Eneo la Malamba Mawili ambalo lipo kata ya msigani linahudumiwa kupitia mtambo wa Maji Ruvu Juu.
Kutokana na maeneo hayo kuzungukwa na vilima vikali na hupata maji siku ya Jumanne, Alhamis na Jumapili, lakini baadhi ya maeneo kushindwa kupata maji pindi msukumo wa maji unapokuwa mdogo.
Mamlaka...
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amewataka wananchi wa Msomera kuhakikisha wanaibeba ajenda ya nishati safi ya kupikia kwa vitendo kuunga mkono jithada za serikali Ili kulinda mazingira na mabadiliko ya tabianchi.
Kapinga ameyasema hayo katika Kijiji cha Msomera wilaya ya Handeni Mkoa...
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) ameongoza Mkutano wa 16 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi (SCFEA) na mkutano wa Mashauriano ya Kibajeti wa Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango wa Sudani...
UFAFANUZI KUHUSU MALIPO YA FEDHA ZA KUJIKIMU KWA ROBO YA NNE
Ijumaa, Mei 17, 2024
Tunapenda kuwafahamisha wanafunzi wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu na umma kuwa tunakamilisha malipo ya fedha za kujikimu (Chakula na Malazi) kwa robo ya nne (Quarter IV) na wanafunzi watarajie kupokea fedha...
Serikali imesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) haitozi kodi kwa wasafiri kati ya Zanzibar na Tanzania bara wanaobeba vitu kwa matumizi binafsi.
Hayo yameelezwa bungeni, jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Danie Silo (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt...
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Kushoto) akipokea Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya Nchini kwa mwaka 2023 kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo (Kulia) katika Ukumbi wa Habari...
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imewasilisha Bungeni Bajeti ya Tsh. 67,905,259,000 inayotarajiwa kutumiwa na Wizara hiyo katika kipindi cha mwaka 2024/25
Katika wasilisho lake Bungeni, Waziri Dkt. Doroth Gwajima amesema Tsh. 47,487,079,000 kati ya Fedha hizo...
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 15, Kikao cha 28, leo Mei 17, 2024 ambapo Waziri Dkt. Gwajima D atasoma Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalum kwa mwaka wa fedha 2024/2025...
Katika kukabiliana na matukio ya uhalifu yanayotokea katika jamii, Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imefanya Kikao Maalumu na Viongozi wa Dini lengo ikiwa kuhusisha kundi hilo maalumu katika kudhibiti matukio ya uhalifu ikiwemo mauaji, mmomonyoko wa maadili, matumizi ya dawa za...
Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha leo Mei 16, 2024 limepokea msaada wa pikipiki 20 toka benki ya CRDB kwa ajili ya kuimarisha usalama wa raia na mali zao katika Mkoa huo.
Akikabidhi pikipiki hizo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe; Paul Makonda amesema pikipiki hizo zimetolewa kwa Jeshi la Polisi ikiwa...
Tundu Lissu amejibu tuhuma zilitolewa dhidi yake kwamba anayoyasema kuhusu Rais Samia na mtoto wake Abdul kutoa pesa ili kuvuruga uchaguzi ndani ya CHADEMA.
Majibu hayo yamekuja baada ya member wa JamiiForums.com kuandika andiko likiwa na madai hayo
Pia soma: Inadaiwa hasira za Lissu...
CASHLESS ECONOMY-DIGITAL ECONOMY (Uchumi wa Kidijitali, matumizi ya fedha kielectroniki kwenye shughuli za kiuchumi).
Leo (16/05/2024) nimesimama Bungeni kuomba ufafanuzi kwa serikali, Katika Dunia ya sasa, uchumi umehamia kwenye mifumo (elekroniki) iwe kununua au kulipa au kupata huduma yoyote...
Serikali imesema kuwa taratibu za kikodi zimebainisha kwamba, mfanyabiashara yeyote mwenye mauzo ghafi yenye kiasi cha shilingi milioni kumi na moja (TZS 11,000,000) na kuendelea kwa mwaka, anapaswa kutumia mashine za kutoa risiti za kielekroniki (EFD) kwa walipakodi wote wanaofanya biashara...
Mbunge wa Buchosa, Eric James Shigongo amesema “Kuna hali mbaya sana kwenye Vyombo vya Habari labda kama Serikali imeamua vife ili wafanye mambo yao sawasawa, hakuna maendeleo bila Vyombo vya Habari.”
Ameyasema hayo wakati akichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na...
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kuhoji juu ya Mradi wa Serikali kupewa fedha nyingi kuliko bajeti iliyopangwa na kuripotiwa kutokamilika, ufafanuzi umetolewa
Mdau alitoa mfano kwa kupitia Bajeti ya Wizara ya Afya 2024/25 iliyosomwa bungeni Mei 14, 2024 ambapo Mradi wa Uimarishaji ya Hospitali...
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2023/24 NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2024/25
Upandishaji Vyeo
Mheshimiwa Spika, kuanzia Julai, 2023 hadi Aprili, 2024 Wizara imewapandisha vyeo jumla ya watumishi 9,397 katika ngazi mbalimbali za uongozi. Hali hiyo...
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 15, Kikao cha 27, leo Mei 16, 2024 ambapo pamoja na Maswali na Majibu, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye atasoma Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2024/25...
Serikali imesema kuwa zoezi la uthamini liliofanyika limebaini kwamba inahitajika jumla ya kiasi cha Tsh. Bilioni 11.3 kwa ajili ya kuwalipa wananchi waliokuwa kwenye eneo la karibu na uwanja wa ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro ambao unadaiwa kutanuliwa.
Akitoa taarifa hiyo mbele vyombo vya...
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili Nerbat Bwiga (33) mkazi wa Ifumbo na Isaya Zumba (38) mkazi wa Airport Songwe kwa tuhuma ya kupatikana na silaha bunduki moja aina ya Shotgun Pump Action bila kibali.
Akizungumza na waandishi wa habari Mei 15, 2024 Kamanda wa Polisi...
Foundation for Civil Society (FCS) na TradeMark Africa wamesaini makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa kuboresha mazingira wezeshi na jumuishi ya kibiashara kuhakikisha Wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wanajumuishwa kikamilifu katika uendeshaji wa biashara, kukabiliana na changamoto kubwa...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.