Zaidi Ya Watumishi Hewa 17,100 Wafukuzwa Serikalini

Tumeeeeeeeechokaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Mtumishi 'hewa' unamfukuzaje sasa? Yaani unafukuza upepo?!!

Ghost spotting! Maajabu ni mengi nchi hii.

-Kaveli-
 
Mmmmhh.. uhakiki hauishi..? So watumishi kupanda vyeo ndio hakuna tena..? Jamani uhakiki wa miezi yote hii.? Rais Magufuli alisema itatumia mwezi mmoja na nusu au max. miezi 2 tu... sasa mbona hii hali inakuwa haieleweki... sbb muda unaenda, na umepita sana.. ndio nn hii..?
 
Serikali inatumia kiini macho cha watumishi kwa lengo la kuastisha ajira, na kuwanyima watumishi wa umma stahiki zao kama promotion, posho, n.k, mpaka sasa hatujaona faida ya kugunduliwa kwa watumishi hewa maana mishara ya kulipa wafanyakazi imepanda badala ya kupungua, Ni bora wawe wakweli kama wana ajiri au hawa ajiri, kwa kiini macho hiki cha watumishi hewa tayari serikali imeshapoteza baadhi ya wahitimu mhimu hasa Madaktari, walimu wa sayansi ambao wengi wameahatimkia nje na wengine wako private school....WATUMISHI HEWA NI KISINGIZIO CHA KUZUIA AJIRA MPYA.
 
ANGALIZO:

Mnapokuwa mnatizama News Bulletin zozote kama unajua huna uwezo wa kukariri au kushika kitu unachokisikia basi uwe una notebook yako pembeni na uwe unaandika kama kumbukumbu kwako la sivyo utakuwa unawapoteza Watanzania wote kwa uzushi. Siku nyingine try to be accurate Mkuu. Hajasema Watu 71000 kama ulivyotudanganya hapo katika bandiko lako bali kasema kwamba tokea mwezi March hadi September wamebaini Watumishi hewa 11,600 na ambao wameshawachukulia hatua za kuwafukuza Kazi ila zoezi la kuwabaini wengine bado linaendelea.

Halafu katika Kiswahili sanifu hakuna neno " amekili " bali kuna neno " amekiri ". Huwa sipendi kuona a very native Tanzanian anakosea ama kuzungumza au kuandika Kiswahili fasaha halafu Mimi " mgeni " tu tena kutoka nchini kwetu Rwanda nakijua vizuri mno hiki Kiswahili chenu na nakipenda sana kukizungumza na kukitumia katika kukiandika. Akhsante Mkuu na nimeona nikupe " makavu " yako " mubashara " kabisa.
Oooh kumbe wewe ni mkimbizi ninyi ndio mlipewa uraia Tabora Mwaka Jana eeh?
 
Tumeeeeeeeechokaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Usichoke mkuu maana ndiyo kwanza kazi imeanza. Nimeona kwenye updates za twitter za east Africa Radio kuwa Kairuki amesema sasa serikali inataraji kuanza kupitia upya mishahara ya watumishi wa serikalini.

Nadhani baada ya hapo wataanza kuhakiki na account za watumishi. Hivyo Mambo ya increments,Ajira na uhamisho yataanza mwakani panapo majaaliwa
 
Amesema kuwa zoezi la uhakiki lililoanza march hadi september mwaka 2016 limebaini watumishi hewa 17100 limeisababishia hasara serikali kubwa pia waziri simbachawe amekili kuwa zoezi la uhakiki wa watumishi hewa limechelewesha ajira mpya kwa kiasi kikubwa

======

Serikali imewabaini na kuwafukuza zaidi ya watumishi hewa 17100 katika kipindi cha miezi sita huku watumishi hao wakitajwa kunufaika na fursa mbalimbali ikiwemo kupata mikopo kwa njia zisizo za halali na kulisababishia taifa hasara kubwa.

Waziri wa nchi ofisi ya rais Menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mhe Angela Kairuki anatoa takwimu hizo za watumishi hewa katika hafla ya kuwaapisha wakurugenzi wapya wa halmashauri 13 walioteuliwa na rais John Magufuli hivi karibuni ambapo amesema kwa kipindi cha mwezi March hadi September idadi hiyo imebainika huku zoezi hilo likitajwa kuwa endelevu.

Kwa upande wake waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mhe George Simbachawene amesema kubainika kuwepo kwa watumishi hewa kumechangia kwa kiasi kikubwa kuchelewesha ajira mpya huku akionya baadhi ya watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kupotosha umma kuhusu ajira waache mara moja kabla hawajachukuliwa hatua

Nao baadhi ya wakurugenzi hao wapya baada ya kula kiapo cha maadili ya viongozi wa umma wamesema wamepokea uteuzi huo na wako tayari kufanya kazi kwa kuzingatia maagizo ya rais katika maeneo yao.

Chanzo: ITV
Watumishi hewa unawafukuzaje kazi?
 
ANGALIZO:

Mnapokuwa mnatizama News Bulletin zozote kama unajua huna uwezo wa kukariri au kushika kitu unachokisikia basi uwe una notebook yako pembeni na uwe unaandika kama kumbukumbu kwako la sivyo utakuwa unawapoteza Watanzania wote kwa uzushi. Siku nyingine try to be accurate Mkuu. Hajasema Watu 71000 kama ulivyotudanganya hapo katika bandiko lako bali kasema kwamba tokea mwezi March hadi September wamebaini Watumishi hewa 11,600 na ambao wameshawachukulia hatua za kuwafukuza Kazi ila zoezi la kuwabaini wengine bado linaendelea.

Halafu katika Kiswahili sanifu hakuna neno " amekili " bali kuna neno " amekiri ". Huwa sipendi kuona a very native Tanzanian anakosea ama kuzungumza au kuandika Kiswahili fasaha halafu Mimi " mgeni " tu tena kutoka nchini kwetu Rwanda nakijua vizuri mno hiki Kiswahili chenu na nakipenda sana kukizungumza na kukitumia katika kukiandika. Akhsante Mkuu na nimeona nikupe " makavu " yako " mubashara " kabisa.
Hata wewe data zako haziko sahihi, kasema 17100 ndio waliobainika bhana, nyani halioni kundule
 
Oooh kumbe wewe ni mkimbizi ninyi ndio mlipewa uraia Tabora Mwaka Jana eeh?

Sijaingia Tanzania mwaka jana bali tupo hapa Tanzania tokea mwaka 1922 hivyo nadhani kuniita Mimi " Mkimbizi " ni sawa na kuni " Juma Nyosso ". Niombe radhi haraka sana Mkuu kabla sijaanza kukukandamiza na " mabomu " yangu ya hatari ya " bunker busters ".
 
Wafanyakazi hewa halafu wamefukuzwa.
Imefukuzwa hewa ?
Reporter please
 
Hata wewe data zako haziko sahihi, kasema 17100 ndio waliobainika bhana, nyani halioni kundule

Sasa 11,600 yangu na hiyo 17100 zina umbali gani Mkuu? Jamaa kasema 71000 sasa ni nani hapo katulisha " matango pori " kiaina? Yaani kwa mfano ulio hai tu ni sawa sawa Waziri katamka Chalinze halafu Mimi nikatamka Mlandizi ila mwenzetu ( huyo aliyekosea ) yeye katamka Nkasi sasa kwa tathmini yako tu hapo ya haraka nani kidogo ana afadhali? Hivi Chalinze na Mlandizi kuna umbali? Sasa Nkasi unakujua jinsi kulivyo mbali? Huko ndiyo mwisho wa dunia Mkuu.
 
acha kujitetea hakuna kosa dogo
 
Hivi lile swali la wale wakurugenzi walioteuliwa julai kushika hizi nafasi wanazojaza hawa 13 walilishia wapi lilipata majibu?
 
Tulianza kwenye uhakiki wa mishahara hewa, kisha watumishi hewa nahisi huku tunakoelekea tutamalizia na utekelezaji wa ahadi hewa
 
Back
Top Bottom