Kama una mpenzi ambaye yupo mbali yataka moyo sana

Mapenzi ya mbali ili yaende na yasikuvurugwe lazima ujizime data ujifanye ujui chochote. Ukipiga usipopokelewa au ikikatwa unatulia kama hakijatokea kitu vile na baadae ukiuliza ukajibiwa kubali tu majibu bila kujali ni uongo au n kweli.
 
Ni sehemu ndogo sana ya wapenzi wanaoishi mbalimbali ambao hudumu kwenye uhusiano wao kwa muda mrefu.

Hiki kinaonekana kuwa ni kitendawili kigumu sana kwa wapenzi wengi kuvumiliana kwenye uhusiano bila kusalitiana.

Ninapozungumzia umbali ninamaanisha wilaya na wilaya, wilaya na mkoa au mkoa na mkoa au nchi na nchi au bara na bara.

Ninaamini miongoni mwetu ama tumeshuhudia au kusikia au kuona au kuadithiwa kuwa kuna mwanaume au mwanamke ambaye alikuwa na mpenzi, mara mpenzi wake akapata nafasi ya kwenda kusoma mkoa mwingine au nchi nyingine, lakini mwisho wa siku ukasikia wapenzi wale wameachana baada ya mmoja kupata mpenzi mwingine huko aliko.

Inawezekana mpenzi wako alihamishwa kikazi nje ya wilaya uliyopo, lakini mwisho wa siku ukabaini kuwa mwenzio amepata mtu mwingine na mapenzi kwako yameanza kupungua au yamepungua kama siyo kwisha kabisa.

Kwanza kabisa ili udumu na mpenzi wako kuwa na ...

UAMINIFU
Kutokuwa na uaminifu miongoni mwenu, kama wapenzi mtakuwa ni waaminifu katika uhusiano wenu, basi kila unapoingiwa na pepo wa usaliti unakumbuka uzuri wa mpenzi wako, basi unaacha na kujizuia kisha unakuwa umemshinda pepo huyo.
Hili suala hata Equation x unaelewa

UZALENDO
Kutokuwa mzalendo kwa mpenzi wako. Jaribu kumpenda kwa kuwa ndiye uliyemchagua kuwa naye, kila siku Tanzania inasema watumishi wake wawe wazalendo, siyo wao tu hata mapenzi yanahitaji uzalendo wa hali ya juu. Uzalendo wa kupenda kitu chako, kumpenda mpenzi wako, mkeo, mumeo au mchumba wako.mkuu Analyse Lazima ujivunie, ujisifie kuwa naye kisha mthamini.

SUBIRA
Wapenzi kutokuwa na subira au uvumilivu; Hili nalo huchangia kwa kiasi kikubwa mapenzi ya mbali kuvunjika. Kama ilivyo subira ya kila mtu kuamini kuwa ipo siku ataondoka kwenye shida na ugumu wa maisha alio nao, basi Mzee wa kupambania amini na kuwa na subira au uvumilivu kwa mpenzi wako ili mfikie ndoto zenu.

MAZINGIRA
Jiepushe sana na mazingira ambayo yanaonekana kabisa yanaweza kukusababisha ukaingia kwenye uhusiano usio rasmi tena, pengine kwa mtu ambaye huna ndoto naye. Tatizo la kujiingiza kwenye uhusiano kwa sababu za kimazingira linaweza kukufanya ukajikuta umezama kwenye mahaba na mtu ambaye hana mapenzi na wewe na mwisho wa siku ukajikuta unaumia sana. Ukabaki kulaumu watu kama dronedrake


MAWASILIANO
Kutokuwa na mawasiliano ya mara kwa mara nayo huchangia sana kuvunjika kwa mapenzi ya mbali au kupoteza ladha, lakini kama mtu anakupenda kwa dhati, anakupenda tu, anaweza kukupigia simu na kukutumia SMS kibao, lakini akawa bado ni tatizo. Chunga sana mzee wa miongozo Smart911



TAMAA
Kama utaishi kwa kutamani vitu usivyokuwa na uwezo navyo ni dhahiri utajikuta unamsaliti mpenzi wako kwa kuwa tu uko mbali na unaona hawezi kukubana wala kukufuatilia. Ingawa ningekushauri ufanye kitu kwa kujiongoza na siyo kwa kuongozwa na tamaa au kwa kuwa mpenzi wako hayuko karibu nawe.


MKUMBO
Acha maisha ya kufuata mkumbo. Kama mwenzako amefanya kitu f’lani, basi eti na wewe unataka ukifanye au ukipate ili uonekane wa kisasa au mjanja. Kumbuka kuwa mwisho wa siku mtamaliza chuo na mengineyo, kila mtu atasambaa, kama uliharibu kwa mpenzi wako, mwenzio hatakuwepo tena na hapo ndipo utakapoanza kumangamanga na dunia

""Se.x is overrated play safe kama kijana usikubali kutafuta matatizo ambayo yataharibu bajeti yako ya maisha. Maana mtaji wetu sisi hustler ni afya ""'. fundi bishoo said
Mm wangu alipata kazi mkoa tena wilayani kijijini huko eti after miezi 2 naona anaanza kunipandishia mapega kwanza alinirahisishia kazi sana nilikuwa namvutia rada ajae nijipangue..

Nilimwambia tu kelebu kule huna cha kunitisha zaidi ya uchawi tu huko ulipo kenge kabisa..!yakaishia hapo.
 
Wataalamu wa Saikolojia na Uhusiano wanadai Mapenzi ya mbali ni kitu cha kawaida na Mtu unaweza kuyafurahia kama vile upo karibu na Mtu wako na siku zote mkaridhishana kimwili na kiakili (bila kuwaza kuchepuka), iwapo tu kati yenu kutakuwa na mawasiliano mazuri, urafiki wa karibu, uaminifu na kujitoa Mapenzini
Mh wanasema hivyo mm hainiingii akilini kabisa uwepo wa mtu matters a lot
 
Mapenzi ya mbali ili yaende na yasikuvurugwe lazima ujizime data ujifanye ujui chochote. Ukipiga usipopokelewa au ikikatwa unatulia kama hakijatokea kitu vile na baadae ukiuliza ukajibiwa kubali tu majibu bila kujali ni uongo au n kweli.
Yaan yana dumu sana kikubwa imani
kinachosaidia watsp video call na kutumiana picha
 
Hongera kwako ila binafsi mahusiano ya mbali sitaki kabisa kusikia bora niwe singo kuliko kuwa na mahusiano ya mbali.
Hapana mkuu
Kwa mapenzi distance is not a barrier, what matters a lot ni honesty respect and faithfulness,

And through sir God everything is possible for he who believes (Mark 9:23)
 
Mm wangu alipata kazi mkoa tena wilayani kijijini huko eti after miezi 2 naona anaanza kunipandishia mapega kwanza alinirahisishia kazi sana nilikuwa namvutia rada ajae nijipangue..

Nilimwambia tu kelebu kule huna cha kunitisha zaidi ya uchawi tu huko ulipo kenge kabisa..!yakaishia hapo.
Ahahahaha Magomvi ya mara kwa mara hufanya mmoja wenu ahisi kuchoka na mahusiano.
Inapotokea sababu za ugomvi ambao unahisi unaweza kuwa chanzo cha kuvunja mahusiano yenu ni afadhali ukazizuia na kutafuta siku nyingine ya kutatua tatizo hilo.
 
Kusumbuana? Me najua kama unampenda kweli mwenza wako utahitaji kumuona kila iwezekanapo lkn kumbe ni kinyume
Kwa wastani kama uanishi mbali na mpenzi wako, kama ni siku za kawaida hakuna dharura zozote wala kitu cha maana cha kuweza kuonane naye unapaswa kuongea naye si zaidi ya mara tatu kwa siku.

Ingawa mawasiliano ndiyo msingi mkuu wa mahusiano ya mbali kuhusu kuonana hilo suala lingine.
 
Hapana mahusiano ya mbali bora niwe single.
Kama kweli unampenda kwa dhati mwenza wako na mmetengana kutokana na sababu za kimasomo ama kazi kwa hakika utakuwa tayari kumtunzia penzi lake hadi mtakapokutana tena.
 
Back
Top Bottom