Afrika ndiyo kinara wa kufanya kazi ngumu lakini kisukari ni tishio je kazi ngumu sio mbadala wa mazoezi?

Sema vyakula vya wanga mkuu. Sisi tunatumia sana nafaka zenye carbohydrates sana kama mahindi na mchele na ngano. Hili lina mchango mkubwa sana kwenye gonjwa la sukari.
Hii ni irrelevant kabisa, Mababu, Mabibi na Wazazi wetu waligonga sana vyakula hivyo ila viwango vya sukari vilikuwa hafifu, mivyakula ya viwandani, soda na bia ndiyo inachangia sana ila si vyakula asilia.

Pia bado uwiano wa kazi ngumu za miaka ya 1900 - 1980 walikuwa wanafanya mazoezi kila siku kutembea na kuendesha baiskeli umbali wa KM 10 - 30 mbali na kazi ngumu pekee walizokuwa wakifanya, huwezi kuwalinganisha na sisi ambao magari yamerahisisha usafiri.

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
 
Afrika watu wanafanya kazi ngumu sana lakini bado kisukari ni tishio, nilikuwa Dodoma kukawa na upimaji wa Bure Cha kushangaza vijana below 40 wengi tu wana sukari.

Nikazama gugo kudadisi statistics zinatisha watu jamii ya black race wapo kwenye risky ya kupata kisukari ukilinganisha na wazungu.

Nikasikitika sana kwani nilijua kazi ngumu ni mbadala wa mazoezi.

Hizi data kwa picha zunainesha Tanzania ni namba 4 kwa wingi wa wa wagonjwa wa kisukari Africa.
Kuna sababu nyingi tu za kisukari .

Mfano kisukari aina ya kwanza ambacho kinatokea kwa sababu ya hypersensitivity kinapelekea kuua beta cells ambazo zinahusika na utengenezwaji wa insulin ,kwa hiyo mwili unakosa insulin kwa ajili ya kurekebisha kiwango cha sukari katika damu , huyu mtu atachoma sindano za insulin miaka yake yote mpaka anaingia kaburini . Kwa hiyo hata afanye mazoezi vipi hawezi kukiondoa.

Kisukari aina ya pili ndio hicho kinachotokana na insensitivity ya insulin receptors at least hiki ukikiwahi unaweza ukapona kwa ku control diet na exercise (Zingatia diet na exercise ) ,kama unafanya mazoezi ila mlo wako wa hovyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
 
Mkuu, naomba uhusiano wa kisukari na mazoezi. Kuna kitu nataka kujifunza.
Mafuta yanachochea insulin receptors kuwa less sensitive na insulin.

Insulin ndio inayo control kiwango cha sukari kwenye damu.

Sasa ukifanya mazoezi unachoma mafuta na kusaidia insulin receptors kuwa sensitive na insulin ,hivyo insulin inakuwa na uwezo wa ku bind kwenye receptors zake na kufanya kazi yake ya ku control sukari kwenye damu.
 
Shukrani sana Mzee wa chai. Maelezo yamenyooka. 🙏🙏
 
Shukrani sana Mzee wa chai. Maelezo yamenyooka. 🙏🙏
Cha kuongezea ni kwamba ukiona dalili za kisukari mfano kusikia kiu mara kwa mara, kusikia njaa, kusikia mkojo na hali ya kupoteza uzito na kuchoka choka , ni heri uende kutafuta tiba mapema.

Kisukari kikikomaa madhara yake ni makubwa mno ikiwemo kuwa hanithi na upofu.
 
Elimu kuhusiana na lishe ndio bado nijanga kubwa sana tunafanya kazi ngumu sawa ila lishe mbovu ndio inapelekea sugar
 
Nyie madokta hebu toeni elimu, humu kila mchangiaji anasema lake.
Mara mazoezi, mtindo wa maisha, wanga sijui, wali mpaka ugali umetajwa.
 
Afrika watu wanafanya kazi ngumu sana lakini bado kisukari ni tishio, nilikuwa Dodoma kukawa na upimaji wa Bure Cha kushangaza vijana below 40 wengi tu wana sukari.

Nikazama gugo kudadisi statistics zinatisha watu jamii ya black race wapo kwenye risky ya kupata kisukari ukilinganisha na wazungu.

Nikasikitika sana kwani nilijua kazi ngumu ni mbadala wa mazoezi.

Hizi data kwa picha zunainesha Tanzania ni namba 4 kwa wingi wa wa wagonjwa wa kisukari Africa.
Mkuu sawa tunafanya kazi ngumu...but it's gonna end kwenye uchumi... imagine huyo mmbeba lumbesa analipwa 1000 mfano kwa gunia then after summation hiyo ndio itumike kula itumike on everything na bado haya magonjwa some of them ni inheritable mwisho wa siku matibabu yake pia kwa hali zetu kua afford ni ngumu .. tofauti na wenzetu wako mbali ..they know the effects but they also know how to manage the situations iwe ni afya elimu etc.
 
Afrika siyo kinara wa kisukari; watu wenye visukari wengi ni wale wenye maisha mazuri wa mijini tu. Kule Uswazi na vijijini hakuka kisukari
 
Hizi wanga wanazozidis ndo vyakula vya bei chee.
Matunda ni ya wenye kipato cha ziada, matunda kibongo bongo hasa mkoa uliojaa mafukara kama dsm, matunda ni anasa labda uwe karibu na soko au unfanya kazi humo sokoni.

Chipsi hata za buku unapata, nguna buku, wali buku, pilau buku.
Matunda bei imechangamka, mtu wa kipato kidogo hata mtumishi anaelipwa below 500k sio rahisi kuafford mlo na tunda kwa mwezi mzima. Tunda na msosi bei inaweza kulingana si hasara hiyo 😂.

Tatizo ni kweli ni elimu ya lishe ila hata hiyo elimu ikitolewa na kueleweka ndo italeta shida zaidi ya vitu kupanda bei, na pia wadau kutoafford.

Tuendako hali ni mbaya zaidi ya hii.
 
Afrika siyo kinara wa kisukari; watu wenye visukari wengi ni wale wenye maisha mazuri wa mijini tu. Kule Uswazi na vijijini hakuka kisukari
Unajidanganya mkuu.
Magonjwa ya kitajiri sasa hivi wanaumea hadi maskini.

Zamani nilikua naamini presha na hizo sukari ni magonjwa ya kidosi.
Malaria, kipindupindu, typhoid nk ni magonjwa ya walalahoi.
Ila hapo kwa walalahoi hayo ni kweli ni magonjwa yao, saivi wameyachukua na yale ya wados.
 
Siamini, kwani kijijini kwetu hatujawahi ksuikia ugonjwa wa kisukari. Maisha yangu yote, kuna mtu mmoja tu ndiye alikutwa na kisukari na hicho hakikuwa Type 2 bali ilikuwa Type 1.

Kisukari husababishwa na mambo mawili tu: mlo na mazoezi. Milo mibovu kama chips mayai na soda bila mazoezi huleta kisukari haraka sana.
 
Siamini, kwani kijijini kwetu hatujawahi ksuikia ugonjwa wa kisukari. Maisha yangub yote, kuna mtu mmoja tu ndiye alikutwa na kisukari na hicho hakikuwa Type 2 bali ilikuwa Type 1.

Kiuskari husababishwa na mambo mawili tu: Mlo na mazoezi. Milo mibovuo bila mazoezi
Basi ni kijijini kwelikweli.
Miji iliyochangamka ndo ina hii changamoto, sasa huko ndichi hata kiepe ni anasa, chakula kila nyumba inajipikia chake local kabisa.

Maduka yanauza viberiti na chumvi, tatizo ni maskini wa mijini mkuu, tuvitu vitu twa barabarani ni sh 100, 200 mpaka buku, unapata shingo miguu kwa jero + ndizi za kukaanga.
 
Kisukari na kudindisha vinahusiana vipi Mzee? Au huo upofu?
Kwa sababu sukari inalundikana ndani ya damu kupitia kiasi kwa hiyo ile mishipa ya damu diameter yake inakuwa ndogo (narrowing of blood vessels) ,pia inapelekea mishipa ya damu kukakamaa hivyo inashindwa kusinyaa na kutanuka.

Uharibifu huu wa mishipa ya damu unatokea mwili mzima kwa hiyo kuna kuwa na poor blood flow , na ili mtu aweze kusimamisha lazima kuwe mtiriko mzuri wa damu kwenye uume, mtiririko mbovu wa damu unapeleka mtu kushindwa kusimamisha kwa sababu kuu ndio hiyo niliyokwambia kuna kuwa na damage ya blood vessela hivyo inapelekea kuwa na poor blood flow.

Blood vessels za kwenye macho pia zikiharibika zinapelekea upofu wa macho (diabetic retinopathy).

Kwa kifupi kisukari kina madhara mengi mno na kinapelekea kuua ogani nyingi kufeli na pia kina shusha Kinga ya mwili ndio maana mtu akipata kidonda kupona inakuwa ni tabu mno kwa sababu ya hiyo immunodeficiency.
 
Mbali na yote yaliozungumzwa, intermittent fasting ni muhimu sana mno kwenye kujikinga na kisukari.

Pia kwa wanaotetea kwamba wazee wetu walikula wanga iziizi kwanini wao sukari hawana, jibu ni kwamba wao walifanya kazi nyingi za nguvu nguvu zilizosababisha matumizi makubwa ya calories zilizozalishwa na miili yao, pili hizo wanga zao waluzila zikiwa na kiasi kikubwa sana cha fibres(naweza kusema nyuzinyuzi zile), sio wanga zetu hizi, zingine zimekobolewa sana, matunda sijui tunasagasaga na kuyala kama juisi (tunapoteza fibres kiasi kikubwa)
 
Back
Top Bottom