Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,385
34,029
Hii ndiyo nadharia inayosemwa inatakiwa kukubaliwa na kila binadamu na ndiyo nadharia inayoitwa na baadhi ya watu kuwa ni kamilifu na timilifu.

Kuwa hakuna ajue wewe binadamu umetokea wapi na kwa nini upo ivo ulivo. Kuwa Binadamu hana kusudio lolote lile la kuwepo kwake duniani.

Na haileweki imekuwaje binadamu kuna mambo anayoyaita mema na mengine anayaita mabaya.

Hitimisho ni kuwa binadamu ni kiumbe kisichoelezeka.
 
Absolutely yes.

Binafsi naamini kwamba Binadamu hana mwanzo wala mwisho, Yupo tu.

Ukianza kuweka ulazima wa kwamba kila kitu kilichopo lazima kiwe na chanzo, Basi hata
"chanzo cha vyanzo" lazima kiwe na chanzo chake,

Ili muundo ule ule wa ulazima huo ufuatwe. Pasiwepo kitu chochote kitakacho kwenda kinyume na ulazima huu kwa kujitokeza chenyewe tu pasipo mwanzo,

Maana kitavuruga muundo mzima wa ulazima huu na kuzua maswali mengi ya kimewezaje kuwepo bila chanzo.
 
Absolutely yes.

Binafsi naamini kwamba Binadamu hana mwanzo wala mwisho, Yupo tu.

Ukianza kuweka ulazima wa kwamba kila kitu kilichopo lazima kiwe na chanzo, Basi hata
"chanzo cha vyanzo" lazima kiwe na chanzo chake,
Nilivoiangalia hii ni KANUNI. Kama ni kanuni ni Lazima iwe na misingi yake.

ULAZIMA kuwa Kila chenye Mwanzo ni Lazima kiwe kina chanzo chake na hicho chanzo kinatakiwa kiwe na chanzo kingine na hali iendele hivyo unatokana na nini?

Hebu elezea kwa kina msingi Wa kanuni hii na uweke ithibati yake.
 
Nikiangalia maumbile ya binadamu na jinsi anavyoishi kwenye hii dunia, najiuliza imekuwaje amekuwa alivyo na jinsi hakuna kiumbe kingine kinachofanana na Binadamu kiutendaji wake.

Ukiangalia Kwa mfano, hivi kweli hakuna mbunifu wa binadamu ambaye ndiye aliyebuni uke ukae kwa mfumo ambao unaweza kuingiliwa na uume.

Hakuna mbunifu aliyebuni mji wa uzazi Kwa mwanamke na kuweka mbegu Kwa mwanaume? Kisha ukifanyika uingilianaji mimba inatungwa.

Baada ya binadamu kuzaliwa ukiangalia kwa makini unaanza kujiuliza, hakuna kweli mbunifu aliyejua kuwa binadamu Ili aishi atahitaji kula hivyo akamuumba akiwa na mdomo?

Mfumo wa kula mpaka kupata haja hakuna mbunifu wake kweli? Yaani mfumo wa mmeng'enyo wa chakula upo tu Wala haukukusudiwa kuwepo ila upo tu. Kweli?

Fikiria macho, masikio, ngozi, na viungo vingine vya binadamu vinavyofanya kazi. Waza kuwa hapa unaposoma hii mada macho, masikio yako yaache kufanya kazi itakuwaje?

Bado nawaza imekuwaje binadamu hana Mwanzo Wala mwisho??
 
Kanuni hii ni ya kwangu binafsi, Si kwamba ni kanuni ya watu wote.

Kanuni hii ni kutokana na kwamba watu wanaodai Mungu ni chanzo cha ulimwengu hawana UTHIBITISHO wa madai yao.
(Ni mawazo yao ya kufikirika tu)

Watu wengi wana amini Mungu Hana chanzo kwamba alitokea tu, Pia wana amini Mungu huyohuyo hana mwisho.

Watu wengi wameweza kuamini Mungu wasiyemjua Hana chanzo Lakini wana lazimisha kwamba Dunia ina chanzo, Na chanzo hicho wanadai ni "Mungu" Kwamba wana amini Haiwezekani Dunia iwe imetokea tu yenyewe Pasipo chanzo.

Sasa ni hivi👇

Kama "Haiwezekani" Dunia isiwe na muumbaji, kwamba lazima awepo aliye iumba "Imewezekana" vipi Mungu asiwe na Muumbaji?

Kama Mungu hana mwanzo, Inashindikana vipi kwa Dunia kutokuwa na mwanzo?

Huu ulazima wa kwamba Dunia lazima iwe na chanzo, ila Mungu yeye Hana chanzo uliwekwa na nani?

Hapa sasa ndipo,Kanuni hii inapo tumika kwamba,

Kama ni lazima kila kitu kilichopo kiwe na chanzo, Basi hata Mungu lazima awe na chanzo. Maana Mungu huyo bado "HAJATHIBITIKA" rasmi kwamba yeye ndio chanzo halisi cha ulimwengu.
( Bado ni mawazo na mafikirio ya watu tu)

Sasa kama bado Mungu HAJATHIBITIKA kuwa chanzo halisi cha Dunia, Hakuna ulazima wa kwamba Dunia imeumbwa na ina mwanzo.

