Japo kazi ya upinzani ni kupinga, lakini sio kupinga kila kitu. Kwenye maslahi ya taifa, tutangulize utaifa, tuwe wamoja, wakweli na tusipotoshe

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,615
113,834
Wanabodi,

Huu ni muswada wa makala ya gazeti.

Nimepata fursa kuendeleza zile makala zangu za "Kwa Maslahi Ya Taifa", ambazo ni makala elimishi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa lengo la kulisaidia taifa letu lisonge mbele. Makala ya leo inazungumzia
kazi ya vyama vya upinzani ni kupinga, lakini sio kupinga tuu kila kitu, kunapotokea jambo kubwa lenye maslahi ya taifa, hapa Watanzania wote tunapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja, wakiwemo wapinzani, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kuwa wakweli, tusipotoshe bali tulisaidie taifa letu kwa michango ya kujenga na kusaidia, na ikitokea serikali iliyoko madarakani inakosea katika jambo la maslahi kwa taifa, serikali inakosolewa constructively kwa kupewa mapendekezo mbadala na sio kwa kubezwa, kutukanwa na kusakamwa.

Rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano alipoingia tuu madarakani, alitangaza vita nyingi nyingi ikiwemo vita ya dhidi ya rushwa, ufisadi na ubadhirifu kwa tumbua tumbua. Vita dhidi ya ujinga kwa kutoa elimu bure, kuongeza mikopo ya elimu ya juu na kujenga mashule na kuongeza waalimu. Vita dhidi ya maradhi kwa kuongeza bajeti ya afya, kujenga vituo vya afya, zahanati, mahospitali, upatikanaji na usambazaji wa madawa na kuongeza watumishi wa afya. Vita dhidi ya uvivu na uzururaji kwa falsafa yake ya hapa kazi tuu kwa kusisitiza kila mtu afanye kazi. Hata tangazo la kupiga marufuku mikutano ya siasa na maandamano, lengo lake ni zuri, uchaguzi umepita, watu wasikalie tuu kupiga siasa na uzururaji wa maandamano na badala yake watu wafanye kazi.

Kati ya vita zote ambazo Rais Magufuli na serikali yake ameitangaza, vita ngumu ni vita ya kiuchumi ili kupambana na adui umasikini, hii ndio vita kubwa zaidi na ngumu zaidi kuliko vita zote. Rais Magufuli ameigawanya vita hii katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo, kujenga Tanzania ya Viwanda, kujenga miondombinu wezeshi, ndio maana tunashuhudia ndege za ATCL zinapaa duniani kote, meli zinajengwa, miradi mikubwa ya reli ya SGR, mabarabara, flyovers, umeme wa Stigler nakadhalika.
Hii vita dhidi ya kulinda rasilimali za taifa ndio vita ngumu kuliko vita zote kwa sababu inahusisha na kupambana na maadui wenye nguvu wakiwemo mabepari wakubwa, makabaila na mabeberu kupitia mashirika makubwa ya kimataifa.
Katika kupambana na vita kwa sekta ya madini, rais Magufuli akasitisha usafirishaji wa mchanga wa dhahabu kwa jina la makinikia, mchanga huo ni wa kampuni ya Acacia ambayo ni kampuni tanzu ya Barrick ya Canada. Tukatunga sheria mpya ya madini kuwa kuanzia sasa, TanzaniaTanzania itamiliki asilimia 16% ya rasilimali zote za ardhini. Hatua hii Tanzania kama nchi tukapata misukosuko ya kutingishwa tulegeze msimamo, ikiwemo ndege zetu kuzuiwa huko Canada, tukapambana hadi ndege zikatoka.

Katika kuutatua mgogoro wa makinikia serikali yetu ikafanya mazungumzo na Barrick yaliyodumu kwa zaidi ya miaka miwili ambapo ni wiki iliyopita tuu ndipo mgogoro huu umemalizika rasmi kwa Barrick kushika hatumu za Acacia hivyo sasa makubaliano yatasainiwa wakati wowote.Mazungumzo haya yalikuwa siri na mkataba pia ulikuwa siri lakini kufuatia wenzetu wazungu kuwa wazi zaidi, katika mauziano ya Barrick na Acacia, mkataba huu ukawekwa wazi na kuzua mijadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii ukiwemo mtandao unaoongoza kwa mijadala, mtandao wa Jamii Forums.

Katika kuujadili mkataba huo baadhi ya wanasiasa wa kambi ya upinzani waki utumia mkataba huo kujipatia umaarufu na kujijenga kisiasa kwa kutumia baadhi ya hoja za ukweli, kuchanganya na uongo na hata kutumia upotoshaji wa makusudi kama kuaminisha watu kuwa huu mkataba tayari umeisha sainiwa kitu ambacho sii kweli bali ni upotoshaji wa makusudi au wa bahati mbaya kutokana na kutokutafsiri vizuri lugha ya Malikia.

Wapenzi wasomaji wangu kwa vile mkataba huu ni wa lugha ya Kiingereza, nitalazimika kutumia baadhi ya maneno ya Kiingereza kwa ajili ya uhalisia

Mhe. Zitto alipoona ile Draft Agreement ikielezwa kuwa imekuwa initialed, akaibuka na upotoshaji kuwa huo mkataba tayari umesainiwa!, kwakwe neno draft agreement amelitafsiri kuwa ndio mkataba halisi, na neno kuwa initialed kwake ametafsiri kuwa huku ndiko kusainiwa kwenyewe!, hizi lugha za watu jamani, zisitufanye kuonekama waongo na wapotoshaji, tuwe wakweli daima, tell the truth and the truth will set you free!.

Mimi niliandika bandiko na kuyasema mazuri ya mkataba huo ni pamoja na
  1. Sasa mgogoro wa Acacia na serikali yetu, umemalizika rasmi kwa sababu sasa Acacia doesnt exist anymore.
  2. Migodi yote mitatu iliyokuwa chini ya Acacia, sasa itakuwa chini ya Barrick
  3. Yale makubaliano ya serikali yetu sasa yatatekelezwa.
  4. Kwa kuanzia tutalipwa dola milioni 300 zilizokuwa ni kishika uchumba, lakini sasa sio kishika uchumba tena bali ni kifuta machozi cha kusamehe lile deni kubwa la kodi la dola bilioni 190.
  5. Barrick ataunda kampuni mpya ya ubia na Tanzania kuchukuwa shughuli za Acacia
  6. Kwenye hiyo kampuni mpya, serikali ya Tanzania itakuwa na shares asilimia 16%.
  7. Bodi ya hiyo kampuni mpya itakuwa na Watanzania.
  8. Makao Makuu yatakuwa Mwanza, Tanzania
  9. Menejiment itakuwa na Watanzania.
  10. Tutagawana manufaa ya kiuchumi pasu kwa pasu, yaani 50/50.(NB.Manufaa ya kiuchumi ni economic benefits na sio faida profits)
  11. Watanzania wenye sifa wataajiriwa nafasi za juu.
  12. Wafanyakazi wa migodi, watasomeshwa elimu ya ujuzi kufikia kiwango cha sisi kuwa na wataalamu wa kila kitu kwenye migodi
  13. Manunuzi makubwa yatafanyika nchini.
  14. Makinikia yatachenjuliwa nchini pale ambapo Tanzania tutaonyesha uwezo.
  15. Migodi itatumia zaidi ya dola milioni 70 kila mwaka kutoa huduma za kijamii, CSR.
Ndipo Mhe. Zitto naya akaibuka na bandiko lenye kichwa cha habari
MAKUBALIANO YA SERIKALI NA BARRICK GOLD CHANGA LA MACHO

Zitto akaandika naomba kunukuu
"Kiambatanisho namba 4 kimeweka muhtasari wa kinachoitwa ‘Material Terms’ katika Makubaliano ya awali kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold ambayo yamesainiwa (INITIALED) mwezi Mei mwaka huu. Kimsingi Barrick imelazimishwa na kanuni za masoko ya mitaji kuweka wazi makubaliano hayo. Ni masikitiko makubwa kuwa Serikali yetu haijathubutu hata kuliambia Bunge kuwa kuna makubaliano ya namna hiyo wakati wa Bunge la Bajeti, imesaini kwa siri kama ulivyosainiwa mkataba wa Buzwagi.

Ikumbukwe kuwa makubaliano hayo yamesainiwa wakati Bunge likiwa linaendelea na mkutano wake jijini Dodoma. Sisi kama wawakilishi wa Wananchi imebidi kusubiri masoko ya mitaji ya ‘MABEBERU’ wa London yaweke wazi masuala yanayohusu nchi yetu.

Ingekuwa nchi nyengine, Makubaliano haya ya KIMANGUNGO kati ya Serikali ya Rais Magufuli na Kampuni ya Barrick, ingetosha kuiondoa Serikali madarakani. Rais John Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi wameuza nchi yetu kwa kipande cha dhahabu. Wamelihujumu Taifa.

Kabwe Z.Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Vuga, Zanzibar
Julai 20, 2019" Mwisho wa kunukuu.

Nami nilimjibu naomba kujinukuu
"Mkuu Mhe. Zitto, kwanza asante kwa bandiko hili na uzalendo wako kwa nchi yako. Kwa vile mimi ni miongoni wa wana jf ambao tumeandika sana kuhusu hili, nitachangia baadhi ya vipengele vichache with due respect, na kwa wasiojua lugha ya Malikia, ni kwa heshima na taadhima, tuwe wakweli toka ndani ya nafsi zetu, tuache upotoshaji, just tell the truth and the truth will set you free, sii kweli kuwa mkataba huu umeisha sainiwa!, hilo neno (INITIALED) sio kuonyesha kuwa umesainiwa, bali katika mikataba, kunatakiwa signatories watie initials zao kwenye kila page ya draft kuonyesha wameelewa, lakini draft ni draft na mkataba ni mkataba!, ku INITIALED sio kusaini.

Hicho kiambanisho 4 ni draft, na mimi nimekiweka kwenye bandiko langu kuhusu kununuliwa kwa kampuni yang Acacia

Huu ndio utakuwa ushindi wa kwanza wa kishindo wa rais Magufuli na awamu ya tano katika vita dhidi ya rasilimali madini na ndio kuanza rasmi utekelezaji wa kwanza wa sheria mpya ya madini.
Hongera Prof. Kabudi, Hongera Rais Dr. Magufuli na Hongera sisi Watanzania wote katika ujumla wetu japo kwenye hili la makinikia, bado kuna mambo hayajakaa vizuri.

Hatuwezi kusema kila kitu mpaka baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, na nikasisitiza kwenye makinikia kuna lakini sikuiweka hiyo lakini kwa sababu bado hatujaona makubaliano yaliyofikiwa, hayo ni mapendekezo tuu, yaani draft, siku zote drafts zote huwa ni tentative, inaweza kubadilika, hivyo naomba kusisitiza katika hili tuwe wakweli, tuvute subra na tutumie ukweli, tuache upotoshaji!. Japo pia nakiri baadhi yang hoja za Zitto zina mashiko na zilitasaidia sana taifa kuboresha makubaliano haya kabla hayajasainiwa.

Sijamuita Zitto mpotoshaji, nimesema kwenye hoja zake kuna upotoshaji. Kwa vile Zitto namfahamu fika toka enzi zetu za UDSM, hivyo naifahamu intelect ya Zitto, haiwezekani katika kiambatanisho hicho, awe hayajaona maneno haya
"Appendix 4 Summary of the material terms of the current draft documentation under discussion (but not yet finalised) with the GoT The discussions between Barrick and the GoT have advanced to the point where draft documentation was initialled by the GoT on 19 May 2019". Hapa maana yake hii ni draft tuu imekuwa initialled na GOT lakini haijawa finalized, kwa Zitto ninayemjua mimi, haiwezekani Zitto awe hakuyaona maneno haya.

Kwenye document hiyo, kuna maneno ya capital letters na bold
"THERE IS NO CERTAINTY THAT THE TRANSACTION DOCUMENTS WILL BE AGREED WITH THE GOT IF THE SCHEME BECOMES EFFECTIVE AND THE TERMS OF THE FINAL FORM OF TRANSACTION DOCUMENTS, IF AGREED, MAY DIFFER FROM THOSE SUMMARIZED BELOW."
Siamini kuwa Zitto hakuyaona maneno haya, kwa wasio jua lugha ya Malikia ni "hakuna uhakika kama makubaliano haya yatakubaliwa na GOT, na hata yakikubaliwa, yanaweza kuwa ni tofauti na kilichokubaliwa hapa!. Hivyo Zitto kusema ni mkataba umesainiwa, huu sio sahihi, ni upotoshaji kwa makusudi tuu sio kuwa hakuona mistari hiyo!.

Kwenye kipengele cha 11 cha makubaliano hayo kinasema wazi kuwa
"11. The conditions set out in (a) to (g) of paragraph A10 above may be waived by the Acacia parties and the conditions set out in (h) to (i) of paragraph A10 above may be waived by the GoT. "
Hapa wanasema masharti ya mkataba huu yaliyowekwa kwa ibara ya 10, yanaweza kukubaliwa au kukataliwa na Acacia, au na GOT kuthibitisha kuwa makubaliano haya sio final and conclusive, haiwezekani Zitto ninayemjua mimi, hakuliona hili!.

Kipengele cha 12 kinasema
"12. Those provisions which are stated to become effective on signing of the Framework Agreement"
Hapa kwa lugha ya Malkia ni masharti hayo, yatatakiwa kutekelezwa baada ya kusaibiwa kwa makubaliano hayo, bado hakuna makubaliano yoyote yaliyosainiwa!. Siamini kuwa Zitto hakuliona hilo.

Kwenye kiambatisho hicho kuna hii para
"The discussions between Barrick and the GoT have advanced to the point where draft documentation was initialled by the GoT on 19 May 2019, albeit with a number of substantive issues still outstanding which are subject to further discussion. Whilst a basis for settlement has been developed, the terms have not yet been finalised"
Naamini kabisa Zitto anajua maana ya maneno hayo, hawa jamaa wanasema bado kuna issues ni still outstanding na zinahitaji majadiliano zaidi.

Sasa ili kumtendea haki Mhe. Zitto, naomba kuziweka hoja zake zote 5 na kusema hoja zipi ni za kweli na hoja zipi ni za upotoshaji tuu.

1. Zitto Anasema: Dola Milioni 300 za kumaliza mgogoro KIINI MACHO
Serikali imekubaliana na Barrick kuwa italipwa Dola milioni 300 (wastani wa TZS 700 Bilioni) kama malipo ya kumaliza mgogoro wote (full, final and complete settlement) na SIO kishika uchumba kama Serikali ilivyoeleza umma. Barrick watalipa fedha hizi kwa muda wa MIAKA 7 na zitakuwa ni baada ya kuondoa madai yote ya kodi ambayo Acacia inaidai Tanzania.

Itakumbukwa kuwa Acacia Group ina madai ya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT refunds) inayofikia takribani Dola za Marekani milioni 240 (wastani wa 552 Bilioni). Hivyo katika malipo ya Dola za Marekani Milioni 300, zitakazobakia baada ya kutoa madai ya VAT refunds ni Dola Milioni 60 (wastani wa 138 Bilioni) tu. Kama tutakavyoona katika hoja ya pili hapa chini hata hizi Dola za Marekani Milioni 60 kimsingi hazitatolewa.

Kwenye hoja hii Zitto kuna sehemu amesema kweli, hapa tumepigwa. lakini kuna sehemu Zitto sio tuu hakusema kweli bali amepotosha. Kwa vile Mhe. Zitto ni Mbunge akisema kitu ndipo watu wanakizingatia na kukitilia maanani, hivyo hii observation ya Zitto will make a big impact kwenye the final draft. Na hili la dola milioni 300 ndio kalipotosha wakati sisi akina kajamba nani, ma lumpen proletariat' hili tuliliona kitambo na tukalisemea sana humu, because we are nobody, no one heard lakini sasa kulisemea Zitto, kila mtu atasikia.

Baada ya Barrick kuinunua Acacia, ni kweli tutalipwa kifuta machozi cha dola milioni 300, sii kweli kuwa malipo haya yatatolewa baada ya kuondoa VAT refund, bali kweli kuwa malipo haya yatalipwa katika kipindi cha miaka 7.
Tukiisha saini tuu mkataba, tutalipwa upfront ya dola milioni 100. Hivyo hoja ya Zitto kuwa kwenye dola milioni 300, tutaambulia dola milioni 60 sii kweli. Ile siku Barrick wanakuja kusaini mkataba, ile kuangusha tuu wino kusaini, kitita cha dola milioni 100 kinawekwa mezani as upfront payment kama ilivyoelezwa hapa
"There will be an initial upfront “payment” by way of assignment to the GoT of minerals contained in containers at Dar es Salaam port with a value of US$100 million". Shilingi milioni 200 zilizobakia, ndizo zitalipwa katika mikupuo 6 ya dola milioni 33.33 kwa mwaka katika miaka 6.

Pamoja ya Zitto kutokuwa mkweli, lakini ukweli wa Zitto kuwa tunapigwa uko pale pale. Tunapigwa kwa sababu hizi dola milioni 300, tuliahidiwa as goodwill money, hasikupaswa kuwa conditional wala hazikupaswa kulipwa kido kidogo, zilipaswa kulipwa there and then.

Kitu cha pili kwa vile hiki kilikuwa ni kishika uchumba tuu na kuonyeshea goodwill ya kulipia mahari kamili ya binti yetu ambayo ni dola bilioni 190, lakini serikali yetu imesamehe mahari yote, na kile kishika uchumba sasa ndio kigeuzwa kifuta machozi, hapa sasa ndipo tulipopigwa!. Hapa nilishauri serikali yetu lazima itufafanulie Watanzania the basis ya msamaha huu.

2. Zitto Anasema: Barrick Gold Wamesamehewa Kodi ya Ongezeko la Mtaji USD 85.6M
Serikali ya Tanzania imetoa misamaha mbalimbali ya Kodi kwa Kampuni ya Barrick Gold katika makubaliano yaliyoingiwa ikiwemo kodi ya ‘Capital Gains’ ambayo inatokana na mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick. Itakumbukwa kuwa mwaka 2012 Bunge lilitunga sheria ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Mtaji kwa mauzo ya mali zilizopo Tanzania ili kudhibiti ukwepaji wa Kodi.

Barrick inainunua Acacia kwa Hisa ambazo Barrick haikuwa inamiliki ambazo zimepewa thamani ya Dola Milioni 428. Capital Gains Tax ya 20% ilipaswa kulipwa lakini Rais Magufuli na Profesa Kabudi wametoa ‘waiver’ (Msamaha) na kupoteza Mapato halali na ya kisheria kwa nchi yetu ya Dola Milioni 85.6 (wastani wa TZS 200 Bilioni). Tukirejea hoja ya kwanza hapo juu utaona kuwa sio tu Tanzania kiuhalisia haitapata Dola Milioni 300, bali pia tunaipa zawadi Barrick ya Dola Milioni 25.6 (wastani wa TZS 59 Bilioni) za ziada.

Mimi nimejibu: Hili ni kweli, hawa wamesamehewa na ni kawaida kwa serikali yetu kutoa misamaha ya aina hii kwa kutotoza capital gain tax kwenye acquisitions kibao, au kwenye hostile take overs,
Celtel ilibadilika kuwa Zain, ikabadilika kuwa Airtel, hakuna tulicholipwa!.
Sheraton ilibadilika kuwa Moven Pick, Royal Palm sasa Serena sijui kama tulilipwa kitu!.
Mobitel, iligeuka kuwa Tigo sijui kama tulilipwa kitu!.
Kibo Breweries ilikuwa taken over kwenye hostile take over, sijui kama tulilipwa kitu, hivyo hapa Zitto is right, but its not the first time, kama kule kuingine tumetoa misamaha hiyo, why not now?.

Zitto amesema:Tanzania kupewa Hisa 16% za daraja B lakini Watanzania kunyimwa umiliki wa 30% kupitia Soko la Hisa la DSE
Ni kweli kuwa Serikali itapewa hisa za bure 16% kwenye Kampuni tanzu zote za Acacia hapa nchini kama tulivyoambiwa na Serikali. Lakini hisa hizo ni za Daraja la B ambazo ni hisa dhaifu kulinganisha na zile za Daraja la kwanza. Hisa hizo haziruhusiwi kuuzwa, hazina kura kwa masuala fulani fulani ya Kampuni na huwezi hata kuziweka kama dhamana ya mikopo. Hata mgawo wa gawio hisa hizi hupata baada ya wale wa daraja A kulipwa kwa ukamilifu.

Licha ya makubaliano haya ya hovyo na yasiyo na tija, Serikali yetu imetoa ‘waiver’ (msamaha) kwa Barrick kutoorodhesha hisa kwenye Soko la Hisa la Tanzania. Sheria ya Madini ya mwaka 2010 (Wakati wa Waziri William Ngeleja) na Kanuni zake iliweka sharti kwamba ni lazima makampuni ya madini yauze 30% ya hisa kwa Watanzania kwenye soko la Hisa la Tanzania.

Makubaliano ya Mei 2019 kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania yametoa msamaha kwa Barrick kutekeleza sharti hilo la kisheria. Uamuzi huu unavunja sheria za nchi, ni hujuma kwa Watanzania kumiliki maliasili zao na ni ukosefu wa maarifa ya kiuchumi kwa kiwango kisichomithilika wala kuvumilika.

Mimi Nimejibu: Hili la hisa za daraja B ni kweli lakini sii kweli kuwa Watanzania tumenyimwa umiliki wa 30% kupitia DSE!.
Hizi hisa aslimia 16 za Tanzania, ni free carried shares, tumepewa bure, na kote free carried shares huwa haziuzwi ila sii kweli kuwa hazina voting rights. Pia sii kweli kuwa Watanzania tumenyimwa umiliki wa 30% kupitia DSE!.
Naomba hapa ikumbukwe, shares zinazouzwa ni shares za Acacia zinazo trade kwenye London Stock Exchange tuu, hata yale mambo ya PUSU ni mambo yao, sijasikia lolote kuhusu shares za Acacia zinazo trade kwenye DSE, hivyo business ya hisa za Acacia ndani ya DSE zinaendelea as usual.Hata baada ya sale kukamilika, hivyo kampuni mpya italazimika kuuza 30% ya hisa zake kwenye DSE na Watanzania wenye fedha, watakuwa free kununua hisa hizo kwenye soko.

Tukija kwenye voting rights, sii kweli kuwa Tanzania hatuna voting rights, bali ni kawaida kwa free shares zote hazina voting rights ya pro rata ya share to shares bali tuna voting rights za block shares. Sisi Tanzania wenye free carried shares za 16%, serikali yetu iteteua mjumbe mmoja wa bodi ambaye ni Mtanzania, ataingia na kuwa mjumbe wa bodi ya hiyo kampuni mpya, kwa zile asilimia 16% za shares zetu na ndani ya kikao cha bodi, atakuwa na voting righs za kupiga kura 1 as a block vote kuwakilisha zile shares 14, wakati wajumbe wengine wa bodi, watakaowakilisha zile subscribed shares za asilimia 84%, wanatakuwa na voting rights ya votes 84 kwa uwiano wa share to shares votes pro rata according to shares subscription. Hivyo ndani ya bodi ya hiyo kampuni Mtanzania atakayeingia humo, atakuwa anapiga kura moja kuwakilisha the block ya zile shares zetu 16 za bure, na katika mgao wa faida, sii kweli kuwa tutapata mgao baada ya wale wengine, huu ni uongo!, Tanzania tunagaiwa mgao sawa kabisa wa faida kwa mujibu wa shares hizo.

Kwa wasio jua kuhusu shares za group A na group B shares za group A ni shares za watu walio invest kwa kutoa fedha zao kununua shares, yaani subscribed shares, na shares group B ni shares za heshima, shares za hisani zinazotolewa bure, shares hizi za hisani haziruhusiwi kuuzwa, wala kuwa disposed or transferred na zina block votes rights. Hili hufanyika kwa makampuni kuwapa hisa za heshima land owners, mfano UAE, hakuna foreigner anayeruhusiwa kumiliki ardhi, ardhi yote ni ya wazawa, hivyo investor akija lazima aingie ubia na wazawa mzawa anatoa land, investo ana jenga, kama alivyofanya Rugemalila kwenye IPTL alitoa ardhi yake na kupewa 30 m% ya shares, IPTL ikaikwa kwa PAP, Ruhemalila akalipwa shares zake, akagawa fedha zake, sasa anateswa bure bila kosa lolote!.

Zitto Amesema: Bunge lafungwa mikono kubadili sheria yeyote
Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick wamekubaliana kuwa baada ya mkataba wao kukamilika Bunge la Tanzania haliwezi kutunga sheria yeyote ambayo itabadili makubaliano hayo na kodi zote zilizokuwa zinafanya kazi wakati wa kuingia makubaliano hazitaweza kubadilishwa kipindi chote ambacho Barrick watakuwa wanafanya kazi Tanzania (fiscal stabilisation).

Makubaliano ya namna hii ndiyo kitu kilicholeta Buzwagi mwaka 2007 ambapo Serikali za Rais Mkapa na Rais Kikwete ziliingia mikataba ya kulifunga Bunge kutimiza majukumu yake ya kikatiba kama Dola (sovereign). Sheria ya Madini yam waka 2010 iliondoa sharti hili kufuatia mapendekezo ya Kamati ya Bomani. Rais Magufuli na Waziri Kabudi wameturudisha kwenye unyonyaji wa kihayawani kabisa.

Mimi nimejibu: Kwenye hili pia Zitto hajasema kweli, kwenye document hii yenye kurasa 91, hakuna popote Bunge la JMT limetajwa!. Makubaliano haya yatatawaliwa na sheria za Tanzania. Hakuna popote Bunge limetajwa, bali kilisemwa ni maadam sheria iliyotungwa ninaelekeza free carried shares ni asilimia 16%, baada ya kusainiwa kwa makubaliano haya, serikali haiwezi kuongeza kile kiwango cha shares zaidi ya asilimia 16% za kisheria unilateral, kama ilivyofanya kwa sheria mpya ya madini "the GoT will not unilaterally seek to increase its share ownership or economic participation rights in the TMC", hii maana yake, serikali haiwezi kujiamua yenyewe pekee bila kuishirikisha Barrick.

Hili mimi nililizungumzia kitambo ile tuu tunabadili sheria, kuwa kisheria, sheria yoyote ambayo ni sheria nzuri, inaanza kufanya kazi tangu pale inapotungwa. Sheria yoyote inayotungwa halafu ina act retrorespect is a bad law. Hivyo tulipopitisha sheria mpya, nikasema tuwashukuru sana Barrick wamekubali kuanza upya kwa sheria mpya, Hakuna mwingine yoyote mwenye mkataba wa zamani amekubali kubadili na kutumia sheria mpya na hatuwezi kuwalazisha.

Zitto amesema: Barrick wameruhusiwa kufungua kesi ughaibuni kinyume na Sheria

Kwa mujibu wa sheria mpya za madini za mwaka 2017 makampuni yamezuiliwa kufungua mashauri yake nje ya Tanzania. Migogoro yote inapaswa kushughulikiwa na mahakama za ndani ya nchi. Serikali ya Tanzania imekubaliana na Barrick kuwa migogoro itafanyika kwa mujibu wa kanuni za UNICITRAL na Rais wa Kituo cha usuluhishi wa migogoro cha Singapore ndio atateua wasuluhishi ambao hapatakuwa na Mtanzania.

Mimi nimejibu: Kwenye hili, Zitto yuko right 100% kipengele kwenye sheria yetu mpya kinachokataza usuluhisi nje ya Tanzania ni hiki
1563770513163.png


Ile siku sheria hii inapitishwa Bungeni, mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa sheria, Tundu Lissu, alionya kuhusu hili kuwa hatuwezi kupitisha sheria ambayo hatuwezi kuitekeleza and soon tutakuja kuifanyia marekebisho. Hivyo hapa Zitto yuko right, makubaliona haya ni kinyume cha sheria, hivyo ni illegal.

Hitimisho
Kuwa Upinzani basic kazi yake iwe ni kupinga tuu kila kitu, kiwe kizuri kiwe kibaya wao ni kupinga tuu. Kazi rasmi ya upinzani sii kupinga tuu, bali ni kupinga kuonyesha makosa na kwa hoja mbadala za ukweli na sio kwa hoja za uongo na upotoshaji na kwenye jambo lenye maslahi kwa taifa kama hili la rasilimali madini, Wapinzani, CCM, SerikalI na Watanzania wote tusimame as one tuongee lugha moja kwa sauti moja.

Wito kwa Wapinzani: Sio kupinga tuu kila kitu, kwenye maslahi ya Taifa tuwe kitu kimoja. Wito kwa Serikali: Ikubali Kusikiliza hoja za msingi za upinzani na kuzifanyia kazi. Tanzania ni nchi yetu sote, sio Tanzania ya CCM pekee au Tanzania ya serikali ni Tanzania ya Watanzania wote wakiwemo CCM, serikali, wapinzani na hata akina sisi wenye vyama kimya kimya, let's stand as one.

Jumatatu njema
Paskali
 
Hahaha, kaka umekosea kusema wasipinge bila kujali wanapinga nini, Umoja wa kitaifa siyo lazima wakubali mambo ya rais aliyepo madarakani, inawezekana yote yakawa ya hovyo, hivyo sioni kwanini wasiyapinge yote kwa maslahi ya taifa.

Na ukweli unapimwaje kaka, maaana wewe umesoma sheria, How do you measure the Truth?

Utaifa ndio unafanya wanapinga mambo ya hovyo hovyo yanayofanywa na mtawala aliyepo madarakani.

Lini umesikia wakenya wakipingana na hoja za JPM, au lini umesikia waganda wakilalamikia maamuzi ya mahakam za tanzania, au tume ya uchaguzi, au ukandamizaji wa polisi Tanzania?

Yote yanayolalamikiwa hulalamikiwa na watanzania, na hiyo ni kwa sababu ya utaifa wao, na uzalendo kwa nchi yao.

Ni ajabu kumuacha mtu afanye mambo ya hovyo hovyo TANZANIA hii usiyakemee au kuyakataa kabisa halafu ukawa mzalendo.

Uzalendo ni kuweka maslahi ya wengi na taifa mbele, Siyo ubinafsi na dhuluma.

Sasa tunapotoshwa, na tunapinga kwa nguvu upotoshaji huo, tunaambiwa sisi sio wazalendo, eti mpotoshaji ndiye mzalendo.

Tunaambiwa tumuamini tu, bila hata yeye kutuambia anafanya nini kwa nini?

Ni vyema akawa transparent KWA MASLAHI YA TAIFA, Jiulize kwanini mikataba haiendi bungeni, kwanini manunuzi yasiyo na maelezo yanaamishiwa ofisi ya rais?

Kwanini watanzania wasi hoji mali na rasilimali zao?

Uzalendo ni nini au lina maana gani kwako?

Utaifa ni nini kwako, na umoja na ukweli ni nini au vina maana gani kwako mleta mada?
 
Pascal Mayalla kabla ya kuendelea na uzi baada ya lepe, nikukumbushe jambo

Upinzani ''opposition'' ni wanaopinga, lakini kazi yao si kupinga bali kuwa mbadala

Hivyo kazi ya upinzani ni mbadala ambao hugeuka kupinga pale kunapokuwepo na hoja za chama tawala na Upinzani.

Ni hoja ndizo zinazaa kupinga lakini si kazi yao kupinga bali kutumia mbadala unaozaa kupinga
 
Uliwahi kumuuliza Rais kuhusu utawala wa Sheria, akakujibu kuwa maana ya Mayala ni njaa. Leo bado unajikomba na kujibaraguza na sasa unawatetea mabeberu Barrick, be independent of who you are.
 
Uzalendo sio kumkubali rais aliepo wala matendo yake, hatulazimishani, uzalendo utakuja wenyewe automatically, tangu gogoro LA masisiemu lianze mada kama hizi ni miyeyusho sana!
 
Zitto amesema:Tanzania kupewa Hisa 16% za daraja B lakini Watanzania kunyimwa umiliki wa 30% kupitia Soko la Hisa la DSE
Mkuu Pascal Mayalla kwenye hilo la class A na B nakuomba upitie ufafanuzi huu.

Kwenye swala la kuwa listed DSE nafikiri serikali ina nafasi ya kukataa pendekezo hilo lakini Barick wao wamesema kwenye hiyo draft kwamba wasilazimishwe kuwa listed DSE.
Kama walivyosema hawatowajibika kujenga mtambo wa kuchakata makinikia hapa Tanzania
 
Back
Top Bottom