Taja madeni yako unayodaiwa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,770
45,358
Kuna watu madeni yanawatia stress wanashindwa hata kula wakiyawaza wanaishia kufakufa tuwasaidie kwa kuwatajia madeni yetu ili wajione Hawapo peke yao.

Nikianza na Mimi mwenyewe.

1. Mkopo wa BOT(hazina)kila mwez 160000
2. Mkopo NMB kila mwezi 120000
3. Nyangao credit 90000 kila mwez bado miez miwili nimalize
4. Mama mwenye nyumba kodi 240000 miez mitatu
5. MGODI VODACOM 70000
6. Dukani kwa Rashid 30000
7. Nipige Tafu 21000
8. Fundi Fulani 50000
9. Maji na umeme 15000
10. Mfanyakazi mwenzangu alinikopesha 20000
11. Kwenye Mabar huwa sina madeni Makubwa ni kama 25000

Mimi nayowadai watu ni kama laki na kitu.
 
Nadaiwa mpaka sioni cha ajab kuhusu madeni.

Yan kifupi nimeanza kufanana na deni so hata siogopi..honeatly sikumbuki ni mangapi ila mengi sana.

Kumudu kudaiwa ni kipaji sana. Sema tu hakikisha una afya, hii carreer haihitaji wagonjwa wagonjwa kama presha, moyo na kisukari..utakufa siku si zako
 
1. 1 M rafiki yangu ananidai nitampa februari mwezi huu aniache nipumue.

2. 26 K, nilipita kwa mangi nikachukua vitu, lipa kwa mpesa kwenda tigo pesa ikakataa, Mangi akaniambia nenda katoe utanipitishia, sijapita. Nikipita nitampa.

3. Fungu la kumi, huwa napeleka mahali, sijawa mwaminifu december mwishoni! 🤦🏻‍♀️ Mungu anisaidie nipeleke ndani ya siku 3 hizi.
 
Back
Top Bottom