Madeni Yanakutia Stress? Fanya Hivi...

Baada ya maradhi sugu, hakuna kitu kinachokosesha amani kama kuwa na madeni.

Hili jambo linatia stress ya hali ya juu mno.

Na mbaya zaidi ni kuwa stress hii inakufanya ushindwe ku focus kufanya vitu vyenye tija katika maisha yako kama kuendesha biashara yenye kukuingizia faida.

Muda wote huna raha.

Akili imejaa mawazo.

Simu zikipigwa, moyo unapiga pa!

"Nani tena huyo?"

Unaogopa kupokea simu za watu wanaokudai.

Unaanza kujenga tabia ya kusema uongo na kuwakwepa watu kadri uwezavyo.

Kiufupi unaishi maisha ya stress na ya ku pretend.

Kwa nje inawezekana watu wanakuona na nyumba nzuri, gari nzuri n.k.

Kumbe mali zote ni za kukopa. Majasho ya watu wengine.

Mbaya zaidi ni kuwa kila unavyojaribu kuondokana na hilo janga unajikuta unazama zaidi ndani ya shimo la madeni.

Umekuwa MTUMWA wa watu wengine!

Unajihisi dhalili mno kupita kiasa.

Sasa unafanyaje kuondokana na hili janga na kujenga utulivu wa moyo?

Unafuata hatua zifuatazo:
  1. Fahamu Chanzo cha Tatizo:
    Nusu ya utatuzi wa tatizo ni kuelewa chanzo cha tatizo. Watu wengi wanaolimbikiza madeni wanafanya hivyo kwa kutaka kuishi maisha yaliyokuwa juu ya uwezo wao.

    Unataka na wewe uonekane una nyumba na usafiri mzuri ili upate kuheshimiwa na washikaji zako.

    Huna kiwanja, na wala huna pesa za kununua kiwanja lakini unatamani kumiliki kiwanja.

    Unafanyaje?

    Unatafuta njia ya mkato.

    Unaenda benki kukopa pesa za kununua kiwanja pamoja na kujenga nyumba yako.

    Kama huna pesa leo za kununua kiwanja kitu gani kinakufanya uamini kuwa kesho utakuwa nazo?

  2. Elewa Mzunguko Wako wa Pesa:
    Kaa chini na upige mahesabu kwa kina kufahamu kiundani matumizi yako ya kila mwezi.

    Una mambo gani ambayo sio ya msingi yenye kupunguza kipato chako kila mwezi?

    Ukishaelewa, fuata hatua ya 3.

  3. Kata Gharama, Usiishi Maisha ya Uongo:
    Ukitaka kuendelea kuzama ndani ya shimo la madeni endelea kujidanganya.

    Kama kipato chako ni cha shs. 400,000 kwa mwezi huwezi kuishi maisha ya mtu mwenye kipato cha shs. 700,000 kwa mwezi.

    Utakuwa mwongo!

    Unatakiwa kuishi maisha ya mtu mwenye kipato cha shs. 300,000 kwa mwezi ili uwe na akiba ya shs. 100,000 kila mwezi.

    Kama hupendi hayo maisha fanya mkakati wa kuongeza kipato chako.

    Sio kukopa pesa na kuishi maisha ya uongo.

    Hakuna ulazima wa kumiliki gari kama huweza kumudua gharama zake.

    Uza gari na upande dala dala.

    Hakuna ulazima wa kuishi katika nyumba ya kodi ya shs. 400,000 kwa mwezi kama uwezo wako ni nyumba ya shs. 200,000 kwa mwezi.

    Fanya hivi kwa matumizi yako yote yasiyo ya muhimu hadi uwe unaokoa pesa kila mwezi.

  4. Panga Mkakati wa Kuongeza Kipato Chako:
    Baada ya kufanya hayo, kinachofuata ni kupanga mkakati wa kuongeza kipato ili uweze kulipa madeni haraka.

    Je unaweza kutafuta kazi ya ziada kuingiza kipato cha ziada?

    Je unaweza kutumia taaluma yako kutoa huduma fulani?
    (k.m. kama wewe ni mwalimu, je unaweza kufundisha tuition?)

    Je unaweza kutumia taaluma yako kuanzisha biashara kwa mtaji mdogo?

    Kaa chini na kalamu na karatasi na andika idea tofauti ya kuongeza kipato chako?

    Kama unahitaji msaada wa kupata wazo zuri la biashara kwa mtaji mdogo unaweza kuenda hapa: Wazo Fasta.

    ONYO! Usiendekeze fursa zenye kuahidi pesa za haraka bila ya kufanya kazi!

    Utaendelea kuzama katika shimo la madeni

  5. Panga mkakati wa kulipa madeni:
    Kama unaokoa kiasi fulani kila mwezi kutokana na kazi yako na unaingiza kipato cha zaida, utakuwa na dira nzuri ya kutokomeza madeni yako.

    Kama una maradhi ya kutosimamia pesa zako vizuri mweke mtu unayemuamini (kama mke wako au mume wako) kusimamia ulipaji wa madeni yako.

    Kila mwezi mkabidhi fungu la pesa kwa ajili ya kupunguza madeni.

    Andika listi ya watu/benki/taasisi zote zinazokudai pamoja na gharama zake.

    Wapigie simu watu wote wanaokudai na kuwaambia mkakati wako wa kumaliza deni lako.

    Waambie utakuwa unawalipa kiasi gani kila mwezi na tarehe ngapi hata kama ni kidogo namna gani.

    Hata kama hawatofurahi, waambie kuwa huo ndio uwezo wako.

    Wanaweza wasifurahishwe lakini kama kila mwezi wanaona pesa zinaingia watakuheshimu na wataacha kukusumbua.

    Hakikisha unawalipa kwa tarehe uliyowaambia na kama itatokea dharura wajulishe mapema. Kamwe usikubali yeye awe mtu wa mwanzo kukutafuta.

    Njia nzuri ya kutokomeza stress ya kulipa madeni ni kuanza kumlipa mwenye deni la chini yao ikisha ya juu yake na kuendelea.

    Ukifanya hivyo utapunguza watu wanaokudai kwa kasi kubwa na utakuwa una enjoy kulipa madeni kwani utajisikia furaha na amani ndani ya moyo wako.

    Kama unadaiwa na ma benki na taasisi, inamaanisha wanakata deni lao kwenye mshahara wako kila mwezi.

    Hakikisha una kipato cha ziada kumudu maisha yako ya kila siku hadi madeni yaishe.

  6. Jenga Nidhamu ya Kuhifadhi Pesa:
    Umaskini unatokana na nidhamu mbovu ya kutumia pesa ambazo huna.

    Utajiri unatokana na nidhamu nzuri ya kuweka akiba kwenye kipato kidogo unachopata na kutumia akiba hiyo katika biashara au uwekezaji kuzalisha pesa zaidi.

    Matajiri wengi waliishi maisha ya duni kabla ya kujulikana na jamii kuwa wao ni matajiri.

    Wamefanya hivyo kuhakikisha kila mwezi kuna akiba ya pesa ya ziada kwa ajili ya kuwekeza katika biashara yenye kumzalishia pesa.

    Acha kuishi maisha ya kujionyesha na focus katika kuzalisha uchumi wako.

Namwomba Mwenyezi Mungu akuondolee mtihani huu na akupe utulivu wa moyo.

Una swali? Uliza chini

Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako,

Dr. Said Said - Mkurugenzi online Profits
Asante sana
 
Kwanini usizalishe hela zako mwenyewe. Unashindwaje kutafuta hela zako mwenyewe hadi upande mgongo wa mtu mwengine?
Kiuchumi hili sio tatizo kutumia pesa za wengine au nguvubkazinya wengine kwa lengo la kuongeza tija.
Zingatia kutumia fedha za wengine katika namna itakayokufanya uoate faida nankuzirudisha kwa wakati
 
Nakubaliana na wewe kwa 100% ikiwa Unazungumzia business entity ya matajiri. Biashara zao ndio zenye kukopa sio wao. By definition tajiri hahitaji kukopa otherwise huyo sio tajiri.
 
Mkuu unakumbuka ulivyokula pesa yangu na kunidanganya kuhusu sumaku ya kunasa wateja na ukaseti matangazo na hayakuwa na impact?
Nilijua tu yaani,

Kuna mahali niliona kaweka link ya hiyo tovuti yake, eti anafundisha jinsi ya kuingiza hela mtandaoni

Kumbe ni sales funnel tu ya kuuza kozi,

Ni bora kuwa jambazi kuliko kuwa grifter kama hivi

Na hapa hata hajongelea kitu cha maana, ni mbinu ambazo mtu yeyote anaweza kuzifikiria

Red flags zipo kama zote;

Anaweka timer ya offer kuisha ndani ya muda mfupi ili ujisajili haraka
Screenshot_20240328-141310~2.png

Testimonials za mchongo ili umuamini
Screenshot_20240328-141431~2.png

Anataka ujisajili apate email yako aanze kuku-upsell mambo mengine akupige hela
Screenshot_20240328-141354~2.png

Eti hivi vyombo vya habari vimem-feature😆
1711625647588.png
 
Nilijua tu yaani,

Kuna mahali niliona kaweka link ya hiyo tovuti yake, eti anafundisha jinsi ya kuingiza hela mtandaoni

Kumbe ni sales funnel tu ya kuuza kozi,

Ni bora kuwa jambazi kuliko kuwa grifter kama hivi

Na hapa hata hajongelea kitu cha maana, ni mbinu ambazo mtu yeyote anaweza kuzifikiria

Red flags zipo kama zote;

Anaweka timer ya offer kuisha ndani ya muda mfupi ili ujisajili haraka
View attachment 2946926

Testimonials za mchongo ili umuamini
View attachment 2946938

Anataka ujisajili apate email yako aanze kuku-upsell mambo mengine akupige hela
View attachment 2946949
Asante mkuu,ni huyu. Chukueni tahadhari ndugu.
 
Hujajibu maswali yangu sasa unabadilisha topic. Jibu maswali yangu. Wewe ni nani, unafanya biashara gani na elezea exactly nimekutapeli vipi.
Wewe ni tapeli, umenitapeli kwa kuniuzia course useless na kunisetia matangazo ambayo hayajaleta matokeo kama ulivyo niahidi. Sumaku ya kunasa wateja mtandaoni ni mradi wa kitapeli, chukueni tahadhari.
 
Wewe ni tapeli, umenitapeli kwa kuniuzia course useless na kunisetia matangazo ambayo hayajaleta matokeo kama ulivyo niahidi. Sumaku ya kunasa wateja mtandaoni ni mradi wa kitapeli, chukueni tahadhari.
Nilijua tu yaani,

Kuna mahali niliona kaweka link ya hiyo tovuti yake, eti anafundisha jinsi ya kuingiza hela mtandaoni

Kumbe ni sales funnel tu ya kuuza kozi,

Ni bora kuwa jambazi kuliko kuwa grifter kama hivi

Na hapa hata hajongelea kitu cha maana, ni mbinu ambazo mtu yeyote anaweza kuzifikiria

Red flags zipo kama zote;

Anaweka timer ya offer kuisha ndani ya muda mfupi ili ujisajili haraka
View attachment 2946926

Testimonials za mchongo ili umuamini
View attachment 2946938

Anataka ujisajili apate email yako aanze kuku-upsell mambo mengine akupige hela
View attachment 2946949

Eti hivi vyombo vya habari vimem-feature😆
View attachment 2947006

Tunaishi dunia ya ajabu kama kutoa kozi 4 bure imekuwa utapeli.

Kwa vile unapenda kunifanyia marketing naomba uende na channel yetu ya YouTube ushare screenshot mahojiano ya wanafunzi wetu.

View: https://www.youtube.com/playlist?list=PLLOg8s26qj-YMos8or0O428soi_z0Poa8
 
Wewe ni tapeli, umenitapeli kwa kuniuzia course useless na kunisetia matangazo ambayo hayajaleta matokeo kama ulivyo niahidi. Sumaku ya kunasa wateja mtandaoni ni mradi wa kitapeli, chukueni tahadhari.
Kama kuniita tapeli itakupa usingizi mnono usiku hakuna shida. Endelea kuniita hivyo.
 
sounding too personal mdogo angu, just leave them alone.
As long as havunji sheria achana nae.
Au kama kumkosoa, mkosoe constructivelly.

Matangazo yq kampuni nyiing tu tena kubwa hayana uhalisia just like the guy do.

masuala ya matangazO na offers etc ni katika ku simplify the process of sales
Makampuni sawa tu

Ila huyu anauza kozi za kuingiza hela mtandaoni, ni tapeli.
 
Baada ya maradhi sugu, hakuna kitu kinachokosesha amani kama kuwa na madeni.

Hili jambo linatia stress ya hali ya juu mno.

Na mbaya zaidi ni kuwa stress hii inakufanya ushindwe ku focus kufanya vitu vyenye tija katika maisha yako kama kuendesha biashara yenye kukuingizia faida.

Muda wote huna raha.

Akili imejaa mawazo.

Simu zikipigwa, moyo unapiga pa!

"Nani tena huyo?"

Unaogopa kupokea simu za watu wanaokudai.

Unaanza kujenga tabia ya kusema uongo na kuwakwepa watu kadri uwezavyo.

Kiufupi unaishi maisha ya stress na ya ku pretend.

Kwa nje inawezekana watu wanakuona na nyumba nzuri, gari nzuri n.k.

Kumbe mali zote ni za kukopa. Majasho ya watu wengine.

Mbaya zaidi ni kuwa kila unavyojaribu kuondokana na hilo janga unajikuta unazama zaidi ndani ya shimo la madeni.

Umekuwa MTUMWA wa watu wengine!

Unajihisi dhalili mno kupita kiasa.

Sasa unafanyaje kuondokana na hili janga na kujenga utulivu wa moyo?

Unafuata hatua zifuatazo:
  1. Fahamu Chanzo cha Tatizo:
    Nusu ya utatuzi wa tatizo ni kuelewa chanzo cha tatizo. Watu wengi wanaolimbikiza madeni wanafanya hivyo kwa kutaka kuishi maisha yaliyokuwa juu ya uwezo wao.

    Unataka na wewe uonekane una nyumba na usafiri mzuri ili upate kuheshimiwa na washikaji zako.

    Huna kiwanja, na wala huna pesa za kununua kiwanja lakini unatamani kumiliki kiwanja.

    Unafanyaje?

    Unatafuta njia ya mkato.

    Unaenda benki kukopa pesa za kununua kiwanja pamoja na kujenga nyumba yako.

    Kama huna pesa leo za kununua kiwanja kitu gani kinakufanya uamini kuwa kesho utakuwa nazo?

  2. Elewa Mzunguko Wako wa Pesa:
    Kaa chini na upige mahesabu kwa kina kufahamu kiundani matumizi yako ya kila mwezi.

    Una mambo gani ambayo sio ya msingi yenye kupunguza kipato chako kila mwezi?

    Ukishaelewa, fuata hatua ya 3.

  3. Kata Gharama, Usiishi Maisha ya Uongo:
    Ukitaka kuendelea kuzama ndani ya shimo la madeni endelea kujidanganya.

    Kama kipato chako ni cha shs. 400,000 kwa mwezi huwezi kuishi maisha ya mtu mwenye kipato cha shs. 700,000 kwa mwezi.

    Utakuwa mwongo!

    Unatakiwa kuishi maisha ya mtu mwenye kipato cha shs. 300,000 kwa mwezi ili uwe na akiba ya shs. 100,000 kila mwezi.

    Kama hupendi hayo maisha fanya mkakati wa kuongeza kipato chako.

    Sio kukopa pesa na kuishi maisha ya uongo.

    Hakuna ulazima wa kumiliki gari kama huweza kumudua gharama zake.

    Uza gari na upande dala dala.

    Hakuna ulazima wa kuishi katika nyumba ya kodi ya shs. 400,000 kwa mwezi kama uwezo wako ni nyumba ya shs. 200,000 kwa mwezi.

    Fanya hivi kwa matumizi yako yote yasiyo ya muhimu hadi uwe unaokoa pesa kila mwezi.

  4. Panga Mkakati wa Kuongeza Kipato Chako:
    Baada ya kufanya hayo, kinachofuata ni kupanga mkakati wa kuongeza kipato ili uweze kulipa madeni haraka.

    Je unaweza kutafuta kazi ya ziada kuingiza kipato cha ziada?

    Je unaweza kutumia taaluma yako kutoa huduma fulani?
    (k.m. kama wewe ni mwalimu, je unaweza kufundisha tuition?)

    Je unaweza kutumia taaluma yako kuanzisha biashara kwa mtaji mdogo?

    Kaa chini na kalamu na karatasi na andika idea tofauti ya kuongeza kipato chako?

    Kama unahitaji msaada wa kupata wazo zuri la biashara kwa mtaji mdogo unaweza kuenda hapa: Wazo Fasta.

    ONYO! Usiendekeze fursa zenye kuahidi pesa za haraka bila ya kufanya kazi!

    Utaendelea kuzama katika shimo la madeni

  5. Panga mkakati wa kulipa madeni:
    Kama unaokoa kiasi fulani kila mwezi kutokana na kazi yako na unaingiza kipato cha zaida, utakuwa na dira nzuri ya kutokomeza madeni yako.

    Kama una maradhi ya kutosimamia pesa zako vizuri mweke mtu unayemuamini (kama mke wako au mume wako) kusimamia ulipaji wa madeni yako.

    Kila mwezi mkabidhi fungu la pesa kwa ajili ya kupunguza madeni.

    Andika listi ya watu/benki/taasisi zote zinazokudai pamoja na gharama zake.

    Wapigie simu watu wote wanaokudai na kuwaambia mkakati wako wa kumaliza deni lako.

    Waambie utakuwa unawalipa kiasi gani kila mwezi na tarehe ngapi hata kama ni kidogo namna gani.

    Hata kama hawatofurahi, waambie kuwa huo ndio uwezo wako.

    Wanaweza wasifurahishwe lakini kama kila mwezi wanaona pesa zinaingia watakuheshimu na wataacha kukusumbua.

    Hakikisha unawalipa kwa tarehe uliyowaambia na kama itatokea dharura wajulishe mapema. Kamwe usikubali yeye awe mtu wa mwanzo kukutafuta.

    Njia nzuri ya kutokomeza stress ya kulipa madeni ni kuanza kumlipa mwenye deni la chini yao ikisha ya juu yake na kuendelea.

    Ukifanya hivyo utapunguza watu wanaokudai kwa kasi kubwa na utakuwa una enjoy kulipa madeni kwani utajisikia furaha na amani ndani ya moyo wako.

    Kama unadaiwa na ma benki na taasisi, inamaanisha wanakata deni lao kwenye mshahara wako kila mwezi.

    Hakikisha una kipato cha ziada kumudu maisha yako ya kila siku hadi madeni yaishe.

  6. Jenga Nidhamu ya Kuhifadhi Pesa:
    Umaskini unatokana na nidhamu mbovu ya kutumia pesa ambazo huna.

    Utajiri unatokana na nidhamu nzuri ya kuweka akiba kwenye kipato kidogo unachopata na kutumia akiba hiyo katika biashara au uwekezaji kuzalisha pesa zaidi.

    Matajiri wengi waliishi maisha ya duni kabla ya kujulikana na jamii kuwa wao ni matajiri.

    Wamefanya hivyo kuhakikisha kila mwezi kuna akiba ya pesa ya ziada kwa ajili ya kuwekeza katika biashara yenye kumzalishia pesa.

    Acha kuishi maisha ya kujionyesha na focus katika kuzalisha uchumi wako.

Namwomba Mwenyezi Mungu akuondolee mtihani huu na akupe utulivu wa moyo.

Una swali? Uliza chini

Ni mimi mwenye kujali mafanikio yako,

Dr. Said Said - Mkurugenzi online Profits
Ongezea: mikopo ya bank unazuia watu kuzaliana,. Mdaiwa hana hamu ya kufanya mapenzi
 
Back
Top Bottom