JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Huu Muungano ni chenga kabisa una kero nyingi mno, naona kwa Zanzibar wao ni raha kwenda mbele. Sisi wote ni Watanzania lakini ajabu Mtanganyika akienda Zanzibar endapo atahitaji kuendesha gari basi atatakiwa kuomba kibali maalum kinachotolewa na mamlaka za huko, vinginevyo utakuwa unavunja sheria. Hili suala halijakaa sawa kabisa, sawa na lile la kulipia kodi electronics kutoka Zanzibar, au Mzanzibar kumiliki ardhi Bara wakati Mtanganyika anawekewa vikwazo mfululu kumiliki ardhi Zanzibar. Huu Muungano ni wa kishenzi sana.
Wakati napitia pitia mitandaoni kutafuta style mpya kwa ajili ya shangazi yenu ndio nikakutana na hili bandiko kuwa aina ya kujamiiana huku mwanamke akiwa amemkalia mwanaume juu ('woman on top' or 'cowgirl' or 'reverse cowgirl'), hatari kwa afya ya mwanaume kwani hupelekea maumivu makali kwani hupekelea fracture ya uume kwa asilimia kubwa wakati wa kushiriki tendo la ndoa. Inashauriwa mwanaume ndio akae juu ili kupunguza uwezekano wa kupata madhara.
Nimeona mjadala kuhusu mihula anayoruhusiwa kugombea makamu aliyeshika madaraka ya Urais kutokana na kuchukua kiti katikati ya muhula baada ya Rais aliyekuwepo madarakani kushindwa kuendelea aidha kwa kufariki akiwa madarakani, kujiudhuru au sababu za kiafya. Mjadala umechagizwa na kauli ya Sophia Mjema aliyesema Rais Samia ni hadi 2035, huku wanaharakati wakipinga vikali kuwa hana sifa ya kugombea mihula miwili tena. Je, ukweli ni upi?
Aprili 27, 2023, akaunti ya Mtandao wa Twitter inayotumia jina la MainLandAfrica iliweka chapisho linalodai kuwa Bilionea wa Marekani Dan Friedkin amekodisha takriban Ekari 6,000,000 za ardhi nchini Tanzania. Chapisho hilo lilienda mbali zaidi kwa kudai kuwa Friedkin ni mmiliki wa Ekari zingine 25,000 za ardhi zinazounda pori la Akiba la Mwiba. Wanaojua kuhusu huyu jamaa watupe details anafanya biashara gani na ardhi kubwa kiasi hicho?
Inadaiwa huyu jamaa bhana enzi za utumwa, alitumika na masta wake kama mbegu ya kuzalisha watumwa wenye nguvu. Inadaiwa kutokana na kuwa na nguvu, umbo maridadi na urefu wa futi 7 hivyo masta wake alimpa upendeleo wa kipekee wa kumpunguzia majukumu mengi huku kazi yake kubwa ilikiwa ni kulala na kuwapa mimba wanawake mbalimbali ili waweze kumzalia masta wao watoto wenye nguvu ambao wangetumika katika shughuli za kitumwa. Roque Jose Florêncio aliacha idadi kubwa sana ya watoto.
Ingawa ni kama utani na inachekesha ila huwezi amini kuwa ng'ombe akijamba/kutoa ushuzi basi kile kitokacho huambatana na gesi ya methane ambayo huzalisha joto na moto/mwanga. Wanaharakati mbalimbali wa mazingira wamekuwa wakidiscourage ufugaji/uzalishaji wa ng'ombe kwa wingi na kusema wazi kuwa ushuzi wa ng'ombe huleta mabadiliko ya hali ya hewa, kwa sababu ng'ombe hutoa methane, gesi chafu inayohusishwa na ongezeko la joto duniani. Ng'ombe akiwa anajamba, ukiwasha njiti ya kiberiti moto unawaka kutokana na gesi ya methane. Ningependa kujua ukweli wa hili jambo.
Hii dunia ina vitu vya ajabu sana na vya kushangaza. Kuna historia baadhi unaweza unaweza kushangazwa nazo mojawapo ikiwa hii niliyopata kusimuliwa. Msitu wa Nyumbanitu una historia nyingi za kushangaza. Msitu huu upo katika Wilaya ya Wanging'ombe mkoa wa Njombe. Msitu huu nimepata kusimuliwa kuwa endapo mwanamke atakuwa kwenye siku zake basi hatoruhusiwa kuingia katika msitu huo, Ikiwa atakaidi basi akiingia kwenye huo msitu ndio utakuwa mwisho wake wa kuonekana maana atapotea mazima. Nadhani hili jambo mnaona linavyostaajibisha. Najiuliza huu msitu una nguvu na miujiza gani mpaka uweze kuwatendea hivyo dada zetu.
Miaka kadhaa nyuma niliwahi kusikia mwanamke mmoja nchini Uganda kajifungua watoto wawili (mapacha) wenye baba tofauti, hali hii ilinishangaza sana. Hali kama hii iliripotiwa pia Septemba 9, 2022 kwenye jarida la CNBC ambapo mwanamama mmoja kutoka Minerois, Brazil alithibitika kuwa na ujauzito wa mapacha ambao baada ya kupimwa DNA zao ilibainika kuwa walikuwa wa baba tofauti. Kisayansi, ni kweli kuwa jambo hili linaweza kutokea? Kama jibu ni ndio, linatokeaje?
Kijana wa miaka 29 aliushangaza ulimwengu kwa kitendo cha kikatili kisichokuwa na chembe ya utu. Inadaiwa baada ya kumpindua na kumuua Rais aliyekuwa madarakani William Tolbert, Samuel Doe alihakikisha anamaliza mizizi ya mtangulizi wake kwa kuua viongozi wote waandamizi. Inadaiwa Aprili 22, 1980 viongozi 13 walifikishwa ufukweni mwa bahari ya Atlantic nchini humo, wanaume hao 13 walikuwa nusu uchi ambapo walifyatuliwa risasi na vikosi vya Rais Samuel Doe. Kati ya waliouawa ni pamoja na Frank E. Tolbert ambaye alikuwa Kaka yake na rais Tolbert, na Rais wa Bunge la seneti. Picha: hali ilivyokuwa siku ya mauaji Muosha huoshwa, Rais Samuel Doe naye alikuja kupinduliwa na kuuawa kikatili sana na waasi.
Back
Top Bottom