Je, binadamu ni mfano wa seli ndani ya umbile la Mungu?

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,253
5,411
Ulimwengu wote kwa jinsi ulivyo unamtegemeano wa moja kwa moja kwa kila kilichomo huwa na mwingiliano na chenzake "kutegemeana kimazingira".

Hivyo basi kama haishivyo chawa au kupe juu ya ngozi ya mnyama mwingine ni sawa pia na wale wadudu waishio katika utumbo mpana tumboni mwa mnyama huyo pasipo na madhara yeyote.

Lengo si kuzungumzia baiolojia ila najaribu tu kufikiri kwa picha kubwa dhahania juu ya uwepo wa Mungu na mwingiliano wake na binadamu kupitia kanuni hii ya kiulimwengu.

Tuseme Mungu ni ulimwengu "yaani ulimwengu na vyote vilivyomo ni ukamilisho wa mwili wake' hivyo basi binadamu nikama chembechembe nyeupe au nyekundu za damu yake tu na pia bila uwepo wa binadamu ndani yake na yeye hana maisha.

Nini kinafanya niseme hivi;

kama isingekuwa hivyo kwanini Mungu hawezi kumwondosha binadamu huku kila siku anamkosea?

Kwanini aseme tuko ndani yake na yeye ndani yetu?(kumbe kuna kutegemeana)

kwanini sisi nao hatuite ni miungu pia?(je,ni kwakuwa nasi tunayo miili ndani ya miili tuna seli ndani ya seli tuna DNA na DNA hizo ndiyo sisi na sisi ndiyo ulimwengu wenyewe wa viumbe hai na visivyo hai ambao twamuumba yeye)

Kama yeye ni muumba wa vyote na chanzo cha kila kitu basi uovu na haki vyote ni sifa ya matendo yake na anatutaka tuishi ndani yake katika utaratibu wa kiafya utakaomwepusha na kuangamia "ulimwengu usiharibiwe sababu ndiyo makazi ya roho yake"

Kwanini tupumue na Mungu pia apumue kama sisi? Je, upepo (mfano wa pumzi) udongo (mfano wa chakula) na maji (mfano wa damu) si chanzo cha uhai wetu tukiwa hapa duniani na twajivunia tukisema asilimia 70 miili yetu ni maji, sasa naonekanaje kama nimechanganyikiwa nikiusanisha kitendo hiki na mfano wa seli hai zinavyosurvive ndani ya miili yetu.

Je, kwanini ujiulizi katika maandiko yeyote yale Mungu haja-ahidi kumwangamiza mdhambi yeyote completely akiwemo shetani badala yake watachomwa moto milele, najua utasema roho mara nafsi haifi nakubali juu ya nadharia hiyo ila ni kwa vipi mtu "Mungu"" anaweza kujiangamiza mwenyewe?

(atakapo choma moto milele part ya mwili wake utakuwa ni mfano wa kujiadhibu yeye mwenyewe kwa matendo yake

(yaani upande mmoja wa makosa 'shetani' utaisi maumivu daima na wema 'utaishi kwa amani' hii ni sawa na kuugua ugonjwa usio na tiba ambapo adhabu yake ni kuukubali na kuishi nao katika face mbili tofauti yaani upande mwingine waendelea kuenjoy maisha yako kama kawa ila upande mwingine waendelea kugugumia na maumivu pasipo kugive up juu ya uhai wako)

Ndiyo maana kukata tamaa ni kosa kubwa mno katika neno lake yaani yeye hajajikatia tamaa mwenye mwili wake afu wewe tuseli bilioni ujiwaishe kufa lazima atajitahidi kuulinda mwili wake dhidi ya maradhi ya aina yeyote ile.

Baada ya kutafakari kwa akili hizi hizi finyu za awamu ya sita nimebaini kuwa kama tulivyo sisi ndani ya ulimwengu tuliojikutamo hata bakteria pia utuzoom kama ulimwengu wakiwa nje au ndani yetu na sisi umzoom tuliye ndani yake kama ulimwengu na tukishindwa kumjua kwa sababu ya ukubwa wake usiosemekana tunamwita "Mungu"

lakini ukweli ni kuwa nishati ya kujiendesha na kukabiliana na mazingira yake na siye pia tunamchango hivyo kwa pamoja sisi ni system moja na wote ni kama hatujui tumefikaje fikaje hapa na tuko wapi na tunaenda wapi ndiyo maana hakuna ahadi ya moja kwa moja ya mwisho wa ulimwengu ni lini kwa maana pengine hata ulimwengu mwenyewe hajui mwisho wake ni lini.
 
Kwanza kabisa hakuna sehemu Mungu amesema yeye yupo ndani yetu

Ila kuna vitabu vimeandika madai ya ayosema kuwa Mungu amesema yeye yupo ndani yetu.

Hizo ni sentensi mbili zinazotofautiana na zote zinazungumzia kitu ambacho hakijathibitishwa.
 
ya kutafakari kwa akili hizi hizi finyu za awamu ya sita nimebaini kuwa kama tulivyo sisi ndani ya ulimwengu tuliojikutamo hata bakteria pia utuzoom kama ulimwengu wakiwa nje au ndani yetu na sisi umzoom tuliye ndani yake kama ulimwengu na tukishindwa kumjua kwa sababu ya ukubwa wake usiosemekana tunamwita "Mungu
Actually kibaiolojia, unaweza kumuona Mungu kwa staili hiyo.

Lakini ambaye tunaishi naye ndani yake na yeye ndani yetu kwa levo yetu ni Yesu.
Yesu ndio anakuwa tena ndani ya Mungu na Mungu ndani yake overall ndio hivyohivyo tu

UNAWEZA KUPITIA PIA HAPA kwa udadavzi wa hii concept bwana UndavaWazo la Mungu linavyojionesha kwenye miili na mifumo/Mfumo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom