Kazi ya binadamu duniani imeshaisha takriban miaka 445,000 iliyopita

baro

JF-Expert Member
May 12, 2014
2,988
3,733
Binadamu ni project au mpango wa viumbe wa sayari ya mbali ambao walimtengeneza binadamu kwa ajili ya kazi yao ambayo ilikuwa ni kufanya kazi katika migodi ya dhahabu.

Sayari ya Dunia Ilivyotokea na kuwa kitovu cha dhahabu (A Planet Of Gold)

Kabla ya miungu ya juu haijakuwapo. Sayari ya Ki (dunia) kabla haijatokea na ulimwengu ulikuwa utupu, Peke yake kwenye utupu kulikuwa na Apsu, Mzaliwa wao wa Kwanza wa AEON(Creator of all). Katika vilele vya Juu, miungu ya mbinguni ilikuwa bado haijaumbwa,Katika chini ya maji, miungu ya mbinguni ilikuwa bado haijaonekana.

Juu na chini, miungu ilikuwa bado haijaundwa, hatima ilikuwa bado haijaamuliwa. Bado hakuna mwanzi ambao ulikuwa umeumbwa, hakuna ardhi yenye vilima iliyotokea,Apsu alitawala peke yake kwenye utupu.Kisha kwa pepo zake maji ya kwanza yalichanganyika kwa nguvu ya kimungu na wa juu ya maji alila usingizi fofofo.

Katika usingizi huo fofofo juu ya vilindi vya maji Apsu alijetengeneza mke aliyeitwa Tiamat (Mama wa Wote).Mama wa mbinguni, mrembo wa maji kwelikweli alikuwa,katika huo usingizi fofofo Tiamat akajifungua mtoto aliyeitwa Mummu ambaye alitokea pembeni ya Apsu. Baada ya Tiamat kujifungua Mummu , Apsu alimpa zawadi ya kung’aa ambayo ni chuma ing’aayo (dhahabu pekee ya yeye kumiliki milele na milele). Basi hao wawili maji yao yalichanganyika tena na watoto wa kimungu baina yao wakazaliwa nje.

Chini ya maji Mwanamume na mwanamke waliumbwa; waliitwa kwa majina Lahmu na Lahamu,Apsu na Tiamat wakawapa makazi Lahmu na Lahamu chini yao maji huko mbinguni.

Juu ya maji Anshar na Kishar waliumbwa, wakakua na kuwazidi ndugu zao kwa ukubwa hawa pia walimbwa kama wanandoa huko mbinguni, wakazaa mtoto waliyemwita An, katika mbingu za mbali na kuwa mrithi wao na Antu akawa mke wa An na makao yao yakawa juu ya maji huko mbinguni.

Hivi ndivyo walivyoumbwa wanandoa watatu wa mbinguni, Chini na Juu, katika vilindi vya maji vilivyoumbwa( Wanandoa hawa ni Lahmu na Lahamu, Anshar na Kinshar pia An na Antu),Kwa wote majina waliitwa, familia ya Apsu pamoja na Mummu na Tiamat.

Wakati huo, sayari ya Nibiru alikuwa bado haijaonekana, Dunia ilikuwa bado haikuwepo. Maji ya mbinguni yalikuwa hayajachanganyika na bangili ya mbingu iliyoitwa (Hammered bracelet) ilikuwa bado haijajitenga kutoka kwa Tiamat.Wakati huo, mizunguko ilikuwa bado haijaundwa kikamilifu,Hatima za miungu zilikuwa bado hazijaamriwa kwa uthabiti,Ndugu wa mbinguni waliungana pamoja, njia zao zilikuwa zisizo na uhakika.

Kwa Apsu njia hizi zilimchukiza sana kwa sababu hazikuwa za uhakika,Tiamat pia, hakupata kupumzika, alihuzunika na kukasirika , hivyo Tiamat akaunda umati wa kuandamana naye kando yake,alizaa jeshi lenye kunguruma na lenye hasira dhidi ya wana wa Apsu. Kwa kuwa Tiamat alikuwa na uwezo wa kimungu alijizalisha watoto kumi na moja, Alimfanya mzaliwa wa kwanza aitwaye Kingu, kuwa mkuu kati yao yaani alipewa cheo cha kutoa Amri kama kamanda na akamwekea ubao wa hatma kifuani mwake,kupata mzunguko wake mwenyewe , ili kupigana na miungu uzao wake Tiamat na Apsu.Wakati miungu ya mbinguni iliposikia kuhusu hili, waliitisha kikao cha baraza kujadili. Miungu ilijadili nani atasimama dhidi ya Tiamat? miungu iliulizana. Hakuna hata mmoja katika mizunguko yao aliyesonga mbele, hakuna silaha ya vita ingebeba.

Kutokana na hayo ya Tiamat na baraza la miungu kuhusu Kingu,katika moyo wa kilindi cha maji mungu mpya alizaliwa katika chumba cha Hatima, mahali pa hatima. Aliumbwa na Muumba mwenye ustadi, alikuwa mwana wa Jua lake mwenyewe. Kutoka kilindini ambako alizaliwa, mungu huyo Jua aliondoka kwa haraka pamoja na zawadi ya Muumba wake, Mbegu ya Uzima, aliondoka navyo vyote. Alikokwenda mungu huyu Jua aliweka njia yake kwenye utupu hatima mpya aliyokuwa akitafuta akawa ameipata kama lilivyokuwa lengo la Apsu.

Wa kwanza kumuona mungu Jua kama anga inayotangatanga alikuwa Antu aliyekuwa akitazama kila mara. Umbo lake lilikuwa la kuvutia, mng'ao aliokuwa akiangaza,Mwendo wake ulikuwa wa Bwana, mwendo wake ulikuwa mwingi sana. Kati ya miungu yote iliyoumbwa na Apsu alikuwa mkuu zaidi, kupita miungu mingine, Jua yeye alikuwa mzunguko wake uliokamilika wala usiochukiza kama miungu wengine. Mungu Antu kwa kuwa ilikuwa jinsia ya kike alipomtazama tu mungu Jua, titi lake kwa mtoto halikunyonyesha kamwe. Mungu Jua akamuita Antu njoo, uwe mwanangu! Alimwita,acha niwe mama yako, Alitupa wavu wake na kumkaribisha, akafanya mwendo wake kwa madhumuni yaliyofaa.

Mwendo wa Antu ukabadilika baada ya kukubali mzunguko wa Jua na uso wa Antu ukageukia kwa An mumewe na ukaonekana vizuri, An alipoonekana mungu Jua akamwambia An, Mwanangu! Mwanangu! Hongera kwa kwa kuinuliwa na alipiga kelele na akasema Utawekwa kwenye uongozi, jeshi karibu nawe litakuwa watumishi wako acha Nibiru liwe jina lako, mungu Jua aliinama kwa Nibiru, akigeuza uso wake kwenye kifungu cha Nibiru, alitandaza wavu wake, kwa Nibiru alitoa watumishi wanne, Mwenyeji wake kando yake kuwa: Upepo wa Kusini, Upepo wa Kaskazini, Upepo Mashariki na upepo Magharibi.

Baada ya An na Antu kuwa Nibiru na akapata mzunguko kupitia mungu Jua, mungu Anshar alitangaza kwa furaha huko mbinguni kuhusu Nibiru kuwasili katika mzunguko wa jua.

Anshar akamtuma mjumbe aitwaye, Gaga, ambaye alikuwa kando yake, kama mjumbe alitumwa kwa An (Nibiru) afikishe ujumbe huu na akasema.

“Tiamat, yeye aliyetuzaa, sasa anatuchukia, ametengeneza jeshi linalopigana dhidi yetu, amekasirika kwa hasira ,Juu ya miungu, watoto wake mwenyewe, mashujaa kumi na mmoja aliowazaa wanaoongozwa na Kingu wanandamana naye, Kingu kati yao akampa ukamanda, akamwekea ubao wa hatima kifuani mwake bila haki ,Hakuna mungu kati yetu anayeweza kusimama dhidi ya jeshi lake,acha Nibiru awe mlipiza kisasi wetu, acha amshinde Tiamat, aokoe maisha yetu,Kwa ajili yake anaamuru hatima yetu, na aende na kukabiliana na adui yetu mkuu ambaye ni Tiamat”

Baada ya ujumbe huo An wa Nibiru alimjibu Gaga kwa ajili ya kupeleka ujumbe kwa Anshar na kusema

“Niko tayari kuanza vita dhidi ya Tiamat na kama nikishinda na kuokoa maisha ya miungu basi Anshar akutanishe miungu yote na atangaze ukuu wa hatma yangu na miungu yote ikubaliane barazani kunifanya kuwa kiongozi na wasujudie amri yangu”

Miungu yote ilikubali na kushauriana Ili kumfanya Nibiru kuwa Mlipiza kisasi wao wote walikubali, kwake hatima iliyotukuka iliamriwa. Kuanzia leo na kuendelea, amri zako haziwezi kupingwa wakamwambia.

Hakuna miungu miongoni mwetu atakaye ruka mipaka yako,Nenda, Nibiru, uwe mlipa kisasi wetu, Walimtengenezea mzunguko wa kifalme kuelekea Tiamat,Walitoa baraka kwa Nibiru, walitoa Nibiru silaha za kutisha. Anshar alitoa pepo tatu zaidi kwa Nibiru zilileta: Upepo Mwovu, Kimbunga, Upepo Usio na Kifani.

Kishar alitoa mwali mkali uliojaza mwili wake, wavu wa kuifunika Tiamat katika vita. Kwa hivyo akiwa tayari kwa vita, Nibiru kuelekea Tiamat aliweka mkondo wake(orbit) moja kwa moja. Sasa haya ndiyo maelezo ya Vita vya Mbinguni,Na jinsi dunia ilivyotokea, na hatima ya Nibiru.

Vita ikapiganwa kati ya Nibiru na Tiamat ambaye ni bibi yake na Nibiru, Tiamat akiwa na wafuasi wake 11 wakiongozwa na Kingu walipigana vita lakini walishindwa na Nibiru kwa msaada wa miungu wengine , Tiamat akauliwa na wafuasi wake wote 11 wakakamatwa na kibao cha hatma akanyangaywa Kingu na kufungwa na pia Tiamat akafungwa huku akiwa maiti

Tiamat mfu baadae akagawanyika na sehemu yenye maji na dhahabu ikatoka kwake na kwenda mbali zaidi kwa msaada wa upepo ambapo ndio ikawa sehemu ya dunia hii ya leo.

Apsu baada ya kuona Nibiru ameshinda vita dhidi ya Tiamat muasi akamuagiza Nibiru kuwa ,”Kwa miale yako ya joto, toa uponyaji kwa majeraha,acha sehemu iliyovunjika kwa Tiamat ipewe maisha mapya, katika familia yako kama binti na kuwa maji na yakusanyike mahali pamoja, nchi iliyo imara ionekane,Kwa Ardhi Imara na aitwe, Ki (Dunia) tangu sasa jina lake liwe hivyo”

Apsu aliendelea kusema kwa Nibiru “ Acha Dunia(Ki) iungane na familia yangu, Ardhi Imara ya chini, acha Dunia jina lake liwe, Kwa kugeuka kwake iwe mchana na usiku,katika siku zile za miale yangu ya uponyaji kwake,Hebu Kingu awe kiumbe wa usiku, kuangaza usiku 1 atamteua rafiki wa dunia ambaye ataitwa Mwezi kuwa wa milele,Nibiru aridhika na maneno ya Apsu alizivuka mbingu na kuzichunguza nchi,Miungu iliyompandisha cheo akawawekea vituo vya kudumu,Mizunguko yao aliiweka kwamba hakuna atakayevuka wala kupungukiwa na mwenzake.Aliimarisha kufuli za mbinguni, milango ya pande zote mbili aliiweka. Pia Nibiru akachagua makao ya nje na miungu wengine akaomba mzunguko mkubwa kuwa hatma yake na akakubaliwa”

Miungu yote ilizungumza kutoka kwenye vituo vyao: Wacha enzi ya Nibiru iwe kubwa zaidi,yeye ni mng'aro zaidi wa miungu, basi awe Mwana wa Jua, Kutoka sehemu yake Apsu alitoa baraka zake.

Pia Apsu akongeza kwa kusema “Nibiru itashikilia kuvuka kwa Mbingu na Dunia, Kuvuka litakuwa jina lake,Miungu haitavuka juu wala chini, atakuwa na cheo cha kati, atakuwa mchungaji wa miungu. Sharti itakuwa mzunguko wake, kwamba Hatima yake itakuwa milele”

Hii ndio namna ulimwengu ulivyoanza, miungu ya mbinguni kuumbwa na kutokea kwa dunia kutokea hadi sasa.

Binadamu alivyotokea

Miaka 445,000 hivi iliyopita, wanaanga kutoka sayari nyingine walikuja duniani kutafuta dhahabu.

Wakiruka chini katika moja ya bahari za Duniani(ambapo ilijulikana kama sayari KI), walipanda ufukweni na kuanzisha makazi waliyoyaita Eridu (maana yake "Mbali na nyumbani." ). Baada ya muda makazi ya awali yalipanuka hadi kufikia misheni/vituo kamili Duniani vya wenzao kufikia, vituo hivyo vilikuwa ni Kituo cha Kudhibiti Misheni, kituo cha anga za juu, shughuli za uchimbaji madini, na hata kituo cha njia Mirihi(Kituo katika sayari ya Mars).

Viumbe hawa waliitwa wana wa ANU au ANUNAKI(viumbe toka mbinguni), walitoka sayari iliyoitwa NIBIRU( leo inajulikana kama sayari X au planet X), kiumbe wa kwanza kufika hapa duniani aliitwa ALALU akiwa na Pilot wa chombo chake cha anga aitwae ANZU ambaye ndiye pilot wa kwanza kutua kwenye sayari ya Lahmu(Mars) na baadae Duniani (Ki).

Safari ya Alalu Duniani

Alalu alikuwa mfalme wa NIBIRU lakini alinyanganywa madaraka kutokana na uongozi mbaya na pia kushindwa katika shindano la mieleka ambalo lilimpa kiti cha ufalme Anu na hivyo akaamua kutoroka NIBIRU na vifaa vya anga pamoja na silaha za maangamiz (Nuclear weapons) na kuelekea Duniani, Kutoroka kwa Alalu kutoka Nibiru ulikuwa mwanzo wake wa kugundua dhahabu.

Alalu alijaliwa ufahamu mkubwa na maarifa mengi aliyoyapata kwa kujifunza kutoka kwa babu yake Anshargal na Enshar wa huko mbinguni NIBIRU,Kwa hivyo Alalu alijifunza mengi pia kutoka kwa wahenga na makamanda mbalimbali wa vita. Pia alijifunza kuhusu vita ya Tiamat ambayo ilipelekea kutokea kwa Bangili Iliyopigwa Nyundo(Hammered bracelet) na sayari ya dhahabu na maji ambayo ni Dunia(Ki).

Alipofika Duniani na chombo chake cha anga hakukuwa na sauti wala mtu wa kumkaribisha alikuwa yeye na pilot wake Anzu katika sayari ya kigeni,Kulikuwa na vilima,kulikuwa na mimea mingi,Mbele yake kulikuwa na mabwawa, akachukua kifaa cha kutafuta dhahabu kwa kukiweka ndani ya maji na matokeo akapata kuwa kwenye maji kuna dhahabu, hivyo aliruka kwa furaha na kusema sasa hatma ya NIBIRU iko mikononi mwangu.

Alirudi kwenye chombo chake cha anga na kutuma ujumbe katika sayari ya NIBIRU kuwa “ Katika ulimwengu mwingine mimi niko, dhahabu ya wokovu nimepata,Hatima ya Nibiru iko mikononi mwangu; kwa masharti yangu lazima uzingatie, haya yalikuwa maneno ya Alalu kwa mfalme wa NIBIRU aitwaye Anu” baada ya ujumbe huu mfalme Anu aliitisha baraza na kuwaeleza kila kitu pia wajumbe wa baraza walishangaa walijua Alalu ameshakufa, hivyo ili kuhakikisha ikabidi ateuliwe mtu wa kwenda kuhakikisha kama ni kweli, hivyo Mkwe wa Alalu ambaye pia alikuwa mtoto wa Kwanza wa mfalme Anu akajitolea kwenda kuhakikisha, hivyo safari ya kutoka NIBIRU kuja duniani ikaanza tena, ambapo sasa ni EA mtoto wa Anu na Mkwe wa Alalu.

EA mwenye hekima pia alishauri sababu kuna uadui kati ya mfalme Anu aliyepo madarakani na Alalu mfalme aliyeondolewa basi kama dhahabu ikithibitika ipo , takwa la Alalu kupewa kiti cha ufalme litekelezwe kwa kupigana tena mieleka katia ya Anu na Alalu na atakayeshinda atakuwa mfalme.

Ushauri huu ulikubaliwa na baraza na iliyobaki sasa ni EA kuja duniani kuhakikisha uwepo wa dhahabu kama alivyotuma taarifa Alalu.

EA alifika duniani na kuhakikisha kuwa dhahabu ipo na Alalu alituma taarifa za kweli, hivyo basi unaanzishwa mkakati wa kuletwa wataalam na wafanyakazi duniani kwa ajili ya kuchimba dhahabu ambayo itasaidia kuokoa sayari yao ya NIBIRU.

Wafanyakazi wa migodi ya dhahabu ambayo iliitwa Abzu (Afrika kusini na Zimbabwe ya sasa) waliitwa Igigi wana wa Anunaki walifanya kazi lakini walianza uasi kwa sababu walikuwa wanachoka sana, hivyo basi EA ambaye baadae alipewa jina la ENKI alikuwa anafanya utafiti kuhusu viumbe walivyoikuta duniani ambao walikuwa kama jamii ya sokwe, Enki aligundua kuwa hawa viumbe walikuwa kama wao lakini wao ni kama hayawani na wanaishi na wanyama na wanatembelea miguu 4.

Baada ya uasi wa Anunaki wa migodini, Enki anawashirikisha ndugu zake waliokuja duniani kusimamia shughuli za uchimbaji dhahabu ambao ni Enlil mdogo wake na mrithi halali wa kiti cha ufalme huko Nibiru sababu mama yake ni mke wa ndoa na Enki yeye ni mtoto wa mke mdogo, pia dada yao aitwae Ninmah na mtoto wa Enki ambaye alikuwa mbobezi wa sayansi (genetic engineering).

Katika mjadala huo, Enlil anapinga sana pia kutokana na cheo chake cha Lord of Command anapinga wazo hilo , lakini wenzake wanamwambia bila hivyo uasi utaendelea na tutakosa dhahabu ya kwenda kuzida sayari yetu, Enilil anasema kazi ya uumbaji ilishafanyika na ni ya Aeon(Creator of All) hivyo sio kazi yetu,

Ninmah, dada yao anajibu kwa kusema sisi hatuumbi bali tunafanya genetic engineering sababu kiumbe kimeshaumbwa tayari na AEON, mzozo unakuwa mkubwa inabidi watume taarifa NIBIRU , baraza la kifalme linakaa na kujadili na hatimaye wanaruhusu mchakato wa kutengeneza kiumbe huyo ambaye aliitwa LULU.

Yanafanyika majaribio takaribani 39 na jaribio la 40 ndilo linaleta matokeo chanya ambapo binadamu wa kwanza anazaliwa na kuitwa Adam na mke wake anaitwa Ti-amat, huyu binadamu anakuuwa na ufanano wa Anunaki.

Lakini jambo la ajabu huyu binadamu hazai, hivyo Ningshizda mtoto wa Enki anawaita Ninmah na Enki katika nyumba ya uhai (House of Life) ambapo binadamu alitengenezwa kuwa kuchanganya udongo wa dunia na formula za Nibiru.

Ningshizda anawaambia Enki na Ninmah alichogundua na nini anataka kufanya ili hawa viumbe wazaliane ili waweze kufanya kazi migodini, anagundua kuwa katika Genetic engineering binadamu wana tree of branches 22 wakati wao Anunuaki wanazo 22 hivyo kwenye DNA yao kusababisha wao kutozaliana sababu hizo branches 2 zilizokosekana ndizo za uzazi, hivyo anawwambia inabidi awapige sindano za usingizi na atoe kila mmoja kwenye ubavu wake branches 2 za DNA na kuwawekea Adam na Ti-amat.

Ningshizda anafanikiwa kuwalaza Enki na Ninmah na kutoa hizo branches na kuziweka kwa Adam na Ti-amat lakini wenzake wakawa na wasiwasi kuwa hizo branches 2 ndizo zenye siri pia ya uhai ya wao Anunaki kuishi miaka mingi, Ningshizda anawajibu kuwa kuhusu uhai amezingatia na hawa viumbe wataishi miaka michache.

Hivyo baadae Adam na Ti-amat wanaanza kuzaa wafanyakazi wa migodini kama dhumuni lilivyo la wao kufanya kazi za migodini na Anunaki wapumzike.

HIVYO BASI KAZI YA BINADAMU ilikuwa ni kufanya kazi za migodini haya mengine yaliyojitokeza kama shetani,dini n.k sio ya Mungu (AEON) bali ni ya viongozi wa Anunaki ambao baadae walifundisha binadamu wawaabudu.

Hivyo basi, binadamu hakuumbwa na Creator of All(AEON) bali ni Genetic Engineering tu ya wana wa Anunaki ambao sio miungu bali sisi tuliwaita miungu.

Viongozi wa Annunaki hapa duniani , majina yao na tunavyowatambua

  • Lord Enki – LUCIFER (Omnipotent)
  • Lord Enlil – YAHWEH
  • Ninmah – LILITH
  • Ningshizida – Thoth/Ibilisi
  • Horus- Yesu ( Mungu wa Misri ya kale)
Baadae ilitokea vita ya kuabudiwa na wao kwa wao wakaanza kupigana na kutafuta ushawishi wa kuabudiwa hadi leo.

CREDIT: Maelezo haya ni kutoka katika nyaraka mbalimbali zilizogunduliwa SUMERIA (Mesopotania).
 
Hizi hekaya ni sawa na Hekaya za Alfu Lela ulela...

Asante kwa Fasihi simulizi
Screenshot_20231226-175328_1.jpg
 
Ningekua mimi ndio mungu nilie umba watu na binadamu basi ningekua nakuja kuwatembelea viumbe wangu kuwapa elimu nakufanya waniamini mimi tu. sasa imagine now days niamini vitabu tu ambavyo vimeandikwa na mtu kama mimi hapana siwezi. et niamini story ambazo hazieleweki hata.
 
Hawajafunga ila wamebadilisha ratiba ya kula. Siku ina masaa 24 wao wameamua kutumia masaa ya kulala kula badala ya kawaida tuliyoizoea.

Kinachonikera ni pale jamii yao wanapokuwa wengi mahali fulani hutaka watu wengine nao wabadiri ratiba zao za kula pasipo sababu za msingi
 
ukutaka kujua hilo historia halisisimui linazungumzia mambo yaleyale yakibinadamu!,ndoa,vita,utumwa na uzazi!!.
kwa mimi binafsi nikianza kuzungumzia mambo ya kimungu siwezi kugusia vitu vidogo vidogo kama hivyo!,maana tafsiri ya Umungu ni sambamba na vitu ama sheria kubwakubwa!.

hakuna cha tofauti hapo hizo ni kama zilezile hekaya za vitabu vya dini!

Mi sidhani kama hata Mungu (kama yupo) analugha rahisi hivyo!,halafu kwa upeo wake kujihusisha sana na matendo ya binadamu ni kumshusha sana!,mara atatuhukumu kwa dhambi zetu!..😂

itakuwa amekosa kazi za kufanya ye alipoumba akabalansi akamaliza so ameshaweka vitu kwa uwiano anajua hata mdhambike vipi hamtamuharibia mambo aliyoyaweka! by the way alietengeneza kitu ndie anaekihitaji sasa nashangaa binadamu sijui kwanini mnamuhutaji huyo Mungu! mpaka hapo tunaonyesha tumeshafeli kwenye kumjua tu huyo Mungu!
 
ukutaka kujua hilo historia halisisimui linazungumzia mambo yaleyale yakibinadamu!,ndoa,vita,utumwa na uzazi!!.
kwa mimi binafsi nikianza kuzungumzia mambo ya kimungu siwezi kugusia vitu vidogo vidogo kama hivyo!,maana tafsiri ya Umungu ni sambamba na vitu ama sheria kubwakubwa!..
hakuna cha tofauti hapo hizo ni kama zilezile hekaya za vitabu vya dini!..

Mi sidhani kama hata Mungu (kama yupo) analugha rahisi hivyo!,halafu kwa upeo wake kujihusisha sana na matendo ya binadamu ni kumshusha sana!,mara atatuhukumu kwa dhambi zetu!..
itakuwa amekosa kazi za kufanya ye alipoumba akabalansi akamaliza so ameshaweka vitu kwa uwiano anajua hata mdhambike vipi hamtamuharibia mambo aliyoyaweka! by the way alietengeneza kitu ndie anaekihitaji sasa nashangaa binadamu sijui kwanini mnamuhutaji huyo Mungu! mpaka hapo tunaonyesha tumeshafeli kwenye kumjua tu huyo Mungu!
Hii ndiyo point muhimu

By the way alietengeneza kitu ndie anaekihitaji sasa nashangaa binadamu sijui kwanini mnamuhutaji huyo Mungu! mpaka hapo tunaonyesha tumeshafeli kwenye kumjua tu huyo Mungu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom