Fanya hivi usipofanikiwa niite mbwa nimekaa pale

Utajua wewe

JF-Expert Member
Feb 20, 2024
286
620
Fedha inatakiwa uwe na nidhamu nayo katika kuitumia. Kanuni ifuatayo imetumika kwenye vyanzo vyako vyote vya fedha ili uwe na mafanikio yenye amani.

Kanuni
•Fungu la kumi 10%
•Akiba 30%
•Matumizi 40%
•Dharura 10%
•Msaada 5%
•Sadaka 5
Jumla 100%

Hii kanuni inafanya kazi katika kila fedha unayopata kama pato lako la mwezi.

Mfano Kama unapata Sh. Laki 5 kwa mwezi (500,000/=) fungu la 10 ni Sh. 50,000/=, hii ni mali ya Mungu si yako. Unatakiwa utoe kanisani kila mwezi, pia hata kama umepewa fedha kama zawadi unapaswa uitolee fungu la 10.

Faida za Fungu la kumi
•Hulinda kazi au biashara unayoifanya dhidi ya adui.
•Magonjwa, ajali(vitu vitakavyokufanya utumie fedha bila mpangilio) n.k yanakuwa mbali nawe.

Akiba 30
•Fedha hii unaiweka kwa matumizi yako ya baadae kama kujenga, kusomesha, kulima, vitega uchumi n.k.
mfano kama pato lako kwa mwezi ni sh. 500,00/= asilimia 30 ni sh. 150,00/=

Matumizi 40
•Fedha hii itatumika kwa matumizi ya kila siku, chakula, maji, umeme n.k
•Hutumika pia kwa matumizi mengine ya starehe, mavazi n.k
•Kama pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/=, asilimia 40 ni sh. 200,000/=
angalizo matumizi yasizidi fedha hiyo.

Dharura 10
•Hii ni fedha unayotunza kwa ajili ya mambo usiyoyatalajia kama msiba, magonjwa au kukwama jambo lolote n.k.
•Kama pato lako ni sh. 500,000/= unatunza sh. 50,000/= kwa ajili ya dharura kwa mwezi.

Msaada 5%
•Hii ni fedha ya msaada kwa watu wenye shida; watoto yatima, wajane, walemavu n.k
• kama pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/= unatunza sh. 25,000/= kwa ajili ya msaada.

Sadaka 5%
•Kama pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/= tenga sh. 25,000/= kwa ajili ya sadaka kwa mwezi.
•Igawe fedha hii Mara 4 kwa sababu mwezi una jumapili 4 ambapo utapata ni sh. 6,250/=. Hivyo kila jumapili utaenda kutoa sh. 6,250/=.

Kumbuka;
Kitu chochote kinachoitwa sadaka kiombee kabla hujakitoa kama siku mbili 2 au 3 ndipo uitoe sadaka.
•Jaribu na anza hata na kidogo kidogo, kuwa na nidhamu ya fedha uone nayo itakavyokuheshimu.
NB:

#MAENDELEO HAYANA CHAMA#
 
Nimescreenshot shukrani ila nna swali..

Izo 15% za fungu la Kumi na sadaka inamaana wasio na imani zinaenda wapi? Pia umesema tutoe kanisani ulimaanisha na msikitini au waislam hawana?

Ila izo 85% nimezielewa. Nilitaka iyo 15% nikaongezee kwenye 85%
 
Nimescreenshot shukrani ila nna swali..

Izo 15% za fungu la Kumi na sadaka inamaana wasio na imani zinaenda wapi? Pia umesema tutoe kanisani ulimaanisha na msikitini au waislam hawana?

Ila izo 85% nimezielewa. Nilitaka iyo 15% nikaongezee kwenye 85%
Apo imeandika ivyo kutakana na imani yangu ila kama ni muislamu inabidi akatoe msikitini course pia wana zaka na taratibu zao
 
Back
Top Bottom