kati ya Shilingi Milioni 800 za Kitanzania hadi Shilingi Bilioni Moja.

3. Mwisho kabisa Chanzo chao Kikubwa cha Mapato ni Ubunifu wao wa Kutoza Pesa kwa kila Mtu ambaye anafagiliwa katika Wimbo mpya na wa Album mpya. Kiasili Wakongo ni Watu ambao wanapenda Sifa, Kujulikana na Ufahari kiasi kwamba hata Watani zangu Wahaya na Ndugu zangu Wajita kutoka Mkoa wa Mara wanasubiri (namaanisha hawafui Dafu) Kwao.

Zifuatazo ni Gharama (Tozo) kwa Mtu yoyote (hata Wewe Mtanzania Mwenzangu) ukitaka ni ruhksa za Kuchajiwa kama tu utataka Jina lako au Biashara yako litajwe/itajwe katika Wimbo mpya wa hawa Wasanii Tajwa hapa.

- Ukitaka Jina lako litajwe mwanzoni mwa Wimbo utalipa Dola za Kimarekani 100000

- Jina lako likitajwa katikati ya Wimbo utalipa Dola za Kimarekani 7500

- Jina lako likitajwa pale ambapo Sebene linaanza utalipa Dola za Kimarekani 5000

- Jina lako likitajwa pale ambapo Sebene sasa limeshakole utalipa Dola za Kimarekani 3000

- Jina lako likitajwa pale Muziki ukiwa unaenda Kuisha (na huku ndiko Wengi hupataka) basi utalipa Dola za Kimarekani 2000

Na hakuna Nyimbo zozote za Wasanii hawa Tajwa (hasa zile Mpya) mnazozisikia hakuna Majina yasiyopungua 50 hadi 70 huyasikii yakitajwa humo hivyo.

Wewe kaa chini sasa hapo ulipo na upige Hesabu ni kiasi gani cha Pesa hawa Wanamuziki huwa wanakiingiza na ambacho ndicho huwa kinawapa Jeuri ya Kuvaa Nguo za Thamani Kubwa, Kuendesha Magari ya Kifahari, kuwa na Makazi Ulaya (hasa Ufaransa na Ubelgiji) na kuwa na Mahekalu huko Kwao Congo DR hasa katika Mji ambao Masikini hawezi Kuuishi wa Kinshasa kutokana na kuwa ni Mji wenye Gharama kubwa.

Mishahara ya Waimbaji wao wote ambao huwa mnawaona Stejini (hasi wale Marapa ambao Kwao huitwa Atalakus na Kifaransa wanaitwa Animateurs) huwa ni Shilingi Milioni Saba za Kitanzania huku wale Wadada Wanaenguaji ambao huwa mnawaona na baadhi yenu Kuwaona kama vile huwa Wanajidhalilisha huwa wanalipwa kila Mmoja Mshahara wa Shilingi Milioni Tano za Kitanzania kwa kila Mwezi.

Mwisho kabisa kinachoendelea kuwapa Jeuri hawa Wasanii tajwa na Bendi zao ni Udhamini mbalimbali ambao wanaupata kutoka katika Makampuni makubwa ya Vinywaji kama Primus na ile ya Simu ya MTN bila kusahau na Kampuni zingine Kubwa za Mavazi na Mitindo zilizoko Ulaya (Marekani, Ufaransa na Ubelgiji)

Haya na Mimi GENTAMYCINE bado najichanganga hapa tararibu ili angalau nipate tu Dola zangu 2000 ili nimtafute JB Mpiana na Bendi yake ya Wenge Musica BCBG wanitaje mwishoni mwa Wimbo kwa Majina yangu halisi ya Kalemera Rwigyema Mazimpaka Kadogoo Kisungura ambayo hata Marafiki zangu wakubwa hapa akina adriz, Bujibuji Simba Nyamaume na King Kong III wanayajua vyema ili nikitajwa nae nije niwakoge (niwatambie) hapa hadi mkome.
 
Hiyo namba tatu naamini hata bendi zetu zenye asili ya Congo kina FM Academia na wengine waliiga toka kwa bendi za Congo.

Nyimbo nyingi za Koffi Olomide kawataja kina George Weah, Mutombo Dikembe [mcongo aliyekuwa anakipiga NBA].

Ndio maana ulipotaja kiasi cha pesa ambazo hao jamaa hutoa ili majina yao yatajwe nimekuelewa zaidi, wale wazito pesa walikuwa nazo.
 
Huwezi amini huyo pamoja na Kutajwa Kwake kote huko na Bendi nyingi za hapa Tanzania bado hizo Bendi hazikufaidika nae Kimapato kama Bendi hizo za hao Wenzao wa Congo DR ambao nimewazungumzia hapa katika Maelezo yangu ya Kiufafanuzi zaidi.
😂😂😂😂
Nakumbuka miaka ya 1999 Twanga Pepeta ni ya moto sana ilikuwa inamtaja sana Uncle wangu ambaye alikuwa ni mfanyabiashara wa madini kule Tunduru mkoani Ruvuma na sijui kama alikuwa anawapa pesa au alikuwa anawanunulia pombe tu.
 
1. Hakuna Msaniii yoyote mkubwa wa Congo DR kuanzia kwa JB Mpiana, Koffi Olomide, Werrason, Felix Wazekwa, Roga Roga na Bendi yake ya Extra Musica, Fally Ipupa na Ferre Gola utamuita aje nchini Kwako kufanya Show bila ya Kwanza kumuingizia katika Akaunti yake kuanzia Shilingi Milioni 400 hadi 500 za Kitanzania.

2. Malipo yao pia hutegemea na nchi ambayo wanaenda Kufanya Shows zao. Kwa mfano wakiwa wanaenda nchi za Ulaya na hata Marekani huko ambako pia Waafrika wanaopenda Nyimbo zao/Miziki yao Gharama zao ambazo huwa wanataka wapewe Kwanza ndiyo waelekee huko huanzia kati ya Shilingi Milioni 800 za Kitanzania hadi Shilingi Bilioni Moja.

3. Mwisho kabisa Chanzo chao Kikubwa cha Mapato ni Ubunifu wao wa Kutoza Pesa kwa kila Mtu ambaye anafagiliwa katika Wimbo mpya na wa Album mpya. Kiasili Wakongo ni Watu ambao wanapenda Sifa, Kujulikana na Ufahari kiasi kwamba hata Watani zangu Wahaya na Ndugu zangu Wajita kutoka Mkoa wa Mara wanasubiri (namaanisha hawafui Dafu) Kwao.

Zifuatazo ni Gharama (Tozo) kwa Mtu yoyote (hata Wewe Mtanzania Mwenzangu) ukitaka ni ruhksa za Kuchajiwa kama tu utataka Jina lako au Biashara yako litajwe/itajwe katika Wimbo mpya wa hawa Wasanii Tajwa hapa.

- Ukitaka Jina lako litajwe mwanzoni mwa Wimbo utalipa Dola za Kimarekani 100000

- Jina lako likitajwa katikati ya Wimbo utalipa Dola za Kimarekani 7500

- Jina lako likitajwa pale ambapo Sebene linaanza utalipa Dola za Kimarekani 5000

- Jina lako likitajwa pale ambapo Sebene sasa limeshakole utalipa Dola za Kimarekani 3000

- Jina lako likitajwa pale Muziki ukiwa unaenda Kuisha (na huku ndiko Wengi hupataka) basi utalipa Dola za Kimarekani 2000

Na hakuna Nyimbo zozote za Wasanii hawa Tajwa (hasa zile Mpya) mnazozisikia hakuna Majina yasiyopungua 50 hadi 70 huyasikii yakitajwa humo hivyo.

Wewe kaa chini sasa hapo ulipo na upige Hesabu ni kiasi gani cha Pesa hawa Wanamuziki huwa wanakiingiza na ambacho ndicho huwa kinawapa Jeuri ya Kuvaa Nguo za Thamani Kubwa, Kuendesha Magari ya Kifahari, kuwa na Makazi Ulaya (hasa Ufaransa na Ubelgiji) na kuwa na Mahekalu huko Kwao Congo DR hasa katika Mji ambao Masikini hawezi Kuuishi wa Kinshasa kutokana na kuwa ni Mji wenye Gharama kubwa.

Mishahara ya Waimbaji wao wote ambao huwa mnawaona Stejini (hasi wale Marapa ambao Kwao huitwa Atalakus na Kifaransa wanaitwa Animateurs) huwa ni Shilingi Milioni Saba za Kitanzania huku wale Wadada Wanaenguaji ambao huwa mnawaona na baadhi yenu Kuwaona kama vile huwa Wanajidhalilisha huwa wanalipwa kila Mmoja Mshahara wa Shilingi Milioni Tano za Kitanzania kwa kila Mwezi.

Mwisho kabisa kinachoendelea kuwapa Jeuri hawa Wasanii tajwa na Bendi zao ni Udhamini mbalimbali ambao wanaupata kutoka katika Makampuni makubwa ya Vinywaji kama Primus na ile ya Simu ya MTN bila kusahau na Kampuni zingine Kubwa za Mavazi na Mitindo zilizoko Ulaya (Marekani, Ufaransa na Ubelgiji)

Haya na Mimi GENTAMYCINE bado najichanganga hapa tararibu ili angalau nipate tu Dola zangu 2000 ili nimtafute JB Mpiana na Bendi yake ya Wenge Musica BCBG wanitaje mwishoni mwa Wimbo kwa Majina yangu halisi ya Kalemera Rwigyema Mazimpaka Kadogoo Kisungura ambayo hata Marafiki zangu wakubwa hapa akina adriz, Bujibuji Simba Nyamaume na King Kong III wanayajua vyema ili nikitajwa nae nije niwakoge (niwatambie) hapa hadi mkome.
Kumbe
 
Kama ni hivyo ule wimbo wa jb mpiana ( No comment shenghen ) utakuwa umeshika rekodi ya kupiga pesa kwa wingi kuliko wimbo wowote,maana mwanzo mpaka mwisho anataja majina tu.
Achilia mbali tu Album ile Wenge Musica BCBG 4 X 4 Kupiga sana Hela ila pia Bendi nzima ilikuwa chini ya Udhamini wa Mafia wa wakati huo ambaye pia ni Mtoto wa Hayati Rais wa Zaire ( sasa Congo DR ) Mobutu Seseseko aitwae Jose Kongolo Mibeko la Lalwaa jina la Utani alikuwa akiitwa Saadam Hussein. Kipindi hiko Bendi ya Wenge BCBG na ya Quarter Latin yake Koffi Olomide zilikuwa chini ya Udhamini mkubwa wa Serikali kwakuwa huyu Mtoto wa Mobutu Jose Kongolo alikuwa ni Mtu wa Kujichanganya nao na aliwabeba sana kwa Fedha alizokuwa Akiiba kwa Mgongo wa Hayati Baba yake na pia kwa Dhahabu na Almasi alizokuwa Akiiba huko.

Ukisikiliza Albums zote za Wenge Musica BCBG na za Quarter Latin lazima tu utasikia akina JB Mpiana na Koffi Olomide wakimpaisha kwa kusema Jose Kongolo Sadame Missele wakimaanisha Jose Kongolo Sadam wa Makombora. Ikumbukwe pia kuwa Jose Kongolo alikuwa ni Mwanajeshi mkubwa tu na Mpenda Vita ambaye alishiriki sana Kuua Mwenyewe ( Yeye kama Yeye ) wale Wapinzani wa Hayati Baba yake japo hata Yeye pia alifariki kwa Kujiua ndani ya Boti ya Kijeshi aliyoitumia Kulikimbia Jeshi la Hayati Laurent Desire Kabila baada ya kuambiwa limeshaichukua rasmi Congo DR kwa msaada wa karibu na Wanajeshi wa Uganda, Rwanda na wana Usalama kadhaa wa Tanzania ambao Kimaadili nawahifadhi.

Dada yake Jose Kongolo aitwae Ngawali ambaye wengi wenu mlimjua kwakuwa ndiyo alikuwa akipanda Ndege aina ya Jet ya Baba yake kutoka Kinshasa asubuhi kwenda Darasani Kusoma nchini Ufaransa katika Jiji la Paris kwa Kufuru Kubwa ya Hayati Baba yao sasa ni Baamedi katika Hoteli moja Kubwa na maarufu huku nchini Ufaransa huku akiwa na Maisha magumu mno tofauti alivyokuwa awali akilalia katika Chumba chenye Madini ya Almasi tupu.
 
Sawa ikiwa lengo la binti yake Kuku Ngbendu wa Zabanga na familia yake lilikuwa ni kufanya kufuru tu.

Hata hivyo, katika uhalisia, mhusika alikuwa hapati faida yoyote kitaaluma ndo mana akaishia hapo Bar. Aidha, safari kutoka Kinshasa au Gbadolite huchukua masaa zaidi ya Sita.

Wakati mwingine tumwachie Abunuwas na hekaya zake kwa kuwa uhalisia haupo.
 
Back
Top Bottom