Search results

  1. JamiiCheck

    Upotoshaji wa taarifa huweza kufanyika kwa kuchukua tukio la zamani na kulifanya lionekane la sasa

    Upotoshaji wa taarifa huweza kufanyika kwa kuleta tukio la lililotokea zamani na kulitangaza au kuliunda ili lionekane kama limetokea leo. Wapotoshaji huweza kutumia mbinu hii kwa namna mbalimbali. Katika mjadala huu tutagusia mbinu tatu zifuatazo: Kubadilisha Tarehe au Muktadha: Mtu anaweza...
  2. JamiiCheck

    Upotoshaji wa Taarifa na Athari Zake kwa Haki katika Jamii

    Taarifa sahihi ni msingi muhimu katika kuhakikisha haki zinapatikana katika jamii zetu. Hata hivyo, upotoshaji wa taarifa ni tatizo linaloweza kusababisha ukosefu wa haki kwa baadhi ya watu. Mathalani, katika vyombo vya utoaji haki kama Mahakama, taarifa potofu zinaweza kupelekea kutoa hukumu...
  3. JamiiCheck

    Upotoshaji wa taarifa huweza kufanya kupitia kutengeneza nukuu potoshi za watu maarufu

    Mitandao ya kijamii imejaa nukuu za Wataalamu na watu maarufu mbalimbali kutoka katika nyanja mbalimbali. Watu wanaweza kupotosha taarifa kwa kutengeneza nukuu zisizo za kweli au kuzibadilisha nukuu za watu fulani ili zifanane na mtazamo wao au kusudi lao. Wapotoshaji huzitengeneza na kudai...
  4. JamiiCheck

    Upotoshaji wa taarifa wakati wa uchaguzi unaweza kuathiri masuala ya kijinsia (Wanawake)

    Upotoshaji wa taarifa wakati wa uchaguzi unaweza kuathiri masuala ya kijinsia kwa njia kadhaa: Kueneza Habari Potofu Kuhusu Wagombea wa Kike: Wakati mwingine, habari potofu zinaweza kutolewa kuhusu wagombea wa kike ili kuwaharibia sifa zao au kuwadhalilisha. Hii inaweza kujumuisha kusambaza...
  5. JamiiCheck

    Aprili 2: Siku ya Kimataifa ya Uhakiki wa Taarifa

    Aprili 2 kila mwaka huadhimishwa kama Siku ya Kimataifa ya Uhakiki wa Taarifa ili kuongeza uelewa na umuhimu wa kuhakiki na kuthibitisha ukweli katika taarifa zetu za kila siku. Katika ulimwengu uliojaa taarifa za haraka na mara nyingi zenye utata, uhakiki unakuwa muhimu zaidi kuliko hapo awali...
  6. JamiiCheck

    Wakati wa Uchaguzi watu hutengeneza Akaunti feki zenye majina ya Wagombea

    Wakati wa Uchaguzi baadhi ya Watu huibuka na kutengeneza akaunti 'feki' na kuzipa majina ya Wagombea au kubadili jina la akaunti zao na kutumia jina la mgombea fulani. Akaunti hizo hutumika kutengeneza taarifa au maudhui mbalimbali yanayomuhusu Mgombea wa Uchaguzi, hutumika kupotosha taarifa...
  7. JamiiCheck

    Yoon Suk Yeol: Taarifa za uongo zinaathiri wananchi kufanya maamuzi sahihi wakati wa uchaguzi

    Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol akiwa katika Mkutano wa Tatu wa Demokrasia uliofanyika Machi 18, 2024 ametoa wito kwa viongozi wote Ulimwenguni kuunga mkono jitihada za kukomesha taarifa potofu Yoon ameeleza Taarifa zisizo za kweli wakati wa Uchaguzi huweza kuathiri mchakato mzima wa...
  8. JamiiCheck

    KWELI Uvutaji wa Sigara huchangia ugumba kwa wanaume

    Matumizi ya tumbaku ni moja ya maafa ya afya ya umma yanayojulikana sana. Licha ya ripoti nyingi kuhusu afya ya umma, matumizi ya tumbaku yanazidi kuongezeka katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), takriban watu Bilioni 1.3 duniani wanavuta...
  9. JamiiCheck

    Utoaji taarifa zisizohakikiwa za vifo vilivyotokana na Ajali huzua taharuki kwenye Jamii

    Pamoja na ukweli kuwa teknolojia imeleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya habari na mawasiliano, ambapo sasa mtu yeyote(Netizen) anaweza kutoa taarifa ikawafikia watu wengi kwa haraka sana, lakini ni vyema kuhakiki na kuthibitisha taarifa yoyote ambayo unaona inaweza kuzua taharuki kabla...
  10. JamiiCheck

    Upotoshaji wa historia ya Mgombea wakati wa Uchaguzi na mbinu za kuepuka kupotoshwa

    Wakati wa uchaguzi, baadhi ya watu hutengeneza taarifa za uongo au kuficha ukweli kuhusu historia ya mgombea fulani ili kuathiri taswira yake kwa umma. Taarifa hizo zinaweza kuwa mwaka wa kuzaliwa, historia ya uraia wake, au elimu yake. Mathalani, mtu au kundi la watu linaweza kusambaza taarifa...
  11. JamiiCheck

    UZUSHI Dhana Potofu kuhusu Ugonjwa wa Figo

    Alhamisi ya pili ya Mwezi Machi kila mwaka, Dunia huadhimisha Siku ya Figo Duniani ili kutoa ufahamu na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa afya ya figo na magonjwa yanayohusiana na figo. Kupitia maadhimisho haya, watu hupata fursa ya kujifunza kuhusu njia za kuzuia magonjwa ya figo, kudhibiti...
  12. JamiiCheck

    Uhakiki wa taarifa ni silaha muhimu ya kupambana na taarifa potofu

    Kuhakiki taarifa ni Silaha ya msingi katika kupambana na Usambaaji wa taarifa Potofu ndani na nje ya Mitandao Jamii inapojenga tabia ya kufanya uhakiki wa kila taarifa inayokutana nayo, itawawezesha kufanya Maamuzi Sahihi katika masuala mbalimbali yanatokea katika Jamii husika Je, wewe ni...
  13. JamiiCheck

    AFP: Upotoshaji wa taarifa wakati wa Uchaguzi huweza kumhusu Mgombea, Chama cha Siasa au Mfumo Mzima wa Uchaguzi

    Shirika la habari la AFP wakiwa wanatoa mafunzo mtandaoni wamebainisha namna upotoshaji wakati wa Uchaguzi unaweza kutokea kwa Mgombea, Chama pamoja na Mfumo. Wanaeleza, Upotoshaji kwa Mgombea hulenga kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu Mgombea fulani. Upotoshaji wa Chama cha Siasa hukusudia...
  14. JamiiCheck

    Hatua za kufuata unapofanya uhakiki wa Picha kwa kutumia TinEye

    TinEye ni nyenzo nzuri ya kutafuta picha kwenye wavuti ambayo inaweza kutumiwa kufanya uhakiki wa Picha. JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha. 1. Fungua Kivinjari Chako Anza kwa kufungua kivinjari chako kwenye kifaa chako...
  15. JamiiCheck

    Hatua za kufuata unapofanya uhakiki wa Picha kwa kutumia Yandex

    Yandex ni njia nyingine ya utafutaji inayotumika sana kufanya uhakiki wa picha. JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha. 1. Fungua Kivinjari Chako Anza kwa kufungua kivinjari chako kwenye kifaa chako cha mkononi au kompyuta...
  16. JamiiCheck

    Hatua za kufuata unapofanya uhakiki wa Picha kwa kutumia Google Image Search

    Uhakiki wa Picha kwa kutumia Google Image Search ni njia muhimu ya kubaini asili au maelezo zaidi kuhusu picha fulani. JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha 1. Tembelea Google Image Search Fungua kivinjari chako na nenda...
  17. JamiiCheck

    Teknoloji ya Akili Mnemba itaathiri chaguzi zinazofanyika mwaka 2024 Duniani kote

    Matamshi ya chuki, propaganda za kisiasa na uongo si matatizo mapya mtandaoni, nyakati za uchaguzi kama hizi huzidisha zaidi matatizo hayo. Matumizi ya roboti, au akaunti bandia (Feki) za mitandao ya kijamii, imerahisisha zaidi kueneza habari zisizo sahihi kimakusudi, pamoja na uvumi usio sahihi...
  18. JamiiCheck

    Matamshi ya Chuki na jinsi ya kukabiliana nayo

    Matamshi ya chuki yaweza kuwa maneno au vitendo vinavyoonyesha hisia za uadui, dhihaka, au kutokuwajali kuelekea mtu au kundi fulani. Yanaweza kujitokeza kwa misingi ya tofauti za kijamii, kitamaduni, kidini, kisiasa, au mambo mengine. Chuki inafarakanisha makundi, huchangia vurugu na migogoro...
  19. JamiiCheck

    Kufanya uhakiki wa taarifa hukuepusha na utapeli wa mitandaoni

    Uhakiki wa taarifa ni mchakato wa makusudi wa kufanya tathmini ya taarifa ili kujua chanzo au uhalisia wake. Katika ulimwengu wa leo, takwimu za Global Media Statistics zinaeleza kuwa zaidi ya 62.3% ya watu duniani wanatumia mitandao ya kijamii, ambayo inafanya kuwa jukwaa kubwa la usambazaji...
  20. JamiiCheck

    Yafahamu matangazo feki ya kazi na namna ya kuyaepuka

    Kupata kazi ni lengo linalohitaji jitihada na tahadhari, lakini katika ulimwengu wa leo wa mtandao, kuna hatari ya kukumbana na matangazo ya kazi feki. Kutambua ishara za matangazo haya na kujifunza jinsi ya kuepuka kushawishiwa ni muhimu kwa mafanikio ya kutafuta ajira. Matangazo ya kazi feki...
Back
Top Bottom