Afrika ndiyo kinara wa kufanya kazi ngumu lakini kisukari ni tishio je kazi ngumu sio mbadala wa mazoezi?

Sema vyakula vya wanga mkuu. Sisi tunatumia sana nafaka zenye carbohydrates sana kama mahindi na mchele na ngano. Hili lina mchango mkubwa sana kwenye gonjwa la sukari.
Mbona wazungu wanakula mikate na tambi sana,sio wanga huo?
 
Sukari ina uhusiano mkubwa sana na upofu pamoja na urijali,
Huwa inaua mishipa midogo ya damu na moja ya mishipa hiyo ni ilie inayosimamisha uume pamoja na macho
Shukrani chief👊
 
Ukifanya mazoezini au kazi ngumu unaunguza au kutumia sukari nyingi kama energy.
Ukiwa unakula tu na haufanyi mazoezini hii sukari inalundikana mwilini na ndo hiyo huleta ugonjwa
Bush dokta kwa msaada ya gugo
Asante sana bush dokta from gugo univasiti. Maelezo yanaeleweka 😅
 
Asante sana bush dokta from gugo univasiti. Maelezo yanaeleweka 😅
Ogopa sana sukari ikishafikia kwenye kuleta ukhanithi!!!
Mzigo unaona kabisa huu hapa!! Halafu chombo haisimami!!! yani kama hakuna kilichotokea 🙂 unaeza kulia!!
 
Umeongelea upande mmoja ukaacha mwingine, ni kweli insulin inatumika ku regulate glucose, lakini inategemea wingi wa glucose, ulaji mbaya wa chakula husababisa glucose kuwa nyingi kuliko uwezo wa insulin, (insulin resistance,) na hapa ndo tatizo la sukari huanzia. Na ndio hiyo. Huitwa type 2 diabetes, insulin inakuwepo lakini inakuwa imezidiwa na wingi wa glucose.
Mnazunguka zunguka, mara carbihydrate mala life style ..

Ishu ni moja tuuu.

Regulation of sugar kwenye blood, hii ni kazi ya Insulin.
ikiwa na afya hii kula ulavyo mwil una in-built capability ya ku regulate sukari kwa Insulin.

Iki feli hii hata uwe unakunywa maji tu,kisukari kitakuondoa
ha
 
Afrika watu wanafanya kazi ngumu sana lakini bado kisukari ni tishio, nilikuwa Dodoma kukawa na upimaji wa Bure Cha kushangaza vijana below 40 wengi tu wana sukari.

Nikazama gugo kudadisi statistics zinatisha watu jamii ya black race wapo kwenye risky ya kupata kisukari ukilinganisha na wazungu.

Nikasikitika sana kwani nilijua kazi ngumu ni mbadala wa mazoezi.

Hizi data kwa picha zunainesha Tanzania ni namba 4 kwa wingi wa wa wagonjwa wa kisukari Africa.
Nchi Ina watu milioni 55! Unapima watu 200 wa mjini! Unasema kisukari kinatisha bongo!
 
Sukari inayosababishwa na hitilafu ya kongosho siyo maarufu sana huku kwetu, (type 1) huwa inatokeaga tu kongosho haitoi insulin au ikazidisha insulin, type 1 diabetes sio lifestyle disease! Ni ugonjwa sana sana wa kurithi( genetic)
Inayosumbua sasa Africa ni type 2 diabetes hii sasa ni lifestyle disease.. Kongosho inatoa insulin ila sukari inakuwa nyingi mwilini kuliko dose ya insulin.
Nimeona wachangiaj wengi wamejitaid kuelezea kuhusu kisukari ila mim nafikir kisukari kinasababishwa na hitilafu kwenye kongosho ,pia na ulaj mbovu unakuta mtu anakula vyakula ambavyo sio rafiki sana Kwa mfano anakula mara Kwa mara nyama nyekundu,soda Kwa wingi,chips ,bia na vinywaj vyenye sukar sana,kumbuka mtu huyu anapofanya hivyo hata kama atafanya mazoez inakuwa Kaz Bure,pia nimeona Kuna tiba yenye seli(stem cell) imewasaidia watu wengi wenye changamoto ya kisukari ikiwemo kubust immunity na kutibu hitilafu ya kongosho,na nimeona wengi wameondokana na maradhi haya hatari maana kisukari ni ndg yake na presha,na utakuta mtu mwenye presha (high blood pressure)yupo kwenye risk ya kupata kisukari.Kwa ufupi haya maradhi ni hatari na yanaua haraka sana,yanasababisha upofu ,uanith ,uharibifu wa Figo ,in na viungo vingine vya mwili,kinachotakiwa ni kuchukua hatua haraka sana
 
Afrika watu wanafanya kazi ngumu sana lakini bado kisukari ni tishio, nilikuwa Dodoma kukawa na upimaji wa Bure Cha kushangaza vijana below 40 wengi tu wana sukari.

Nikazama gugo kudadisi statistics zinatisha watu jamii ya black race wapo kwenye risky ya kupata kisukari ukilinganisha na wazungu.

Nikasikitika sana kwani nilijua kazi ngumu ni mbadala wa mazoezi.

Hizi data kwa picha zunainesha Tanzania ni namba 4 kwa wingi wa wa wagonjwa wa kisukari Africa.
Hili la kusema Afrika watu ndiyo hufanya kazi ngumu zaidi una uhakika nalo? Siyo kama zile zile story za kusema wanaokula ugali ndiyo wenye nguvu na wazungu ni legelege? Mimi nadhani Afrika ndiyo yenye watu wavivu zaidi. Kama umewahi kufika Ulaya au nchi yoyote iliyoendelea nadhani utakubaliana na mimi wanafanya kazi mara kumi kuliko sisi. Huku kwetu kazi ngumu wanafanya watu wa vijijini ambako hakuna vyakula na huduma za afya za kutosha. Mjini watu wanaishi maisha ya hatari sana. Wengi kila siku jioni wanakwenda bar kunywa na kula na maofisini hata kukoroga chai wanafanyiwa.
 
Nimeona wachangiaj wengi wamejitaid kuelezea kuhusu kisukari ila mim nafikir kisukari kinasababishwa na hitilafu kwenye kongosho ,pia na ulaj mbovu unakuta mtu anakula vyakula ambavyo sio rafiki sana Kwa mfano anakula mara Kwa mara nyama nyekundu,soda Kwa wingi,chips ,bia na vinywaj vyenye sukar sana,kumbuka mtu huyu anapofanya hivyo hata kama atafanya mazoez inakuwa Kaz Bure,pia nimeona Kuna tiba yenye seli(stem cell) imewasaidia watu wengi wenye changamoto ya kisukari ikiwemo kubust immunity na kutibu hitilafu ya kongosho,na nimeona wengi wameondokana na maradhi haya hatari maana kisukari ni ndg yake na presha,na utakuta mtu mwenye presha (high blood pressure)yupo kwenye risk ya kupata kisukari.Kwa ufupi haya maradhi ni hatari na yanaua haraka sana,yanasababisha upofu ,uanith ,uharibifu wa Figo ,in na viungo vingine vya mwili,kinachotakiwa ni kuchukua hatua haraka sana
Nakumbuka Mzee wangu katika ukuaji wangu alikuwa ananizuia kunywa maji huku nakula kuwa italeta kisukari sikuwa na uhakika ila ilikuwa fact sana kwangu katika digestion system
 
Mostly vyakula tunakula na kunywa ni hormonal suppressor so unaweza ukafanya mazoezi but hormones sio balanced hapo sasa sukari inaingia
 
Comments za washauri wengi ni kama hawana mtindo mbaya wa maisha. Kitu ambacho si kweli.

Magonjwa mengine yapo kwenye vinasaba, magonjwa hayo huwa yanasubiri visababishi tu.

Wengine tunakunywa pombe monday to sunday, usizungumzie mitoko official ya weekend ambapo mtakunywa hadi asubuhi.
Vyakula ni ugali, nyama choma, wali, tunakunywa sana soda na tukichelewa kula chips na juice au soda inahusika.

Haya mambo wakati mwingine ni Mungu tu lakini pia familia unayotokea, ninavyoona kama mzazi wako alishakuwa na kisukari ni vyema kujiangalia hasa katika ulaji.

Kubadili lifestyle inataka moyo sana na kujitoa lakini hamna namna.

Wanga ndio maisha yetu, familia ina watoto 8, baba kajitafuta uwezo wake ni kununua unga wa mahindi watoto wale ndicho chakula bei nafuu.

Umasikini na kisukari vinapendana sana.

Chanzo cha rate kubwa ya kisukari ni umasikini hakuna lingine.
 
Back
Top Bottom