SoC03 Jinsi ubunifu na teknolojia vilivyonisaidia mimi binti kuwa Graphics Designer

Stories of Change - 2023 Competition

Dynaphics

Member
Jun 5, 2023
5
12
UTANGULIZI
Dunia ya sasa na inakoelekea kuna kukua na kuenea kwa sayansi na teknolojia kwakuwa ina umuhimu sana katika kuleta mafanikio na maendeleo, mambo mengi yanatatuliwa kupitia teknolojia, mambo mengi yanaanzishwa kupitia teknolojia hivyo inanafasi nyingi sana. Lakini wanawake waliopo kwenye sekta hii ni wachache kwakuwa imezoeleka kuwa ni fani ya wanaume.

NAMNA NILIVYOANZA UBUNIFU NA KUITUMIA TEKNOLOJIA.
966FD82C-A9F2-435D-B2C9-B552FFB74C31.jpeg

Baada ya kumaliza stashahada ya sheria mwaka 2020 wakati nasubiri matokeo kutoka ili niweze kuendelea na elimu ya juu zaidi, nilikuwa na miezi kadhaa ya kusubiri kuanza kujisajili na shahada na sikutaka kukaa nyumbani bila kujishughulisha. Niliwasiliana na rafiki yangu mmoja ili anipe nafasi ofisini kwake, kwakua
alinifaham utundu nilionao wa simu alinishauri nijifunze graphic design ili inisaidie kufanya utundu wangu kwa ubora zaidi kupitia computer. Alinisaidia kuniunganisha na rafiki yake ambae ni miongoni mwa graphic designers wakubwa hapa Iringa ambae alinifundisha kwa wiki moja tu kuhusu mambo ya msingi ya kuyafahamu ya program moja inaitwa Adobe Photoshop na baada ya hapo kuanza kunipa vitu vidogo vya kufanya ili niweze kuongeza ujuzi. Nilianza kujifunza kutengeneza matangazo ya picha pamoja na kujifunza kutengeneza logo.

Rafiki yangu hakuachia kunipa nafasi ya kazi tu, aliniunga na group WhatsApp la wajasiliamali Iringa ambalo watu walituma taarifa mbalimbali kuhusu shughuli zao, baada ya kuona hivo nikajitengenezea tangazo kuonesha natoa huduma za graphics licha ya kuwa nilikuwa na ujuzi mdogo tu. Baada ya kulitengeneza nililituma kwenye group nikatafutwa na mtu mmoja alihitaji nifike ofisini kwake kesho yake akihitaji lebo ya chupa za sabuni ya maji aliyokuwa anatengeneza. Nilikubali kuonana nae lakini nilikuwa na woga sana, Ilipofika siku inayofata nilifika ofisini kwake kuzungumza nae na kuelewa anataka nini baada ya hapo nikarudi kwa mwalimu wangu wa graphics anielekeze cha kufanya. Baada ya kupewa maelekezo nilianza kuifanya kazi ile na kumtumia mhusika, alinizungusha sana kuhusu kufanya marekebisho mengi, niliirekebisha kazi sana na mwishowe hakuikubali kazi yangu.

Nilijisikia vibaya baada ya kuhangaika na kazi isipokelewe, lakini nilijisikia vizuri zaidi kwa kuwa na moyo wa kuthubu kwasababu ilinijengea uwezo wa kujiamini.

Kupitia mitandao ya kijamii kadhaa niliweza kujifunza vitu zaidi kuhusu graphics design, niliangalia video mbalimbali youtube za kutoa elimu, baada ya kujifunza nikawa nafanya mafunzo binafsi ili niweze kuongeza ujuzi zaidi.

Nilianza kupata kazi ndogo ndogo na kulipwa pesa ndogo sana ambayo ilinitatulia matumizi yangu madogo madogo sana. Muda mwingine nilikuwa nakaa bila kupata kazi naanza kuwafata watu kuwaelekeza niwafanyie kitu flani na kitawanufaisha vipi, kwa mfano biashara ni matangazo kupitia tangazo zuri la huduma au bidhaa flani likiwekwa kwenye mitandao ya kijamii linaweza kumfikia mtu fulani akavutiwa, ambapo nikikamilisha kumfanyia kazi mtu kama hivo naweza kupewa pesa kama malipo ama nisipewe kabisa. Ila cha muhimu ilikuwa kuongeza ujuzi zaidi kwenye kazi yangu.

Baada ya kurudi chuo kuendelea na shahada ya sheria nilifanya uzembe wa hali ya juu, niliacha kufanya kazi kwa kisingizio cha kuwa sitaki kuchanga masomo na kazi. Lakini siku zilivozidi kwenda nikawa naona wanafunzi wenzangu baadhi waliokuwa wakifanya kazi na kusoma, wapo waliokuwa na kazi ngumu zaidi kunizidi lakini bado walisoma na kujishughulisha, karoho kalinisuta na kuona wao wameweza mimi nitashindwa nini na shughuli zangu za kufanya kwenye laptop tu nisingekosa muda wa kuzikamilisha mbona muda wa kufanya mambo mengine niliupata, hivyo nikaanza kujirudi taratibu kujishughulisha.

Niliendelea na kuwaanza watu kuwaelekeza na kuwafanyia kazi ambapo nililipwa au kuto kulipwa, nikawa napata wateja pia mara moja moja, lakini pia nimekuwa nikijiunga mashindano mbalimbali ninayoyaona mtandaoni ya kutengeneza nembo za biashara, bidhaa au huduma mbalimbali, yote hayo ni kwa nia ya kuongeza ujuzi zaidi na kufikia watu wengi zaidi, muda huo niliongeza gharama ya makato kwakuwa kazi zangu zilikiwa bora zaidi.

UMUHIMU NILIOPATA KUPITIA UBUNIFU NA TEKNOLOJIA
1. Nimeweza kupata kipato kupitia kazi za kutengeneza matangazo, logo, business card na kadharika.
31071687-FDD8-48FF-855C-BEAC0C538470.jpeg

FF86195F-537D-4D2B-8339-4AF6EC6B2C1D.jpeg

4089DAF9-8FC7-4F65-AC06-E74B86953095.jpeg

2. Kuongeza ujuzi kiteknolojia kwasababu achilia mbali matangazo ya picha, najifunza kutengeneza matangazo ya mfumo wa video au katuni ili kuongeza ubunifu zaidi.
77DBD592-DB3B-46EF-943B-EC0A1715401D.jpeg

CHANGAMOTO NILIZOPITIA
1. Kukosa vitendea kazi kama computer yenye uwezo wa kuingia program za kazi za kutosha za kunisaidia kutoa kazi za ubora zaidi pamoja na vifaa vya ku print ili niweze ku print stika za bidhaa au business card.
2. Kama binti sio kila mtu anakutafuta kwa lengo la kukusaidia wengine wanakuwa na maswala yao binafsi na sio ki kazi kama kutaka kuanzisha mahusiano kitu ambacho kinakuwa hakipendezi hasa mtu ukiwa kikazi zaidi.

SULUHISHO
Kuwa na nidhamu, kujiamini pamoja na msimamo

MAMBO YA MUHIMU YA KUZINGATIA
1. Tukiwa na watu wa karibu sahihi watakuwa daraja la kufikia malengo makubwa hivyo ni muhimu kuchagua marafiki sahihi.

2. Kila unapopata nafasi jitahidi kutenga muda wa kujifunza kitu flani kipya ili kuongeza elimu na ujuzi zaidi ya ulionao kama nilivyofanya mimi nikiwa likizo, unaweza ongeza ujuzi kutoka kwa mtu wa karibu, kusoma vitabu, mitandao ya kijamii ama mahali penye mkusanyiko wa watu kama semina.

3. Sio kila muda usubiri wateja tu wakufikie, ukiachilia mbali kujitangaza au kutangazwa kwa namna yoyote unapoweza kufanya kazi hata za bure fanya hii itakusaidia kuongeza ujuzi wa jambo flani na kuongeza watu mana ukiwasubiri tu wanaweza wasije.

4. Kufeli si kushindwa mana kuna kazi nilihangaikia haikupendwa niliumia ila haukuwa mwisho wangu, ilikuwa muendelezo tu wa mimi kuongeza kujiamini zaidi na kupata msukumo wa kufanya kazi bora zaidi.

HITIMISHO
Nina ndoto za kuwasaidia vijana wenzangu hasa mabinti kupitia ujuzi nilionao ili kuweza kufikia malengo yao, kwa mfano binti mjasiliamali anaweza kuwa na bidhaa flani ila hajajua kujitangaza vizuri hivyo nitamshauri awe na nembo ya bishara ambayo itaweza kumtambulisha na kumtofautisha na watu wengine wenye huduma kama yake, pili nitamshauri na kumtengenezea tangazo kali la kuonesha na kufafanua zaidi kuhusu bidhaa au huduma anazojishughulisha nazo ambalo anaweza kulitumia kujipost na kujitangaza kupitia mitanda ya kijamii au kuwa na kipeperushi ambacho anaweza kukisambaza kwa watu flan ambao watapata uelewa wa shughuli yake. Yote hiyo naweza kufanya kwa ujuzi nilionao wa graphics design.
 
Back
Top Bottom