Afrika ndiyo kinara wa kufanya kazi ngumu lakini kisukari ni tishio je kazi ngumu sio mbadala wa mazoezi?

Kwangu kazi ngumu naweza kusema ni mbadala wa mazoezi. Changamoto kubwa huku kwetu ulaji wetu ni mbovu hauzingatii afya.

Mazoezi/kazi ngumu iendane na msosi mzuri(mahitaji ya mwili)
 
Basi ni kijijini kwelikweli.
Miji iliyochangamka ndo ina hii changamoto, sasa huko ndichi hata kiepe ni anasa, chakula kila nyumba inajipikia chake local kabisa.

Maduka yanauza viberiti na chumvi, tatizo ni maskini wa mijini mkuu, tuvitu vitu twa barabarani ni sh 100, 200 mpaka buku, unapata shingo miguu kwa jero + ndizi za kukaanga.
Population kubwa ya Afrika iko vijijini siyo "miji iliyochangamka." na hata hiyo miji unayosema utakuta watua wanshindia chips, mayai, soda na kijiweni; utakosa vipi kisukari kama maisha yako ndiyo hayo?
 
Mkuu, naomba uhusiano wa kisukari na mazoezi. Kuna kitu nataka kujifunza.
assume umekula ubwabwa wako ama ugali wa kutosha, unapoenda kufanya mazoezi ile energy ya carbohydrate itatumika na Mwili hautatengeneza mafuta ya ziada.

ILa umepiga ubwabwa wako halafu unalala ama umetulia ile energy haitumiki na ibabadilishwa kuwa fat, hii fat ina ongeza resistance ya insulin kwenye Mwili, kunapokua na resistance ya insulin cell za Mwili hazi absorb sukari na kupelekea sukari kusafiri kwenye mishipa ya damu hivyo kupata kisukari.

Sio Tu wanga, mafuta, vyakula vya viwandani na junks food nyingi zipo kundi hili.
 
Kwa sababu sukari inalundikana ndani ya damu kupitia kiasi kwa hiyo ile mishipa ya damu diameter yake inakuwa ndogo (narrowing of blood vessels) ,pia inapelekea mishipa ya damu kukakamaa hivyo inashindwa kusinyaa na kutanuka.

Uharibifu huu wa mishipa ya damu unatokea mwili mzima kwa hiyo kuna kuwa na poor blood flow , na ili mtu aweze kusimamisha lazima kuwe mtiriko mzuri wa damu kwenye uume, mtiririko mbovu wa damu unapeleka mtu kushindwa kusimamisha kwa sababu kuu ndio hiyo niliyokwambia kuna kuwa na damage ya blood vessela hivyo inapelekea kuwa na poor blood flow.

Blood vessels za kwenye macho pia zikiharibika zinapelekea upofu wa macho (diabetic retinopathy).


Kwa kifupi kisukari kina madhara mengi mno na kinapelekea kuua ogani nyingi kufeli na pia kina shusha Kinga ya mwili ndio maana mtu akipata kidonda kupona inakuwa ni tabu mno kwa sababu ya hiyo immunodeficiency.
Shukrani kwa maelezo yako mujarabu. Kwenye hiyo paragraph ya mwisho, umenipa jibu la swali ambalo nilikuwa nimejiandaa kuliuliza. Thanks Chief 👊
 
Hizi wanga wanazozidis ndo vyakula vya bei chee.
Matunda ni ya wenye kipato cha ziada, matunda kibongo bongo hasa mkoa uliojaa mafukara kama dsm, matunda ni anasa labda uwe karibu na soko au unfanya kazi humo sokoni.

Chipsi hata za buku unapata, nguna buku, wali buku, pilau buku.
Matunda bei imechangamka, mtu wa kipato kidogo hata mtumishi anaelipwa below 500k sio rahisi kuafford mlo na tunda kwa mwezi mzima. Tunda na msosi bei inaweza kulingana si hasara hiyo .

Tatizo ni kweli ni elimu ya lishe ila hata hiyo elimu ikitolewa na kueleweka ndo italeta shida zaidi ya vitu kupanda bei, na pia wadau kutoafford.

Tuendako hali ni mbaya zaidi ya hii.
Kweli kabisa mkuu hii nchi kuna mda nikiiwaza naona kabisa ni kama sisi kwa dunia ni zile grade za mwisho mwisho
 
Kweli kabisa mkuu hii nchi kuna mda nikiiwaza naona kabisa ni kama sisi kwa dunia ni zile grade za mwisho mwisho
Ndo ivo, yaani huku ukiumwa kwa wengine ni kicheko maana watakuvuna vilivyo.

Ndo serikali ihamasishe tule matunda, dadeki ndizi utanunua buku, ila mind you mkulima wa hiyo ndizi anaweza pata sh 50, mnyororo wa ulaji hapo kati ndo balaa.
 
Afrika watu wanafanya kazi ngumu sana lakini bado kisukari ni tishio, nilikuwa Dodoma kukawa na upimaji wa Bure Cha kushangaza vijana below 40 wengi tu wana sukari.

Nikazama gugo kudadisi statistics zinatisha watu jamii ya black race wapo kwenye risky ya kupata kisukari ukilinganisha na wazungu.

Nikasikitika sana kwani nilijua kazi ngumu ni mbadala wa mazoezi.

Hizi data kwa picha zunainesha Tanzania ni namba 4 kwa wingi wa wa wagonjwa wa kisukari Africa.
Kwanza ni kujua kisukari kinaletwa na nini nipo jibu linapatikana
 
Mwezi wa kwanza tumemzika dogo wa 1998 , amekufa kwa kisukari kabla ya hapo kimemsumbua miaka 2 nyuma.
 
Life style ndo inachangia hizo zingine zinaweza kuwa sababu za kijenetiki.

Unaweza kuwa hard worker Ila lifestyle ikakuangusha na hii ndo huwapata Africa.

MTU mweusi neno kiasi huwa halielewi

Kama ni kula anakomoa
Ngono anakomoa
Kila kitu anakomoa so hawezi kuwa safe .
Mkuuu, umemaliza. Ngozi nyeusi na kiasi ni mbingu na ardhi
 
Kwanza ni kujua kisukari kinaletwa na nini nipo jibu linapatikana
Nimeona wachangiaj wengi wamejitaid kuelezea kuhusu kisukari ila mim nafikir kisukari kinasababishwa na hitilafu kwenye kongosho ,pia na ulaj mbovu unakuta mtu anakula vyakula ambavyo sio rafiki sana Kwa mfano anakula mara Kwa mara nyama nyekundu,soda Kwa wingi,chips ,bia na vinywaj vyenye sukar sana,kumbuka mtu huyu anapofanya hivyo hata kama atafanya mazoez inakuwa Kaz Bure,pia nimeona Kuna tiba yenye seli(stem cell) imewasaidia watu wengi wenye changamoto ya kisukari ikiwemo kubust immunity na kutibu hitilafu ya kongosho,na nimeona wengi wameondokana na maradhi haya hatari maana kisukari ni ndg yake na presha,na utakuta mtu mwenye presha (high blood pressure)yupo kwenye risk ya kupata kisukari.Kwa ufupi haya maradhi ni hatari na yanaua haraka sana,yanasababisha upofu ,uanith ,uharibifu wa Figo ,in na viungo vingine vya mwili,kinachotakiwa ni kuchukua hatua haraka sana
 
1. Kazi ngumu si mbadala wa mazoezi. Mazoezi kama kukimbia yanawezesha ufumiaji na mzunguko wa damu, pia kuna mazoezi ya kunyoosha viungo.
2. Mchango wa sumu za mashambani na anti-biotics ni mkubwa sana kuelekea kudorora kwa afya.
 
Miaka ya 90, kisukari ulijulikana ni ugonjwa special wa matajiri. Wastaafu serikalini,wafanyabiashara matajiri ( wanaokula kiulaini) nk nk.

Uswahilini, na maskini, wenye kupata chakula Kwa taabu, wakulima vijijini,kunywa soda ilikuwa Hadi sikukuu, hawakuwa na tatizo la sukari.

Mimi,nahusisha kisukari mojakwa Moja na ulaji wa vyakula vya mafuta na kula kupitiliza, unene na kutofanya kazi ngumu za Kutoka JASHO.

Ni hayo tu.
 
Mkuu, naomba uhusiano wa kisukari na mazoezi. Kuna kitu nataka kujifunza.
Ukifanya mazoezini au kazi ngumu unaunguza au kutumia sukari nyingi kama energy.
Ukiwa unakula tu na haufanyi mazoezini hii sukari inalundikana mwilini na ndo hiyo huleta ugonjwa
Bush dokta kwa msaada ya gugo
 
Mnazunguka zunguka, mara carbihydrate mala life style ..

Ishu ni moja tuuu.

Regulation of sugar kwenye blood, hii ni kazi ya Insulin.
ikiwa na afya hii kula ulavyo mwil una in-built capability ya ku regulate sukari kwa Insulin.

Iki feli hii hata uwe unakunywa maji tu,kisukari kitakuondoa
 
Kisukari na kudindisha vinahusiana vipi Mzee? Au huo upofu?
Sukari ina uhusiano mkubwa sana na upofu pamoja na urijali,
Huwa inaua mishipa midogo ya damu na moja ya mishipa hiyo ni ilie inayosimamisha uume pamoja na macho
 
Mfumo wa maisha maana afrika watu wanapenda sana vitu vitam
Sio kweli hakuja watu wanakula vitu vyenye sukari kama wazungu, kinachowasaidia wazungu ni huduma za afya zipo bora pia tamaduni ya upimaji wa afya mara kwa mara
 
Back
Top Bottom