Kama una mpenzi ambaye yupo mbali yataka moyo sana

Fundi manyumba

Senior Member
Nov 25, 2018
177
287
Ni sehemu ndogo sana ya wapenzi wanaoishi mbalimbali ambao hudumu kwenye uhusiano wao kwa muda mrefu.

Hiki kinaonekana kuwa ni kitendawili kigumu sana kwa wapenzi wengi kuvumiliana kwenye uhusiano bila kusalitiana.

Ninapozungumzia umbali ninamaanisha wilaya na wilaya, wilaya na mkoa au mkoa na mkoa au nchi na nchi au bara na bara.

Ninaamini miongoni mwetu ama tumeshuhudia au kusikia au kuona au kuadithiwa kuwa kuna mwanaume au mwanamke ambaye alikuwa na mpenzi, mara mpenzi wake akapata nafasi ya kwenda kusoma mkoa mwingine au nchi nyingine, lakini mwisho wa siku ukasikia wapenzi wale wameachana baada ya mmoja kupata mpenzi mwingine huko aliko.

Inawezekana mpenzi wako alihamishwa kikazi nje ya wilaya uliyopo, lakini mwisho wa siku ukabaini kuwa mwenzio amepata mtu mwingine na mapenzi kwako yameanza kupungua au yamepungua kama siyo kwisha kabisa.

Kwanza kabisa ili udumu na mpenzi wako kuwa na ...

UAMINIFU
Kutokuwa na uaminifu miongoni mwenu, kama wapenzi mtakuwa ni waaminifu katika uhusiano wenu, basi kila unapoingiwa na pepo wa usaliti unakumbuka uzuri wa mpenzi wako, basi unaacha na kujizuia kisha unakuwa umemshinda pepo huyo.
Hili suala hata Equation x unaelewa

UZALENDO
Kutokuwa mzalendo kwa mpenzi wako. Jaribu kumpenda kwa kuwa ndiye uliyemchagua kuwa naye, kila siku Tanzania inasema watumishi wake wawe wazalendo, siyo wao tu hata mapenzi yanahitaji uzalendo wa hali ya juu. Uzalendo wa kupenda kitu chako, kumpenda mpenzi wako, mkeo, mumeo au mchumba wako.mkuu Analyse Lazima ujivunie, ujisifie kuwa naye kisha mthamini.

SUBIRA
Wapenzi kutokuwa na subira au uvumilivu; Hili nalo huchangia kwa kiasi kikubwa mapenzi ya mbali kuvunjika. Kama ilivyo subira ya kila mtu kuamini kuwa ipo siku ataondoka kwenye shida na ugumu wa maisha alio nao, basi Mzee wa kupambania amini na kuwa na subira au uvumilivu kwa mpenzi wako ili mfikie ndoto zenu.

MAZINGIRA
Jiepushe sana na mazingira ambayo yanaonekana kabisa yanaweza kukusababisha ukaingia kwenye uhusiano usio rasmi tena, pengine kwa mtu ambaye huna ndoto naye. Tatizo la kujiingiza kwenye uhusiano kwa sababu za kimazingira linaweza kukufanya ukajikuta umezama kwenye mahaba na mtu ambaye hana mapenzi na wewe na mwisho wa siku ukajikuta unaumia sana. Ukabaki kulaumu watu kama dronedrake

MAWASILIANO
Kutokuwa na mawasiliano ya mara kwa mara nayo huchangia sana kuvunjika kwa mapenzi ya mbali au kupoteza ladha, lakini kama mtu anakupenda kwa dhati, anakupenda tu, anaweza kukupigia simu na kukutumia SMS kibao, lakini akawa bado ni tatizo. Chunga sana mzee wa miongozo Smart911

TAMAA
Kama utaishi kwa kutamani vitu usivyokuwa na uwezo navyo ni dhahiri utajikuta unamsaliti mpenzi wako kwa kuwa tu uko mbali na unaona hawezi kukubana wala kukufuatilia. Ingawa ningekushauri ufanye kitu kwa kujiongoza na siyo kwa kuongozwa na tamaa au kwa kuwa mpenzi wako hayuko karibu nawe.

MKUMBO
Acha maisha ya kufuata mkumbo. Kama mwenzako amefanya kitu f’lani, basi eti na wewe unataka ukifanye au ukipate ili uonekane wa kisasa au mjanja. Kumbuka kuwa mwisho wa siku mtamaliza chuo na mengineyo, kila mtu atasambaa, kama uliharibu kwa mpenzi wako, mwenzio hatakuwepo tena na hapo ndipo utakapoanza kumangamanga na dunia

""Se.x is overrated play safe kama kijana usikubali kutafuta matatizo ambayo yataharibu bajeti yako ya maisha. Maana mtaji wetu sisi hustler ni afya ""'. fundi bishoo said
 
Summary ya huu uzi ni hii 👇

DISTANT LOVE KILLS 🤒😎
Wataalamu wa Saikolojia na Uhusiano wanadai Mapenzi ya mbali ni kitu cha kawaida na Mtu unaweza kuyafurahia kama vile upo karibu na Mtu wako na siku zote mkaridhishana kimwili na kiakili (bila kuwaza kuchepuka), iwapo tu kati yenu kutakuwa na mawasiliano mazuri, urafiki wa karibu, uaminifu na kujitoa Mapenzini
 
Wataalamu wa Saikolojia na Uhusiano wanadai Mapenzi ya mbali ni kitu cha kawaida na Mtu unaweza kuyafurahia kama vile upo karibu na Mtu wako na siku zote mkaridhishana kimwili na kiakili (bila kuwaza kuchepuka), iwapo tu kati yenu kutakuwa na mawasiliano mazuri, urafiki wa karibu, uaminifu na kujitoa Mapenzini
JICHANGANYE 😄😄
 
Mapenzi ya mbali yanachangamoto kubwa sana, hasa kwa sisi wanaume ni vigumu kuvumilia mwezi mzima huku ukiwa unaona warembo mbali mbali wenye shepu zao wakikuzunguka bila kudondosha neno.

Vinginevyo labda muwe na uwezo wa kukutana kila mwezi kama inawezekana, tofauti na hapo michepuko huwa inaokoa jahazi.​
 
Mapenzi ya mbali yanachangamoto kubwa sana, hasa kwa sisi wanaume ni vigumu kuvumilia mwezi mzima huku ukiwa unaona warembo mbali mbali wenye shepu zao wakikuzunguka bila kudondosha neno.

Vinginevyo labda muwe na uwezo wa kukutana kila mwezi kama inawezekana, tofauti na hapo michepuko huwa inaokoa jahazi.​
mapenzi ya mbali sio shida shida inakuja pale mmoja wenu anapata huduma na mtu mwingine ndo utaanza kuona madharau na ubize kama wote vinginevyo mapenzi ya mbali matamu sana kila mkikutana mnaonana wapya mkuu
 
Long distance relationship kwa karne hii ni sawa na kushikilia bomu lililo chomolewa fyuzi 🤒😎
Penye upendo wa dhati kati yao wote wawili, inawezekana kabisa!
Mawasiliano ya kila mara (calllings, sms, Whtsp, n.k) yakifanyika kwa dhati inawezekana.
Kama mawasiliano ya mara kw mara hayapo; ni ngumu kudumu.
 
Back
Top Bottom