Afrika ndiyo kinara wa kufanya kazi ngumu lakini kisukari ni tishio je kazi ngumu sio mbadala wa mazoezi?

Afrika watu wanafanya kazi ngumu sana lakini bado kisukari ni tishio, nilikuwa Dodoma kukawa na upimaji wa Bure Cha kushangaza vijana below 40 wengi tu wana sukari...
Si wote wanafanya kazi ngumu, hasa mijini. Wanaokuwa maofisini hawatumii misuli kufanya kazi. Wakiwa nyumbani wanakaa, wakitoka nje wanaingia kwenye magari kukaa, na wakifika ofisini wanakaa, tena muda mwingi.

Kuna vijana wanashinda vijiweni bila kazi yoyote na kujiingiza kwenye ulevi hatarishi iwe mijini au vijijini. Aina ya maisha tunayoishi yamebadilika sana!

Aidha, aina ya vyakula na vinywaji vingi ni hatarishi, ikiwemo mafuta, chips, na nyama za ufugaji wa kisasa kwa madawa mengi. Mwili unatiwa sumu nyingi kutokana na kuacha vyakula na vinywaji asilia. Lakini pia kuna kisukari cha kurithi.
 
Si wote wanafanya kazi ngumu, hasa mijini. Wanaokuwa maofisini hawatumii misuli kufanya kazi. Wakiwa nyumbani wanakaa, wakitoka nje wanaingia kwenye gari kukaa, na wakifika ofisini wanakaa, tena muda mwingi...
Na hii ndiyo sababu kubwa hasa ya vijana wengi kuwa na kisukari. Asilimia ndogo sana ambayo inapata kisukari cha kurithi, lakini asilimia kubwa ni ulaji wa hivyo vitu ulivyovianisha. Kuna uhusiano mkubwa sana wa mlundikano wa mafuta mwilini na kisukari aina ya pili(type 2 diabate).
 
Mkuu, naomba uhusiano wa kisukari na mazoezi. Kuna kitu nataka kujifunza.
Unaweza kufanya mazoezi na bado ukaugua kisukari kutokana na aina ya vyakula na vinywaji unavyotumia.

Fanya mazoezi, kula chakula asilia na kunywa kinywaji asilia, hususan maji safi na salama na matunda au juisi yake asilia.

Na zaidi sana, wakulima tuanze kulima Kilimo-afya (Agrihealth) na si kilimo-biashara (Agribusiness), chenye kemikali hatarishi kwa ardhi, mazao na miili yetu.
 
Mkuu.

Sukari haisababishwi na kutofanya mazoezi au kufanya mazoezi. Uhusiano wa Sukari na mazoezi ni mdogo sana.

Sukari inaletwa sana na LifeStyle (ULAJI WA VYAKULA NA VINYWAJI). Kuna aina ya maisha ukiishi, hata kama unalala GYM bado Sukari unaweza ukapata. Na pia kuna sababu nyingine zinazoweza pelekea kupata sukari, ila sana ni MTINDO WA MAISHA.
Sahihi kabisa
 
Na hii ndiyo sababu kubwa hasa ya vijana wengi kuwa na kisukari.Asilimia ndogo sana ambayo inapata kisukari cha kurithi,lakini asilimia kubwa ni ulaji wa hivyo vitu ulivyovianisha.Kuna uhusiano mkubwa sana wa mlundikano wa mafuta mwilini na kisukari aina ya pili(type 2 diabate).
Ni kweli
 
Mkuu, naomba uhusiano wa kisukari na mazoezi. Kuna kitu nataka kujifunza.
Inaaminika kadiri mtu anapofanya kazi ngumu sana matumizi ya sukari nayo huwa makubwa, nadhani huo ndo msingi wa mleta uzi, rejea tafakuri ya Pro Janabi kwamba kama unatoka clods FM kwenda Escape one huna haja ya kujaza mafuta full tank
 
Ulaji wa vyakula vya mafuta kupindukia,jambo linalosababisha mafuta mengi mwilini na unene kupindukia.

Mambo haya huambatana na ugonjwa wa sukari ambao zamani uliwaandama watu wenye umri angalau miaka 50.

Lakini siku hizi mtu anakuwa na unene uliozidi akiwa na miaka michache.
Mafuta vs Kisukari?
 
Back
Top Bottom