JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Leo, Machi 15, 2021 Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Tanzania ameanza ziara mkoani Tanga na akiwa kwenye kiwanda kimojawapo alichozindua kinachoshughulika na matunda wilayani Korogwe, alipata nafasi ya kusalimu wananchi baada ya kuombwa na mkuu wa mkoa wa Tanga ambapo alianza na salamu kutoka kwa Rais Magufuli "Kabla ya kuwapongeza niwasalimie salam za Rais anawasalimia, anasema tuendelee tuchape kazi, kipindi hiki tushikane tujenge mshikamano, tujenge upendo, tuchape kazi tulete tija kwa Taifa letu" Baada ya salam hizo Mama Samia amewapongeza kwa kuwa na kiwanda kwani ni mkombozi.
Mwananchi Digital imeripoti kuwa katika bandari ya Dar es Salaam kuna malori (magari makubwa ya mizigo) yamekwama kwa siku kadhaa hivyo kusababisha madereva wa maroli kulala na kuamka hapo hadi kufikia siku nne, madereva hao wamedai kulala na kula kwenye magari yao na kuomba kujisadia katika vyoo vya ofisi za jirani kwa kuwa hapo bandarini hakuna vyoo. Madereva hao wamedai chanzo cha uchelewashaji huo wa mizigo unatokana na ucheleweshwaji wa kupakua na kupakia mizigo na na ucheleweshwaji wa vibali vinavyoruhusu mizigo kusafirishwa.
Hayawi Hayawi sasa yamekuwa, ilianza kama kamchezo kakuigiza kutokupeana support za kupostiana kati ya Rayvan na wasanii wenzake wawasafi lakini utetezi ukawa mwingi, Ikafuata mama yake Boss wa Rayvan kumkatia Behewa Rayvan huko Instagram yaan Mama Dangote kumunfollow Rayvan. Zikaja Event zote kubwa za wasafi Ikiwepo EP ya FOA kutopostiwa na kijana huyo Shaban Mwakyusa Almaarufu kama Rayvan na Leo hii kaamua kukata Behewa kwenye Bio yake na kuondoa Taarifa iliyokuwa ikimtambulisha kama msanii wawasafi. Inasemekana Rayvanny kaondoka Wasafi. Hii ni kweli?
Hii ndio taarifa mpya iliyotufikia kwenye Jumatatu hii ya Pasaka , Kwamba Mheshimiwa Juma Raibu aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro , kabla ya kung'olewa hivi karibuni , ameanza kampeni kabambe ya kuondoa miundo mbinu yote aliyojitolea akiwa madarakani . Wakati wa madaraka yake alisaidia kutengeneza miundo mbinu ya maji kwenye uwanja wa Mandela uliopo Kata ya Pasua , ili kusaidia vijana wanaotumia uwanja huo , Sasa baada ya kung'olewa kwenye Umeya naye akaamua Kama Mmbwai basi iwe Mmbwai tu , kang'oa miundo mbinu yote ya maji aliyosaidia . Zipo Taarifa kwamba anapanga kung'oa mabati yote aliyosaidia kwenye mashule mbalimbali pamoja na Zahanati . Akijibu tuhuma hizo, Juma Raibu amesema: “Siwezi ondoa misaada...
Inasikitisha sana tunapoona viongozi waandamizi wa nchi hasa wabunge wakikubali kununua cheap doctorates kutoka vyuo vya kitapeli (rogue colleges). Hiyo inakupa picha kwamba hawa viongozi wetu hawajui hata kuangalia authenticity wakati kila kitu kipo online. Kwanza hiki sio chuo maana hakina address, hakina majengo na wala hakina makao makuu yanayoeleweka. Ni taasisi ya kijanjajanja tuu iliyoanzishwa na matapeli kwa ajili ya kuwatapeli watu wanaotaka umashuhuri nafuu hasa wa udaktari bila kutumia jasho Hiki chuo kilichowapa udaktari wa heshima Mbunge Musukuma na wenzake kina kashfa ya siku nyingi ya kuuza hizi degree za heshima. Ukweli ni kwamba wanauza na sio wanatoa bure ama kulingana na mafanikio uliyonayo katika nyanja husika...
Baadhi ya Halmashauri zimedaiwa 'kuwapiga' cha juu wasimamizi wa mitihani ya kidato cha nne inayoendelea hivi sasa. Kwa utafiti wangu usio rasmi wa kuwapigia watumishi wa Halmashauri tofauti tofauti, nimegundua kwamba kuna Halmashauri zingine zimewalipa wasimamizi siku 19, zingine zikalipa siku 14 na zingine zikalipa kwa siku msimamizi atakazoingia darasani kusimamia. Kwa mfano, kama shule ina mchepuo wa sanaa pekee na ratiba ni siku tano au saba basi wamelipwa kwa siku hizo. Kwanini siku za malipo zitofautiane? Malipo hayo yamegharamiwa na NECTA au kila halmashauri inalipa kulingana na uwezo wake?
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na iliyozua Maswali mengi na Taharuki ya Kiusalama Kawe ni kwamba Kijana Mmoja Dereva Bodaboda amejikuta matatani baada ya kutumwa kupeleka Barua yenye Ujumbe wa Tishio katika Kambi ya Jeshi ya Lugalo. Ilikuwa ni Siku ya Jumapili iliyopita ambapo Kijana huyo ( Dereva Bodaboda ) wa Kawe anayepaki katika Baa Maarufu ya HIPRO Kawe alipojikuta matatani na kuwa mikononi mwa JWTZ mpaka muda huu kwa Mahojiano zaidi. Ikiwa ni muda wa Saa 4 za Usiku Siku ya Jumapili akiwa amepaki Kituoni Kwao hapo HIPRO Bar Kawe alitokea Mtu Mmoja ambaye alimwomba Dereva 'Bodaboda' huyo ampelekee Barua Muhimu Getini Lugalo kilipo Chuo cha Tiba cha MCMS na amkabidhi Afande Luteni ( ninayemhifadhi ) kisha Kumkabidhi Hela ya...
Back
Top Bottom