Upotoshaji wa taarifa huweza kufanya kupitia kutengeneza nukuu potoshi za watu maarufu

JamiiCheck

Member
Nov 3, 2023
54
44
Mitandao ya kijamii imejaa nukuu za Wataalamu na watu maarufu mbalimbali kutoka katika nyanja mbalimbali.

Watu wanaweza kupotosha taarifa kwa kutengeneza nukuu zisizo za kweli au kuzibadilisha nukuu za watu fulani ili zifanane na mtazamo wao au kusudi lao.

Wapotoshaji huzitengeneza na kudai zimesemwa na watu fulani ili kuzipa uzito au kuaminika zaidi, hata kama si sahihi.

Upotoshaji huu unaweza kufanyika kwa sababu za kisiasa, kijamii, au hata kibiashara.

Hivyo, kabla ya kuamini na kutumia nukuu fulani ni muhimu kuhakiki uhalisia wake
 
Ujumbe huu uwafikie nyie Wapotoshaji wote wa Jamiiforums popote mlipo.

Kama umesoma ushauri huu hapa, wafikishie ujumbe wapotoshaji unao wajua.
 
I don't care whether or not they stole my ideas. What I care is that they don't have any of their own. ~Tesla
 
Back
Top Bottom