Ila mtu akianza kuweka ulazima wa kwamba Dunia lazima iwe imeumbwa, Lazima athibitishe kwamba chanzo cha Dunia hakina mwanzo.

Na aeleze na kuthibitisha chanzo hicho cha Dunia, kimewezaje kuwepo bila chanzo kingine.
 
Infropreneur hii hoja kwamba kila chenye chanzo ni Lazima kiwe na chanzo na chanzo chake pia kiwe na chonzo unaweza kuirhibitishaje?

Na huoni kwamba (Kwa maelezo yako) eti chanzo kisipojulikana chanzo chake hicho chanzo kipo tu.

Hivi chanzo cha bahari ni nini??
 
Nikiangalia maumbile ya binadamu na jinsi anavyoishi kwenye hii dunia, najiuliza imekuwaje amekuwa alivyo na jinsi hakuna kiumbe kingine kinachofanana na Binadamu kiutendaji wake.

Ukiangalia Kwa mfano, hivi kweli hakuna mbunifu wa binadamu ambaye ndiye aliyebuni uke ukae kwa mfumo ambao unaweza kuingiliwa na uume.

Hakuna mbunifu aliyebuni mji wa uzazi Kwa mwanamke na kuweka mbegu Kwa mwanaume? Kisha ukifanyika uingilianaji mimba inatungwa.

Baada ya binadamu kuzaliwa ukiangalia kwa makini unaanza kujiuliza, hakuna kweli mbunifu aliyejua kuwa binadamu Ili aishi atahitaji kula hivyo akamuumba akiwa na mdomo?

Mfumo wa kula mpaka kupata haja hakuna mbunifu wake kweli? Yaani mfumo wa mmeng'enyo wa chakula upo tu Wala haukukusudiwa kuwepo ila upo tu. Kweli?

Fikiria macho, masikio, ngozi, na viungo vingine vya binadamu vinavyofanya kazi. Waza kuwa hapa unaposoma hii mada macho, masikio yako yaache kufanya kazi itakuwaje?

Bado nawaza imekuwaje binadamu hana Mwanzo Wala mwisho??
Mbunifu huyo alitokea wapi?

Kabla ya kubuni hivi vitu, Huko aliko kuwa huyu "mbunifu" kulitoka wapi?

Hiyo sehemu aliyo kuwepo huyu mbunifu kabla haja anza ubunifu wake iliumbwa na nani?

Mbunifu huyu aliwezaje kutokea tu Vuuuuuuuuuuh!😄 From Nothing aka anza ubunifu?

Kwamba hakuwa sehemu yeyote ile?
 
Sawa kabisa.

Sasa wewe nimegundua kuwa unawaza kwa mtizamo wa uwezo wako wa kibinadamu

Kwani mbunifu ni Lazima awe na sifa zinazofanana na alivyoviumba? Labda hatujui maana ya kuumbwa
 
Infropreneur hii hoja kwamba kila chenye chanzo ni Lazima kiwe na chanzo na chanzo chake pia kiwe na chonzo unaweza kuirhibitishaje?

Na huoni kwamba (Kwa maelezo yako) eti chanzo kisipojulikana chanzo chake hicho chanzo kipo tu.

Hivi chanzo cha bahari ni nini??
Si kwamba kila chenye mwanzo lazima kiwe na mwanzo, Hapana.

Ila kwa vile unashindwa kuamini Dunia Haina chanzo, Na unataka kuweka ulazima wa kwamba Dunia ina chanzo.

Basi hapa Nita kuuliza, ulazima huu unatoka wapi?

Unathibitisha vipi kwamba Mungu ndiye chanzo na Hana chanzo?
 
Sawa kabisa.

Sasa wewe nimegundua kuwa unawaza kwa mtizamo wa uwezo wako wa kibinadamu

Kwani mbunifu ni Lazima awe na sifa zinazofanana na alivyoviumba? Labda hatujui maana ya kuumbwa
Wewe ulitumia mtazamo gani tofauti na wa kibinadamu, kujua Mungu yupo?

Mtazamo wako huo ulio utumia kujua Mungu yupo, Unaweza kumthibitisha Mungu huyo yupo kwa namna gani?

Na si mawazo yako ya kufikirika tu?
 
Kwa Nini ufikierie kwamba binadamu Hana muimbaji we ukipita mjini unaona vingapi majumba magari, bizaa mbalimbali kutijua tu mmtengenezaji haimannishi vimejitokeza tu vyenyewe
Kwani ni lazima kila kitu kilichopo kiwe kimetengenezwa?

Huu ulazima umeutoa wapi?

Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na mtengenezaji wake, Mungu ametengenezwa na nani?

Na mtengenezaji wa Mungu ametengenezwa na nani?

Na mtengenezaji wa "mtengenezaji wa Mungu" ametengenezwa na nani?
 
Swali la kizushi

Hivi utofauti wa Lugha za binadamu upo tu hauna chanzo chake?

Nguvu aliyonayo binadamu dhidi ya viumbe vingine na mazingira ya ulimwengu hakuna chanzo chake?

Binadamu hana kusudi la kuwepo kwake duniani?

Kwa nini binadamu huzaliwa wakati Iko siku atakufa. Huu mchakato wa kuzaliwa mpaka kufa hauna maana yoyote ile?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom