KWELI Bodaboda atumwa barua yenye ujumbe wa kulipua Kambi ya Lugalo kati ya Novemba 20 hadi 27, 2021

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na iliyozua Maswali mengi na Taharuki ya Kiusalama Kawe ni kwamba Kijana Mmoja Dereva Bodaboda amejikuta matatani baada ya kutumwa kupeleka Barua yenye Ujumbe wa Tishio katika Kambi ya Jeshi ya Lugalo.

12-1024x683.jpg


Ilikuwa ni Siku ya Jumapili iliyopita ambapo Kijana huyo ( Dereva Bodaboda ) wa Kawe anayepaki katika Baa Maarufu ya HIPRO Kawe alipojikuta matatani na kuwa mikononi mwa JWTZ mpaka muda huu kwa Mahojiano zaidi.

Ikiwa ni muda wa Saa 4 za Usiku Siku ya Jumapili akiwa amepaki Kituoni Kwao hapo HIPRO Bar Kawe alitokea Mtu Mmoja ambaye alimwomba Dereva 'Bodaboda' huyo ampelekee Barua Muhimu Getini Lugalo kilipo Chuo cha Tiba cha MCMS na amkabidhi Afande Luteni ( ninayemhifadhi ) kisha Kumkabidhi Hela ya Ujira Tsh 5,000/= badala ya Tsh 2,000/= kwa Umbali wa kutoka hapo.

Kijana huyo Dereva Bodaboda akakubali na kuipeleka hiyo Barua alipoelekezwa huku aliyempa akitokomea zake Kusikojulikana.

Dereva 'Bodaboda' huyo alipofika Getini akakutana na Askari wa JWTZ na kuwaeleza kuwa ametumwa apeleke hiyo Barua hapo kwa huyo Afisa Luteni (ambaye namhifadhi ) ambapo kwa Uweledi mzuri na uliotukuka wa Askari hao pale pale wakamtaka Yule Kijana ( Dereva Bodaboda ) asiondoke Kwanza na pale pale alipokuwa amesimama aifungue na aisome kabla ya Wao Kuipokea na Kuipeleka alikokuwa ameelekezwa.

Ndipo Kijana ( Dereva Bodaboda ) akaifungua Barua hiyo na Kukuta imeandikwa hivi kama ambavyo KEROZENE naenda Kuinukuu hapa....JIANDAENI TUNAKUJA KULIPUA HAPO LUGALO KATI YA TAREHE 20 MPAKA TAREHE 27 MWEZI HUU NA TUTAWAUWA KAMA TULIVYOWAUWA WENZENU WAWILI.... mwisho wa Kuinukuu.

Hata hivyo tayari JWTZ limeshaanza Kuchukua hatua za Kiuchunguzi huku ikiendelea Kumhoji huyo Kijana baada ya kwenda nae wanakokujua huku Mitaa ya Kawe sasa ikifurika tu MP's wa JWTZ Lugalo, Watu wakikamatwa hovyo, Vijiwe vya Kahawa sasa havikaliki tena na Hofu pamoja na Uwoga ukitawala kwa Wakazi wengi.

Kwa pamoja tuiombee Tanzania yetu!
 
Tunachokijua
Taarifa za ndani zimethibitisha tukio hili.

Hata hivyo, uongozi wa Lugalo haukutaka kuzungumzia suala hilo kwa namna yoyote. Hatuna taarifa ya alipo kijana huyo aliyekamatwa.
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom