Soma hapa ujue jinsi ya kujinasua kwenye mtego wa madeni ulionasa

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,090
22,374
Wakuu kwa sasa hali ilivyo ni kuwa watu wengi sana wamenasa kwenye mtego mbaya wa madeni na kujinasua imekuwa mtihani. Iwe mtu alikopa kwa sababu yoyote ile ni kwamba muda wa kudaiwa hakuna anayeonewa huruma. Aliyeomba mkopo wa biashara ikabuma anapata taabu sawa na aliyekopa mkopo akauhonga wote. Kwa uzoefu wangu wa maisha hawa ndo watu wanaofaa kuombewa sana kwa hali wanayopitia. Kudaiwa sio poa. Unaweza ukawa unakula ila haunenepi kwa stress. Sasa ukiwa kwenye hii hali ufanyeje? Nitashea nanyi uzoefu wangu binafsi katika hili kwa sababu hata mimi nimeshawahi kuwa mhanga wa hili jambo zaidi ya mara moja.

Kitu cha kwanza na cha muhimu sana ni kukubaliana na hali kwamba unadaiwa na ni lazima ulipe penda usipende. Yatazame madeni yako na yaorodheshe yote. Watu wengi hukwepa hii hatua kwa kuogopa kujua ukubwa wa tatizo huku wakisahau kwamba kupuuzia haitasaidia lolote. Bado hali itakuwa mbaya ukipuuzia.

Ukishakuwa kwenye madeni kitu cha kwanza ni kuhakikisha unapunguza matumizi yako na baadhi ya mambo kuachana nayo kabisa. Kiufupi ishi kulingana na kipato chako. Hii ya kukata matumizi na kuishi kulingana na hali yako sio utatuzi wa haraka ila itakusaidia kwa muda mrefu na inahitaji nidhamu na kujitoa sana.

Kutafuta chanzo kingine cha mapato ni njia inayoweza kukuondoa kwenye madeni haraka. Kila mtu ana kipaji, nguvu na akili alizojaliwa na Mungu kwahiyo ukiwa kwenye madeni tumia kila ulichojaliwa kujitafutia kipato kingine cha halali ili uongezee kwenye rejesho. Kama miaka 11 iliyopita niliingia kwenye mkwamo mbaya sana kiasi kwamba nilifikiria hata kujinyonga ila nikaamua nje ya kazi niliyokuwa ninafanya nifanye namna nifungue sehemu nifundishe pre-form one. Ingawa haikuwa rahisi ila kwa miezi mitatu nilipata hela iliyomaliza kama 95% ya madeni yangu. Hata miaka michache iliyopita baada ya biashara kuwa na kipato kidogo nilijikuta natenga muda nafanya kazi ya kujitolea kama mtu wa marketing kwenye kampuni fulani na kujiongezea kipato. Yaani kazi yoyote fanya ujiondoe kwenye mtego kwanza.

Na ukiwa kwenye madeni tafadhali sana jipe kipaumbele wewe. Achana na mambo ya kusaidia watu kwanza. Ishu za michango kaa nayo mbali. Jiokoe wewe kwanza. Hata wale wachungaji wanaosema weka sadaka kwenye bahasha tukuombee wakatae. Mungu anaona unayopitia kwahiyo ukiwa na imani atakuokoa sio kima yeyote kwa jina la mchungaji/nabii au mtume ndo atakusaidia. Wale wanaweza kukuingiza kwenye matatizo zaidi.

Nakaribisha tujadili hili.
 
Njia nyingine ni kurelax na kutotilia maanani kama umekosa.

Mdaiwi hana jinai wala hauliwi, Face wanaokudai kuwa bold na weka wazi kuwa huna umekosa mpaka nyakati fulan utakapopata
 
Deni letu ni himilivu, stahimilivu na tunakopesheka kukamilisha miradi ya Maendeleo.

kukopa inaongeza umakini,
Hupati usingizi hovyo hovyo...
unakua na machale na namba mpya zinazokupigia..
Unakua mtaalamu wa ahadi
Mbunifu sana wa mipango ya ukwepaji kulipa..
Mtu wa wasiwasi alie jawa na mawazo na kukosa amani kabisa n.k

Kopa kwa malengo na mipango,
dawa ya deni ni kulipa....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom