Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,507
- 8,132
Labda wameona wakopeshaji mtandaoni wamefanikiwa kwenye 'mkakati' wao wa kudai madeni. Binadamu huwa hatupendi kudhalilishwa hivyo na benki ya I & M wameamua kutumia mkakati huo huo kwa kuwatangaza wote wenye madeni sugu.
Hivi sheria inaruhusu kuanika taarifa za mtu binafsi kwa umma ama hawa wakenya wamepotoka? Na mchakato wa kukopa benki naamini una taratibu zake tofauti na mikopo ya mtandaoni ikiwemo kuweka dhamana, kwanini wasipambane na kuuza hizo dhamana!
Mbona NMB na CRDB huwa wanakubali matokeo ikitokea mikopo chechefu
=======
"Benki inapenda kuwataarifu wadaiwa wake pia kuwa, kukaidi taarifa hii kutachukuliwa kama kuridhia benki kuchukua hatua za ziada ikiwemo kutangaza jina lako na picha, kiasi unachodaiwa na/au kuchukua hatua Zaidi za kisheria dhidi ya mdaiwa, na/au wadhamini wa mikopo ili kuweza kurudisha pesa ulizokopa.
Benki ya I&M Bank Tanzania limited haitahusika na athari zozote zitakazotokana na matangazo ya taarifa za wadaiwa watakaokaidi taarifa /tangazo hili".
Mwananchi gazette